Huu uzi wa kujifariji ila Mama Samia ni rais hadi 2030.
Tumuombee uzima tu. Hakuna namna ambayo Mama Samia kama mgombea urais kupitia CCM akashindwa na Lissu au mgombea mwingine yeyote. Na CCM kumkataa mwenyekiti wao na rais ambaye bado yuko madarakani HAIWEZEKANI ndo maana CCM iliamua Rais ndo awe mwenyekiti pia. Kumletea figisu mwenyekiti ni jambo hatari zaidi kwa mwanaCCM endapo atagundulika.
CCM haikubaliki mijini tu lakini hana vijijini siyo kama inakubalika ila huwa hakuna vyama Mbadala. Nimetembea vijiji vingi sana Tanzania. Ukiondoa kilimanjaro, Arusha na mbeya mikoamingine yote mijini CDM wanawanachama na wafuasi wengi lakini vijijini hakuna watu kabisa.Na sababu kubwa ya vijijini kutokubalika ni sababu ya hofu kwasabu vijijini watu wote huwa wanajuana kwahiyo ukiwa mpinzani ni rahisi kushughurikiwa. Kwa misingi hiyo Bado si rahisi sana CDM kufanya vizuri chaguzi hizi zinazokuja, mijini watapata kura nyingi na viongozi wengi ila vijijini wasahau
Utafiti wako ni fake na wa uongo..
Mimi niandikapo hapa naishi kijijini hasa, mkoa wa Shinyanga maeneo ya vijiji vya Shirima - Shinyanga vijijini..
CHADEMA ndiyo mpango mzima na ina wafuasi wengi balaa kuliko unavyojaribu kudanganya hapa..
CCM ilishaharibu kote mijini na vijijini.
Ndiyo maana ya ushenzi, upumbavu na ujinga uliofanywa na polisiCCM Mbeya juzi na jana kupiga watu na kuzuia kongamano la vijana - BAVICHA kwa sababu ya HOFU YA CCM KUKATALIWA na wananchi..
Wangekuwa wanajua kuwa wanakubalika na kuungwa mkono sana vijijini na hivyo wana kura za kutosha, wangeiacha CHADEMA ya mjini ifanye shughuli zake za kisiasa na wao CCM wawekeze huko vijijini kama wanadhani wanakubalika..!
Ushahidi mwingine uliowazi kabisa ni ziara ya juzi kati hapa ya Tundu Lissu (Makamu Mwenyekiti - CHADEMA) katika kanda ya kati ya kichama yenye mikoa ya Singida, Dodoma na Morogoro..
Alitembelea vijiji vingi mfano Singida ni vijiji vya Shelui, Ibaga, Mwangeza vilivyoko wilaya ya Iramba na Mkalama nk.
Uliona wanakijiji waliokuwa wanajitokeza na kuonesha mwamko na support kwa CHADEMA kuonesha kabisa kuwa wameshachoka na CCM..?
Ndiyo maana nakuambia utafiti wako ni wa uongo na fake kabisa. Na pengine hata hujui mwenendo wa siasa za Tanganyika bali unatumia hisia za kizamani kujiandikia chochote..