Pascal Mayalla
Hakuna amsha amsha ni kutafuta umaarufu kwasababu maalumu, kuficha maouvu
Publicity unaoyoiona si kwa ajili ya chama ni kujisafisha akijua ananuka dhulma na mikono imejaa damu!
Huyu bwana anafahamu aliumiza Umma, hakuna alichokifanya kikafanikiwa isipokuwa kusimamia mabaya. Amejaza vijana mitandaoni wana post upuuzi ili umma usahau au afiche maovu aliyotenda zama zile
Pili, anafanya kazi bila kufikiri kwasababu tu ya kutafuta umaarufu. Si mara ya kwanza kumbuka!
Mfano, juzi kaambiwa kuna maiti imezuiliwa Hospitali ya Sekotoure.
Bila kuuliza au kuwasiliana na Hospitali, mwenezi akaagiza ambulance ikachukue mwili kwenda kuzika
Hospitali ni institution (Taasisi) inaongozwa kwa procedures na guidelines. Maiti kuzuiliwa kuna sababu.
Inawezekana kuna deni la matibabu linalopaswa kulipwa. Mambo ya hovyo kama haya yanaua taasisi kwasababu zinashindwa kujiendesha. Ndiyo yale ya amri za kutoa pesa za mwenge kwenye mashirika, yakafa
Ningemuelewa kama angesema atalipia gharama hizo , mwili utolewe.
Kutoa amri tu ni kukurupuka na kuitia taasisi hasara. Nani atafidia deni hilo kama lipo?
Unaweza kuona hajabadilika, ndio yale ya wanaume kutelekeza watoto, madawa ya kulevya mkoa mmoja kana kwamba Dar ni kisiwa n.k.
Hajui mipaka ya kazi au tofauti ya uenezi na u-RC wala hajui 'coordination and engagement''
JokaKuu