Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Hahaaaa!!!!huyu ni The Greatest
 
We acha tu mkuu,nchi zao ni jangwa lkn huwez sikia hawana chakula wala shida ya maji.
Hapa tunachojua ni mapambio tu,mijitu mizima inatetea matumbo yao
Watu wa Misri, Libya, Tunisia, Morocco wakija tanzania wakaona tuna uhaba wa maji au umeme watashangaa sana tuna akili gani.
 
Hiyo benki ya kilimo ni kama pambo la kisiasa tu it is not efficient at all.

Kwa bahati mbaya sana hakuna administration hata moja ambayo imechukulia kilimo kwa uzito wake wakati ndio shughuli ambayo inafanywa na 80% ya watanzania.

Hakuna efforts za kihakikisha kuwa tunahifadhi mbegu zetu asilia ukiachana na hizi za kizungu wanazotuletea ambazo ukishapanda mara moja huwezi irudia tena.
 
Anashangazwa na waziri kuzunguka kuchukua kero za wananchi wakati Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya wapo huko. Anasema labda sababu ni kupata posho tu.
Hapo yuko juu ya mstari, labda watu wengi watadharau lakini haingii akilini kuona kama mfumo haufanyi kazi hadi mtu mwenye cheo cha kisiasa anazurura mitaani kutatua kero.
 
Inawezekana sehemu kubwa ya nchi yetu watu wake wana uwezo mdogo sana kiakili na kufikiri kwa logic.
Sahihisha sentence yako, ni viongozi wenye uwezo mdogo sana wa akili lakini baada ya kukalia viti wametunga sheria kuhakikisha hawatoki madarakani. Wanadhibiti vyombo vya ulinzi na usalama, tume ya uchaguzi na bunge.
 
Hv unadhn nn tatizo????
 
Ikitokea chama cha siasa kikakomaa na hoja ya kilimo na wakulima, kitaing'oa CCM mapema asubuhi.
Huwezi kuing'oa meli ya CCM huku nanga za vikosi vya ulinzi na usalama, tume ya uchaguzi na bunge zimekita chini.
 
Viwanda havikuachwa na wakoloni, vilijengwa na Nyerere, vikauzwa na Mkapa.
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ila huyu mzee basi tu kichwa kweli kweli! Alipaswa kuwa mshauri wa raisi na tungesogea
 
Ishu ya kuwa na mabwawa kila wilaya ni muhimu sana ili kuwa na kilimo cha uhakika kila mwaka!
 
Hili suala la mawaziri kuzunguka mikoani mfano stendi za mabasi kukakugua tiketi lidhibitiwe kupunguza matumizi ya serikali hasa kipindi hichi ambapo kuna mjadala mkali kati ya kukopa zaidi au kuongeza tozo.

Tatizo la hii nchi ni wizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…