President Samia on a panic mode

President Samia on a panic mode

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Baada ya kumalizana na kina January, Nape, Makamba, Kikwete na kufuatiwa na kujiuzulu kwa M/Mwenyekiti CCM Kinana ambao wangekuwa msaada wake wakati wa uchaguzi, msaada mkuu uliobaki kwake ni kulitumia jeshi la polisi kuwatisha wanaoonekana kuwa wapinzani wake waliobaki.

Kuna hofu kuu 3 zilizo mbele yake kwa sasa ambazo ni, 1. Tetesi ya Tundu Antipas Lissu kugombea, 2. Womanism(Gender) na 3. Nationalism (Origin).

Uhalisia; wanawake wengi huwa hawapendani watakuchekea usoni, wataambatana nawewe kwenye kampeni lkn ukifika wakati wa kuchagua watamchagua Mwanamme. Kwa mila na desturi za Mwafrika ni nadra sana kuongozwa na mwanamke, hili hata vitabu vya dini vimetamka wazi. Hiki kitakuwa kigezo muhimu hasa mpinzani wake akiwa Mwanamme.

Kitu kingine ambacho nakiona ni hofu kwake ni Origin yake (Mzanzibari), ukubali ukatae wakaazi wa Tanzania Bara (Tanganyika) ni wengi kuliko wa Zanzibar, hivyo wakati wa uchaguzi hiki kitakuwa kigezo kingine hasa mpinzani wake akitoka upande wa Bara.

Lissu kwa vyovyote vile atagombea ni threat nyingine. Drama zote zilizofanywa na polisi lengo sio kuwatisha wananchi bali ni kumtisha Lissu asigombee. Samia na CCM wanajua Lissu huwa hakopeshi watawajibu nini wananchi Lissu atakapowauliza kwanini kauza Bandari, kwa nini kauza Loliondo.

Tetesi tunazozipata mtandaoni kuwa kukubalika kwake ni chini ya 32% sio za kubeza ukizingatia hali halisi ya maisha waliyonayo wananchi walio wengi.

Sababu hizi ndizo zinamfanya Samia na CCM wawe na hofu ya uchaguzi.

1723671049062.png

Quinine, an independent thinker.
 
Bado ana chance
Mfano,

Msajili kulazimisha vyama vyote vya siasa kuweka mgombea urais kutoka Zenj na lazima awe mwanamke...

Hii unaweza kutumika kama njia ya kudumisha umoja wa kitaifa, na kuzingatia jinsia katika demokrasia.

vyama vyote vinaweza vikaelekezwa hivyo kwa amri au vifutwe.

Hilo ni tobo tu nawasanua😂
 
Baada ya kumalizana na kina January, Nape, Makamba, Kikwete na kufuatiwa na kujiuzulu kwa M/Mwenyekiti CCM Kinana ambao walikua msaada wake wakati wa uchaguzi..
Hilo la kutokukubalika ndiyo itakuwa kigezo kikuu kutokushinda uchaguzi ukiwa huru na haki.

Watanzania walikuwa wanamkubali mwanzoni.Lakini sasa hakubaliki na watanzania walio wengi.
 
Angeilinda heshima yake kama angekubali kuwa yeye alikuwa ni Rais wa mpito kuelekea Rais atakayechaguliwa na umma. Sasa amejawa na tamaa, na kuamini anaweza kuchaguliwa, wakati kwa muda mfupi amefanya madudu mengi ikiwemo kupora rasilimali za nchi kwa maslahi yake binafsi, wanafamilia na marafiki zake waliowezesha uharamia wa kuporwa kwa rasilimali za Tanganyika.
 
Sio kweli wakati wa Mtume Muhammad(SAW),walikuwako wanawake viongozi kam Bi Khadija,Bi Aisha,Fatma Zahrah.Wanaume wengi walikwenda kujifunza uidlamu kupitia wanawake hawa.Na vile vile Mtume Muhammad alifanyakazi,chini ya Bi Khadija,kabla ya kuwa mkeww na baada ya kuwa mkewe.Vile vile katika uislsmu mamake Yesu,,Maryam(Mariya),nimwanamke bora kuliko wanawake wote.
Tumuulize FaizaFoxy na Malaria 2 kama kwenye utawala wa sharia mwanamke anaweza kuwa kiongozi au amiri jeshi??
 
Mjadala Wa hovyo sana huu. Hivi Samia ashindwe kwa tume ipi ya uchaguzi? Kura za nani zitakazohesabiwa za kumuondoa Samia madarakani. Polisi gani atakayesimamia vituo vya uchaguzi kuwazuia CCM kufanya wanavyotaka?

Samia labda akataliwe na CCM wenzie lakini siyo kwenye sanduku la kura. Tena, kwa taarifa yenu, kutokana na hizo kasoro mlizosema anazo, cjui, mwanamke, mzanzibar, ameuza Loliondo na Bandari, mnampa hasira tu za kushinda kwa kishindo kikuu km Kagame. Mana ni kuamua tu ngapi zitangazwe.

Atangatazwa ameshinda kwa 99.9% ili kuwafunga midomo watu waliofikiria hatachaguliwa na CCM itatamba vibaya kwa ujambazi huo ktk uchaguzi. Mnaishi humu humu na hamuoni hali iliyopo, tena ni ya muda mrefu tu?
 
Baada ya kumalizana na kina January, Nape, Makamba, Kikwete na kufuatiwa na kujiuzulu kwa M/Mwenyekiti CCM Kinana ambao walikua msaada wake wakati wa uchaguz...
Kumbe ndiyo maana Polisi katika hili sakata la Mbeya target yao ilikuwa Tundu Lissu kwa vile wanajua mwili wake umejaa vyuma wakimkanyaga kanyaga watakuwa wamemaliza kile kiporo chao cha Dodoma.
 
Huu uzi wa kujifariji ila Mama Samia ni rais hadi 2030. Tumuombee uzima tu. Hakuna namna ambayo Mama Samia kama mgombea urais kupitia CCM akashindwa na Lissu au mgombea mwingine yeyote. Na CCM kumkataa mwenyekiti wao na rais ambaye bado yuko madarakani HAIWEZEKANI ndo maana CCM iliamua Rais ndo awe mwenyekiti pia. Kumletea figisu mwenyekiti ni jambo hatari zaidi kwa mwanaCCM endapo atagundulika.
 
Baada ya kumalizana na kina January, Nape, Makamba, Kikwete na kufuatiwa na kujiuzulu kwa M/Mwenyekiti CCM Kinana ambao walikua msaada wake wakati wa uchaguzi, msaada mkuu uliobaki kwake ni kulitumia jeshi la polisi kuwatisha wanaoonekana kuwa wapinzani wake waliobaki.

Kuna hofu kuu 3 zilizo mbele yake kwa sasa ambazo ni, 1. Tetesi ya Tundu Antipas Lissu kugombea, 2. Womanism(Gender) na 3. Nationalism (Origin).

Uhalisia; wanawake wengi huwa hawapendani watakuchekea usoni, wataambatana nawewe kwenye kampeni lkn ukifika wakati wa kuchagua watamchagua Mwanamme. Kwa mila na desturi za Mwafrika ni nadra sana kuongozwa na mwanamke, hili hata vitabu vya dini vimetamka wazi. Hiki kitakuwa kigezo muhimu hasa mpinzani wake akiwa Mwanamme.

Kitu kingine ambacho nakiona ni hofu kwake ni Origin yake (Mzanzibari), ukubali ukatae wakaazi wa Tanzania Bara (Tanganyika) ni wengi kuliko wa Zanzibar, hivyo wakati wa uchaguzi hiki kitakuwa kigezo kingine hasa mpinzani wake akitoka upande wa Bara.

Lissu kwa vyovyote vile atagombea ni threat nyingine. Drama zote zilizofanywa na polisi lengo sio kuwatisha wananchi bali ni kumtisha Lissu asigombee. Samia na CCM wanajua Lissu huwa hakopeshi watawajibu nini Lissu atakapowauliza kwanini kauza Bandari, kwa nini kauza Loliondo.

Tetesi tunazozipata mtandaoni kuwa kukubalika kwake ni chini ya 32% sio za kubeza ukizingatia hali halisi ya maisha waliyonayo wananchi walio wengi.

Sababu hizi ndizo zinamfanya Samia na CCM wawe na hofu ya uchaguzi.

Quinine, an independent thinker.
Mkuu

Uelewa wangu huru was duru humu jamvini ni kwamba:-

Dola,CCM,nchi,Ulimwengu wa kiroho ( mbinguni na kuzimu) ulipanga kwamba mtajwa ashike kwa muda tu yaani hata 2025 asifike aje mwingine na akifika aachie kijiti Ili wenye mamlaka waweke wa kwao!!

Sasa mtajwa akaona Bora aendelee Ili atimize malengo nadhani no binafsi sio ya wenye mamlaka!

Hapo kumeibua vita isiyo koma Hadi pale wenye mamlaka watakapofanikiwa lengo lao kuu waliojiwekea iwe peace full au bloodshed kivyovyote vile malengo yao yatimie!!

Sasa sisi tuone nani mshindi wa haya mapambano japo tunajua tutaathirika directly au indirectly!!

Coz nilimsikia mmoja akisema

"Nchi IPO salama mikononi mwa mama"alirudia karibu mara nne kwenye speech yake ,nikajua Kuna tatizo mahalo sio bure!!!

Kwani ni lini nchi imekua "sio salama "!!?Hadi asisitize hivyo!!?
 
Huu uzi wa kujifariji ila Mama Samia ni rais hadi 2030. Tumuombee uzima tu. Hakuna namna ambayo Mama Samia kama mgombea urais kupitia CCM akashindwa na Lissu au mgombea mwingine yeyote. Na CCM kumkataa mwenyekiti wao na rais ambaye bado yuko madarakani HAIWEZEKANI ndo maana CCM iliamua Rais ndo awe mwenyekiti pia. Kumletea figisu mwenyekiti ni jambo hatari zaidi kwa mwanaCCM endapo atagundulika.
Kuna Mungu
 
Back
Top Bottom