Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!

Watu wengi hawaelewi hoja ya amri ya kuchukua mwili i.

Kutoa amri mwili uchukuliwe Hospitali ulikouzuiliwa ni kukiuka taratibu.

Hospitali ilizuia mwili kwasababu si kwa vile tu inataka. Ikiwa marehemu anadaiwa ni wajibu wa Familia kulipia na kama Makonda anawalipia kama mtu binafsi au chama hilo halina tatizo.

Kutoa amri kwa taasisi ni kuidhoofisha i. Milioni 2 za kufidia amri ya makonda zitalipwa na nani?

Pili, utaratibu ni kumpigia simu mkuu wa Hospitali. Tumeona JPM , SSH , Majaliwa wakiwa katika mikutano hawatoi amri hadi wanapowasiliana na Waziri. Makonda hakuwasiliana na uongozi wa Sekotoure na hilo ni kosa

Tukiendelea ujinga wa Makonda ipo siku atatoa amri Mzazi afanyiwe operesheni mtoto atolewa tumboni haraka

Kwani mumesahau ni Makonda huyu huyu alitoa amri Wanaume walazimishwe kupima Tezi Dume! Think about that
Hajui hata mipaka ya haki za binadamu wala haki za Raia , yeye anatoa amri tu.

Si huyu Makonda alianzisha vita ya madawa ya kulevya kwa DSM peke yake.
Yaani unawezaje ku control madawa katika mkoa mmoja wa Tanzania. Haya ni matoke ya amri.

Sasa anapanda Malori ambayo kwa utaratibu si chombo cha usafiri. Anaendesha piki piki bila helmet n.k.

Hoja ya uenezi; ni mwenezi wakiitwa ' Propaganda and mass mobilization'' yaani uhamasishaji na uenezi.

Hii si kazi ya serikali ni ya chama. Kusimamia serikali si kuropoka hovyo, ni kuisimamia kwa taratibu.

Kwamba anawasiliana na serikali kwa utaratibu na si yeye kuwa Mganga mkuu wa Hospitali ya sekotoure majukwaani
 
Hapo kinachotafutwa ni political mileage tu ! Come what may !😅🙏
 
Mkuu Nguruvi3, Konda Boy ni action oriented man, wananchi wanachotaka sio maneno, wanataka vitendo, actions, Konda Boy anafanya actions, hivyo kuwapa wananchi wanachotaka!, kiukweli CCM imekuja juu!.
Wananchi wanataka vitendo, lakini ni wajibu wa viongozi kufuata taratibu
Makonda si mganga wa Hospitali ya Sekotoure, alichotakiwa ni kuwasiliana na Hospitali ajue kwanini mwili umezuiwa.

Baada ya hapo ndipo angeweza kuchukua action kulingana na habari alizopewa na Hospitali iwe kulipia mwenyewe au CCM kulipia au vinginevyo. Deni la Hospitali lazima lilipwe ili Hospitali iendelee kutoa huduma

Mfuko wa Bima unakufa kwasababu ya mismanagement kama hizi. Mashirika ya umma yalikufa kwasababu hayakuendeshwa kibiashara, yaliendeshwa kwa amri za chama enzi hizo.
Zamani kulikuwa na Wenyeviti wa Chama katika kila taasisi kuanzia jeshini, Hospitali, Mashirika ya umma n.k.

Mambo yalikuwa ya amri kutoka kwa wenyeviti wasiojua abcd , mwisho wa siku mashirika yakafa

Kwa nchi zilizoendelea hata Rais hawezi kumwingia mfagiaji eneo lake la kazi. Kwamba kila mtu ana nafasi yake
Sasa huyu bwana anapojigeuza ni Mganga mkuu wa Hospitali ya Sekoutoure ni msiba kwa Taifa

Kumbukeni huyu bwana aliwahi kutoa amri ya Wanaume kupimwa tezi Dume! mkiacha aendelee na amri bila taratibu ipo siku atato amri wazee wenye mabusha wafyekwe haraka, Wanawake wenye mimba wapasulie haraka tuwe na watoto wa kutosha. This is dangerous !

JokaKuu
 
Sukuma Gang.
 
Umeniwahi kumpa Ushauri ,tena nilitaka nisema kwamba mama angesubiria jirani na uchaguzi wa 2024 ndio amteue ila Sasa anaweza vuma baadae wakamzoea.

But akimlaiza ziara huko Mara anatakiwa akae afanye tathmini hata miezi 3 au 4 baadae analimsha tena Kwa Kanda so Hadi ndani ya mwaka akilimaha mara 4 inatosha sana.
 
Yaani ukitaka kujua kuwa CCM walishaishiwa miaka mingi ni hizi hoja hapa. Hivi Bashite ana credibility gani hata za kusimama jukwaani?. Mmeamua kuleta wahuni ili kuimarisha uhuni.
Wanaojua ana Credibility kiasi gani ndio wamemuweka hapo alipo!, Mimi na wewe hatuna Mandate ya kupima Credibility ya mtu!
 
Anachokifanya ndio Chama kilitarajia na kilihitaji kwa sasa
Anayejuwa namna ya kudeal na Ccm ni Tundu Lisu peke yake, sasa ndio namuelewa Lisu.

Huwezi kufanya maridhiano na wahuni, wanahubiri amani huku wameshika mapanga.

Ili kuthibitisha uhuni wao utasikia Olw Sabaya ameteuliwa.

Makonda na Sabaya mikono yao imejaa damu, kitendo cha mama kumrudisha Makonda kwenye system ni dharau kwa Watanzania.

Ccm si watu wa kuwaamini, Lisu ndio anaijuwa namna sahihi ya kudeal na Ccm.
 
Makonda na Sabaya mikono yao imejaa damu, kitendo cha mama kumrudisha Makonda kwenye system ni dharau kwa Watanzania.
Hawa wanaoleta nyuzi za kumpamba kwa upande mwingine wanamhujumu
Tutafukua makaburi na kutonesha vidonda

Tangu aondoke RC Viroba coco beach vimeisha
Watu kupotea kama akina Roma hakuna tena
Hatusikii ya akina Mo
Watu ''kujinyonga'' kwa chupi au t-shirt hatusikii

Huyu bwana na genge lake walifanya uhalifu dhidi ya ubinadamu,mikono imejaa damu wanapmua dhulma na uhalifu

Aliyetuthibitishia hayo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM ambaye sasa ni DC.
Huyu alisimama mbele ya Camera na kuomba radhi Watanzania kwa makosa waliyofanya
 
Ahaaaa
 
To the contrary;
Makonda anathibitisha kuwa chini ya CCM, na Serikali yake, kilichotapakaa nchi nzima ni DHULUMA na UNYANG'ANYI.
Katika umati wa watu wanaomfuata Makonda, sijasikia mtu hata mmoja akinyosha mkono na kumwambia Mwenezi wa Chama Tawala jinsi Watanzania wanavyoneemeka chini ya CCM.
Wote wanalalamika jinsi wanavyoteseka na kudhulumika katika nchi hii inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi.
Kama Wapinzani wana muono sahihi, Makonda ni msaada mkubwa sana kwao.
Makonda ataiumiza sana CCM mwisho wa siku.
I hope the Opposition is smart enough to take advantage of this rare opportunity.
 
Kweli
 
Hongera mkuu
Hongera mkuu wewe ni mchambuzi na maandishi makini sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…