Jambazi amekufa lakini vijizi bado vipo, hata huko digital wataiba tu braza, hawa wezi ili kuwaondoa tunahitaji katiba mpya na tume huru na shirikishi
 
Mimi nilishachukua uamuzi huu mgumu tangu mwaka 2019 wakati wa lile sekeseke la wabunge na madiwani wa upinzani kuunga mkono juhudi, na pia wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Bila Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, kamwe sitapoteza muda wangu kupiga kura ambayo haita heshimiwa. Bora nibaki tu nyumbani nikiangalia tv.
 

Point kubwa hapo ni uchaguzi huru na haki, hapigi kura kwasababu kura yake haina thamani....yaani pia usipige matokeo lazima fulani ashinde ndio maana yake...
 
Nchi inahitaji mabadiliko ya mfumo mzima wa Uchaguzi,kila mwenye akili anajua ule wa 2020 ulikuwa uchafuzi
 

Labda useme tu hutaki huo mfumo wa kidigitali, lakini sio upigaji. Kwa hapa kwetu upigaji upo wazi bila hata huo mfumo.
 
Ana bahati jiwe kafa angethubutu kusema kipind mzee upo mda si mrefu angeambiwa ajisalimishe central
 
Yes ni kweli kabisa lakini pia ni rahisi zaidi ku monitor kuliko haya maboksi.
Watu hawaelewi! Wanakwambia bora mabox na mabegi tu..

Hawajui kupitia server maalumu yenye firewalls za uhakika (wataalamu wapo wanaelewa haya mambo) kama itakuepo ni rahisi ku monitor kuliko mabox na mabegi ya wizi wa kura..
 
Naunga mkono hoja
 
Sema labda aseme kuwe na uwazi na Uhuru hata zikija digitali Kama hamna uwazi wataiba Tena kirahisi zaidi
Achana kabosa na kitu kinaitwa digital yaan computet ndio inahesabu kura apo km huna ma computer engineer utaiba wapi labda utumie ujinga kuiba wazwaz
 
Aah kweli watu walikuwa wamebeba mengi vifuani mwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…