Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!


Kweli Paskali...Ngoma ikilia sana hupasuka. Na mbwembwe ziwe na kiasi na staha.
 
mara aingie na baiskeli, mara aingie na fuso, na hizo simu za maagizo sasa mawaziri wanabidi waitikie tu..
kweli makonda ni" content creator"
ila kwa shangwe anazopewa na wanaomsikiliza kwenye mikutano yake ni wazi tatizo kubwa kwa wananchi wetu ni elimu.. haya maigizo wengi wanayafurahia na kusema makonda ni magufuli mpya, mtetezi wa wanyonge na mkombozi... hahahaah aisee hii nchi inahitaji miaka mingine 60 ndo tuupate uhuru halisi, hichi kizaz kilichokosa elimu kipite kije kizazi kipya ambacho angalau kila raia ana ka elimu ka form 4 na diploma kanakomuwezesha kupambanau mambo na kujui kipi ni fiksi na kipi ni uhalisia.

swali la kujiuliza, ccm imetawala yenyewe tangu uhuru, leo unaposema unatetea wanyonge, unawatetea wanyonge dhidi ya nani? aliyewaacha kwenye umaskini na unyonge ni nani? anayeifisadi nchi na kutowajibika ni nani? aliyeshindwa kutatua migogoro tangu uhuru ni nani?
yan ccm hyohyo ikupige halafu ccm hyohyo ikupe pole, na leso ya kufuta machozi.
ndo maana nasema yote ni maigizo, mpaka wananchi tutapoamua kila uchaguzi kupima hoja na kuchagua chama chochote, hapo tutakuwa tumejikomboa na tutaheshimiwa na hawa tunaowachagua, lakin huu ushabiki wa mkumbo tutaendelea kuwa watumwa, kulipa kodi ili wao na wenza wao walipane mishahara na posho.
 


Mtu anaenda ongea na Marehemu huku analia, halafu anasema yeye ni Mkristo, mambo ya aibu haya.
 
TUjikite zaidi ni kwenye mada za makonda kuliko kuzungumzia mtu asiyehusika .Mwisho wa siku hilo nyomi halimkumpa kura aliyekuwa na nyomi ya kweli si ndio maana yako!
 
Na baada ya kupora uchaguzi dhamira ikawa inamhukumu akaamu kufa
 
Yaani watu wanashangilia kudanganywa kama watoto wa chekechea
 
Katibu mwenezi siyo msemaji wa chama
Kazi yake ni kueneza sera za chama siyo kutoa maagizo na amri kwa mawaziri na waziri mkuu
 
Nilikua sijakuelewa


Nko nafatilia Hotuba zake muda Huu .


Kwa aina ya Viongozi wetu Afrika, anachofanya Makonda ni kizuri Sanaa Sanaa, ila Kwa watu watamfitinisha na Mkuu wa Nchi ionekane kama Makonda ,anataka kua na umaarufu mkubwa kuliko Mkuu wa Nchi
 
Never outshine your boss!.
Mwenezi ni No. 7 kwenye hierarchy ya chama, ana mabosi 6 juu yake M/Kiti, M/Kiti Bara, M/Kiti ZnZ, KM, NKM Bara, NKM ZnZ ndipo anakuja Mwenezi!.
P
 
Well said. Sasa mjomba wangu P, mbona keshaharibu? Kuvua GAMBA hakuibadili NYOKA ilivyo. Kwetu sie WATOTO wa MWL (RIP GENIOUS), huyu jamaa hapiti kwenye chujio la sifa za KIONGOZI tunaemtaka. Kwanza ni narcissist, less endowed kichwani kutokana ba tamshi zake mwenyewe, rude, ... na huenda kama ni kweli, KATILI sana. Mtu unajimwambafy hadi kukosa adabu madhabahuni kweli? Rejea alivohuzuria msiba wa Mzee Mengi, kwangu mimi Bibamu (RIP). Uongozi sio mchezo wa kitoto (tunaita 'kushoiya') !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…