Wanabodi
Huu ni wito kwa Katibu Mwenezi mpya wa CCM, Comred Paul Makonda, kwanza kwa kumpongeza kwa kuifufua hamasa ya CCM kupendwa upya na kukubalika sana kupitia amsha amsha zake za Magufuli type (populist na populism) kila anapopita, tatizo lake ni moja tuu, anaipiga hii ngoma kwa nguvu mno, hivyo kuirindimisha kwa mlio mkubwa sana. Tatizo la ngoma inayovuma, ni ukiisikia ngoma inavuma sana, ujue inakaribia kupasuka!. Ili twende salama na kufika salama 2025, sisi watu wenye jicho la tatu, tunampa ushauri wa bure Mwenezi Makonda, twende taratibu mdogo mdogo ili tufike salama, kwa speed aliyoanza nayo, kama ataendelea kwa kasi hii, asije kushangaa hii ngoma ikampasukia njiani kabla hatujafika safari yetu!.
Rule No. 1. Never Outshine Your Boss
Mwenezi hawezi kumuagiza Waziri Mkuu na kuonya mawaziri, kwa kuwapa ultimatums!. Makonda aishie kwenye kusisitiza utekelezaji tuu wa ilani, na sio kutoa amri kuwaamuru na kuwaamrisha mawaziri!. Makonda hawezi kum summon Waziri Mkuu au mawaziri kwasababu yeye sio mamlaka yao ya uteuzi wala ya nidhamu. Mawaziri hawawajibiki kwa chama, wanawajibika kwa rais. iwapo kuna Waziri yoyote hajatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kikamilifu, chama kinamshitaki kwa rais ndie mamlaka pekee inayoweza kuwa summon na sio Mwenezi!. Waziri Mkuu wa JMT hawezi kupewa maelekezo ya chama na mwenezi kwasababu PM ni mjumbe wa CC ya CCM. Huwezi kuwapigia simu mawaziri na kuwapa maelekezo kwasababu wewe sio rais wa JMT. Magufuli alikuwa anafanya hivyo kwasababu yeye ndio bosi wao!, Makonda asijifanye Magufuli!, huku ni kumu outshine his boss!.
Konda Boy ana overdo bila kujua!. Asioverdo ngoma ikipigwa sana, huwaga haichelewi kupasuka!.
Wito huu ni kwa wanaomtakia mema Paul Makonda na ili kulithibitisha kuwa tunamtakia mema, angalia tumeanza nae wapi.
Mimi nilianza nae hapa
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Nikaja hapa
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
Alipopitia misukosuko tukasimama nae kwanza kwa kutoa wito
Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... kisha tukamshauri
Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .
Kuna watu wenye roho za kwanini tukawaambia
Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!
Na mwisho nikapendekeza
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...
Hivyo mheshimiwa sana Mwenezi Makonda, twende taratibu mdogo mdogo, hii duniani ni tambara bovu, tembea nayo taratibu!.
Wish you all the best
Kakayo
Paskali