Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!

Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!

Pascal Mayalla

Hakuna amsha amsha ni kutafuta umaarufu kwasababu maalumu, kuficha maouvu
Publicity unaoyoiona si kwa ajili ya chama ni kujisafisha akijua ananuka dhulma na mikono imejaa damu!

Huyu bwana anafahamu aliumiza Umma, hakuna alichokifanya kikafanikiwa isipokuwa kusimamia mabaya. Amejaza vijana mitandaoni wana post upuuzi ili umma usahau au afiche maovu aliyotenda zama zile

Pili, anafanya kazi bila kufikiri kwasababu tu ya kutafuta umaarufu. Si mara ya kwanza kumbuka!

Mfano, juzi kaambiwa kuna maiti imezuiliwa Hospitali ya Sekotoure.
Bila kuuliza au kuwasiliana na Hospitali, mwenezi akaagiza ambulance ikachukue mwili kwenda kuzika

Hospitali ni institution (Taasisi) inaongozwa kwa procedures na guidelines. Maiti kuzuiliwa kuna sababu.

Inawezekana kuna deni la matibabu linalopaswa kulipwa. Mambo ya hovyo kama haya yanaua taasisi kwasababu zinashindwa kujiendesha. Ndiyo yale ya amri za kutoa pesa za mwenge kwenye mashirika, yakafa

Ningemuelewa kama angesema atalipia gharama hizo , mwili utolewe.
Kutoa amri tu ni kukurupuka na kuitia taasisi hasara. Nani atafidia deni hilo kama lipo?

Unaweza kuona hajabadilika, ndio yale ya wanaume kutelekeza watoto, madawa ya kulevya mkoa mmoja kana kwamba Dar ni kisiwa n.k.

Hajui mipaka ya kazi au tofauti ya uenezi na u-RC wala hajui 'coordination and engagement''

JokaKuu
Vile mwili wa marehem sio ndugu yako mkuu.tumesikiliza wote aliyetoa ombi kasema mwil umekwama unadaiwa mil 2 utoke. Imetoka ambulance kwend kubeba sasa hapo procedure gani zaid ya kwend kulipa na ni kitu ambacho kimefanyika maana hueez kwend kubeba mwili bila kulipa gharama za matibabu. Hivi sisi huwa tuna shida gani
 
Wanabodi

Huu ni wito kwa Katibu Mwenezi mpya wa CCM, Comred Paul Makonda, kwanza kwa kumpongeza kwa kuifufua hamasa ya CCM kupendwa upya na kukubalika sana kupitia amsha amsha zake za Magufuli type (populist na populism) kila anapopita, tatizo lake ni moja tuu, anaipiga hii ngoma kwa nguvu mno, hivyo kuirindimisha kwa mlio mkubwa sana. Tatizo la ngoma inayovuma, ni ukiisikia ngoma inavuma sana, ujue inakaribia kupasuka!. Ili twende salama na kufika salama 2025, sisi watu wenye jicho la tatu, tunampa ushauri wa bure Mwenezi Makonda, twende taratibu mdogo mdogo ili tufike salama, kwa speed aliyoanza nayo, kama ataendelea kwa kasi hii, asije kushangaa hii ngoma ikampasukia njiani kabla hatujafika safari yetu!.

Rule No. 1. Never Outshine Your Boss
Mwenezi hawezi kumuagiza Waziri Mkuu na kuonya mawaziri, kwa kuwapa ultimatums!. Makonda aishie kwenye kusisitiza utekelezaji tuu wa ilani, na sio kutoa amri kuwaamuru na kuwaamrisha mawaziri!. Makonda hawezi kum summon Waziri Mkuu au mawaziri kwasababu yeye sio mamlaka yao ya uteuzi wala ya nidhamu. Mawaziri hawawajibiki kwa chama, wanawajibika kwa rais. iwapo kuna Waziri yoyote hajatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kikamilifu, chama kinamshitaki kwa rais ndie mamlaka pekee inayoweza kuwa summon na sio Mwenezi!. Waziri Mkuu wa JMT hawezi kupewa maelekezo ya chama na mwenezi kwasababu PM ni mjumbe wa CC ya CCM. Huwezi kuwapigia simu mawaziri na kuwapa maelekezo kwasababu wewe sio rais wa JMT. Magufuli alikuwa anafanya hivyo kwasababu yeye ndio bosi wao!, Makonda asijifanye Magufuli!, huku ni kumu outshine his boss!.

Enzi za Nyerere na Mwinyi, mfumo wa utawala wa taifa letu ulikuwa ni mfumo wa Party Supremacy, ambapo chama ndio kulikuwa kimeshika hatamu kuongoza serikali, hivyo viongozi wa serikali walikuwa na kofia mbili, wakuu wa mikoa ndio viongozi wa CCM wa mkoa na waliingia Bungeni. Kulikuwa mpaka kuna mkoa wa majeshi!, jeshi lilikuwa ni Idara ya chama na kulikuwa na ma kamisaa wa chama jeshini.

Mwaka 1992 tulipoingia mfumo wa vyama vingi, huo ndio ulikuwa mwisho wa party supremacy na kofia mbili, chama ni chama na serikali ni serikali, siasa ikaondolewa jeshini. Kofia mbili zilikuja kubaki kwa rais tuu wa JMT.

Tulianza mfumo wa Parliamentary Supremacy ambapo CCM kinatoa ilani ya uchaguzi kwa serikali kuitekeleza, Bunge ndio linaisimamia serikali.

Ufuatiliaji wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ndio kazi ya Mwenezi, lakini utaratibu wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa ilani ya CCM kwa serikali ni kwa mtindo wa "Eyes on Hands Off", kwa CCM kufuatia utekelezaji kwa eyes on, hivyo hiki anachokifanya Mwenezi Paul Makonda kufuatia utekelezaji wa ilani ndio kazi yake rasmi kwa kuona kwa macho na kuzungumza na wananchi, na watekelezaji wa ngazi ya chini, kuhusu kero zao mbalimbali.

Baada ya kuona na kusikia hatua za utekelezaji wa ilani, zinafuatiliwa kupitia vikao vya CCM kuanzia shina, tawi, kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi taifa, mwenezi taifa anapaswa kupokea taarifa za waenezi wenzake toka chini, kuyaandika na kuyapeleka kwenye vikao vya rasmi vya chama kitataifa na kule ndipo chama kinajadili na kutoa maelekezo ambapo kazi ya Mwenezi ni kuyatangaza maamuzi na maelekezo ya chama kwa watendaji wa serikali na sio Mwenezi kutoa maagizo na ultimatum kwa watendaji wa serikali akiwemo Waziri Mkuu na mawaziri, hiyo sio jukumu la Mwenezi ni jukumu la mamlaka yao ya uteuzi na nidhamu ambayo ni Rais wa JMT.

Sehemu ambapo Konda Boy anajichanganya ni kwa vile Rais Samia ndie Mwenyekiti wa CCM, na yeye ndie msemaji wa CCM, anatoa maagizo kwa viongozi wa serikali, akiwemo Waziri Mkuu na mawaziri ikiwemo kuwapa ultimatums kutoka kwa Rais Samia kama Mwenyekiti wa CCM, wakati Rais Samia anaweza kutoa maelekezo na ultimatums kwa watendaji wa serikali kama Rais wa JMT na sio Mwenezi kuivaa kofia ya rais wa JMT na ku summons mawaziri na kuwapa ultimatums akiwemo Waziri Mkuu!. That is wrong!. Huku ni ku overstepping over and above mamlaka yake, ni Rais wa JMT pekee ndie mwenye uwezo to summon ministers na kutoa ultimatums kwa Waziri Mkuu and not anyone else!. Hata Bunge haliwezi kum summon Waziri Mkuu na kumpa ultimatums bali linaweza kufanya hivyo kwa serikali.

Konda Boy ana overdo bila kujua!. Asioverdo ngoma ikipigwa sana, huwaga haichelewi kupasuka!.

Wito huu ni kwa wanaomtakia mema Paul Makonda na ili kulithibitisha kuwa tunamtakia mema, angalia tumeanza nae wapi.

Mimi nilianza nae hapa Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Nikaja hapa Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
Alipopitia misukosuko tukasimama nae kwanza kwa kutoa wito Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... kisha tukamshauri Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .
Kuna watu wenye roho za kwanini tukawaambia Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!
Na mwisho nikapendekeza Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...

Hivyo mheshimiwa sana Mwenezi Makonda, twende taratibu mdogo mdogo, hii duniani ni tambara bovu, tembea nayo taratibu!.

Wish you all the best

Kakayo

Paskali
Rule No. 1. Never Outshine Your Boss

Rule No. 2. You Must Observe Rule No. 1
 
Vile mwili wa marehem sio ndugu yako mkuu.tumesikiliza wote aliyetoa ombi kasema mwil umekwama unadaiwa mil 2 utoke. Imetoka ambulance kwend kubeba sasa hapo procedure gani zaid ya kwend kulipa na ni kitu ambacho kimefanyika maana hueez kwend kubeba mwili bila kulipa gharama za matibabu. Hivi sisi huwa tuna shida gani
Na huko Hospitali ya Handeni amefariki mama mjamzito kwa kukosa pesa ya kufanyiwa operesheni ili atolewe mtoto!
Wanaona pesa ni zaidi ya uhai wa mama na mwanaye !!
Makonda fuatilia hiyo ya Handeni bado ni ya moto moto !!
 
Vile mwili wa marehem sio ndugu yako mkuu.tumesikiliza wote aliyetoa ombi kasema mwil umekwama unadaiwa mil 2 utoke. Imetoka ambulance kwend kubeba sasa hapo procedure gani zaid ya kwend kulipa na ni kitu ambacho kimefanyika maana hueez kwend kubeba mwili bila kulipa gharama za matibabu. Hivi sisi huwa tuna shida gani
Rudi kasilikilize ile clip kwa umakini

Msemaji anasema '' Tumepata misiba miwili...............na kijana mmoja mwili upo mortuary zinahitajika milioni 2 na laki moja pale Sekoutoure'' Maana yake zinahitaji pesa ili kutoa mwili Hospitali, si kusafirisha mwili

Makonda anatoa amri ambulance ikachukue mwili bila kuwasiliana na taasisi husika ambayo ni Sekoutoure.
Kuna uwezekano yapo malipo yanahitaji, hakuna shida kama angesema atalipia , alichofanya ni kutoa amri kwa Taasisi au Hospitali kutafuta umaarufu na si suluhu ya jambo.

Leo kuna uwezekano Hospitali imeruhusu mwili, lakini je huo ndio utaratibu?

Kwa kiongozi anayejua wajibu, kuwajibika na taratibu za kazi jambo la kwanza lilikuwa kuwasiliana na Hospitali kufahamu tatizo ni nini, halafu atoes suluhu siyo kukimbilia 'toa ambulance ' na bla bla . Huo si uongozi ni ukurupukaji
 
Namshauri Ndugu Makonda afuatilie issue iliyotokea Hospitali ya wilaya ya Handeni ya yule mama mja mzito aliyepoteza maisha eti tu nduguze hawakuwa na pesa shs 150,000/- ili afanyiwe operesheni !

Hiyo issue itamuinua juu sana Makonda !! Hapa kazi tu! Na kazi iendelee !!
Hili ni suala la Wizara ya Afya siyo Makonda!

Makonda ni mwenezi tu yaani mpiga projo, hana mamlaka yoyote isipokuwa kwa wasiojua.
Hawezi kumwajibisha hata mfagizi wa Hospitali katika sakata hilo.
 
Sehemu ambapo Konda Boy anajichanganya ni kwa vile Rais Samia ndie Mwenyekiti wa CCM, na yeye ndie msemaji wa CCM, anatoa maagizo kwa viongozi wa serikali, akiwemo Waziri Mkuu na mawaziri ikiwemo kuwapa ultimatums kutoka kwa Rais Samia kama Mwenyekiti wa CCM, wakati Rais Samia anaweza kutoa maelekezo na ultimatums kwa watendaji wa serikali kama Rais wa JMT na sio Mwenezi kuivaa kofia ya rais wa JMT na ku summons mawaziri na kuwapa ultimatums akiwemo Waziri Mkuu!. That is wrong!. Huku ni ku overstepping over and above mamlaka yake, ni Rais wa JMT pekee ndie mwenye uwezo to summon ministers na kutoa ultimatums kwa Waziri Mkuu and not anyone else!. Hata Bunge haliwezi kum summon Waziri Mkuu na kumpa ultimatums bali linaweza kufanya hivyo kwa serikali.
Utaambiwa uwaziri Mkuu wake unatokana na kukubalika kwa Ilani y CCM kwa wananchi kisha wananchi kuweka CCM madarakani, Na CCM kutengeneza Serikali, na serikali kuundwa huku Waziri Mkuu akiwa ndiye mtendaji Mkuu wa serikali hiyo chini ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama.

Kwa kifupi Chama kipo juu ya serikali!!
Na Makonda anakisemea Chama. Anaye"summon" si Makonda bali ni Chama.

Binafsi, sijamsikia Makonda anasema ninakuagiza, bali anasema Chama kinakuagiza...!!!

Hata hivyo, Nina uhakika 100% unayajua haya mleta mada.
 
Leo kuna uwezekano Hospitali imeruhusu mwili, lakini je huo ndio utaratibu?
Binafsi, napenda utaratibu ufuatwe, sikufurahishwa na kupanda "roli la mchanga" ambalo ni la mizigo si la kubeba watu. Vinginevyo, awe amepewa Kibali na askari wetu wa barabarani.

Hata hivyo, ieleweke Makonda anakisemea Chama, Chama ndicho kinaisimamia serikali, na Serikali ndiyo inasimamia hizo Taasisi zilizoagizwa na Chama kupitia msemaji.
 
Rudi kasilikilize ile clip kwa umakini

Msemaji anasema '' Tumepata misiba miwili...............na kijana mmoja mwili upo mortuary zinahitajika milioni 2 na laki moja pale Sekoutoure'' Maana yake zinahitaji pesa ili kutoa mwili Hospitali, si kusafirisha mwili

Makonda anatoa amri ambulance ikachukue mwili bila kuwasiliana na taasisi husika ambayo ni Sekoutoure.
Kuna uwezekano yapo malipo yanahitaji, hakuna shida kama angesema atalipia , alichofanya ni kutoa amri kwa Taasisi au Hospitali kutafuta umaarufu na si suluhu ya jambo.

Leo kuna uwezekano Hospitali imeruhusu mwili, lakini je huo ndio utaratibu?

Kwa kiongozi anayejua wajibu, kuwajibika na taratibu za kazi jambo la kwanza lilikuwa kuwasiliana na Hospitali kufahamu tatizo ni nini, halafu atoes suluhu siyo kukimbilia 'toa ambulance ' na bla bla . Huo si uongozi ni ukurupukaji
Mkuu Nguruvi3, Konda Boy ni action oriented man, wananchi wanachotaka sio maneno, wanataka vitendo, actions, Konda Boy anafanya actions, hivyo kuwapa wananchi wanachotaka!, kiukweli CCM imekuja juu!.

Kwa CCM, hii ni sifa!, angalia nilisema nini kumhusu Makonda na sifa hii Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... nilisema
Wanabodi,

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea Magufuli ile 2025, kiukweli kabisa Tanzania itanyooka!.

Paskali.
Makonda ni populist leader anatumia system ya utawala ya populism kwa kuwa ni pragmatist anafanya pragmatism, na hiki ndicho wananchi wanachotaka, hivyo Makonda anawapa wananchi wanachotaka, CCM inazidi kupendwa na kupaa!.

P
 
Vile mwili wa marehem sio ndugu yako mkuu.tumesikiliza wote aliyetoa ombi kasema mwil umekwama unadaiwa mil 2 utoke. Imetoka ambulance kwend kubeba sasa hapo procedure gani zaid ya kwend kulipa na ni kitu ambacho kimefanyika maana hueez kwend kubeba mwili bila kulipa gharama za matibabu. Hivi sisi huwa tuna shida gani
Huyo ni mnafiki marehemu akishafariki kinachofuata ni kuzika mwili wake! Hapo mwananchi anaomba msaada ili mwili ulipiwe ukazikwe! Mwenezi kama chama akasema hilo limekwisha kwa maana anaenda kulipia na ambulance ilikuwepo hapo hapo kwenye msafara wake! Unafiki wa wabongo walitaka sijui atoe maelekezo gani ili kuonesha anafata utaratibu!
 
Vile mwili wa marehem sio ndugu yako mkuu.tumesikiliza wote aliyetoa ombi kasema mwil umekwama unadaiwa mil 2 utoke. Imetoka ambulance kwend kubeba sasa hapo procedure gani zaid ya kwend kulipa na ni kitu ambacho kimefanyika maana hueez kwend kubeba mwili bila kulipa gharama za matibabu. Hivi sisi huwa tuna shida gani

Roho mbaya zimetutawala.
 
Binafsi, napenda utaratibu ufuatwe, sikufurahishwa na kupanda "roli la mchanga" ambalo ni la mizigo si la kubeba watu. Vinginevyo, awe amepewa Kibali na askari wetu wa barabarani.

Hata hivyo, ieleweke Makonda anakisemea Chama, Chama ndicho kinaisimamia serikali, na Serikali ndiyo inasimamia hizo Taasisi zilizoagizwa na Chama kupitia msemaji.

Bado nimebaki kushangaa inakuwaje magwiji wa Siasa humu JF Kama mzee Nguruvi kushindwa kuelewa mtiririko mwepesi Kama huu?!

Ni kwamba kumbukumbu ya Mwenezi wa CCM 2010 mpaka 2014 imeshaondoka vichwani mara hii?

Ni lini mbwa alipanda juu ya mti bila kupandishwa?
 
Hili ni suala la Wizara ya Afya siyo Makonda!

Makonda ni mwenezi tu yaani mpiga projo, hana mamlaka yoyote isipokuwa kwa wasiojua.
Hawezi kumwajibisha hata mfagizi wa Hospitali katika sakata hilo.
Polical mileage huwa inatafutwa kwa namna yeyote ile !!
Yetu macho na masikio !
Ngoja tuone !!
 
Back
Top Bottom