PreGE2025 Prof. Eginald PAN Mihanjo: CCM ijiandae kuwa chama cha upinzani

PreGE2025 Prof. Eginald PAN Mihanjo: CCM ijiandae kuwa chama cha upinzani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
25 Aprili 2025


View: https://m.youtube.com/watch?v=wbk2XLS77j8
Ushindi haupatikani kwa kutegemea 'chawa' wala wingi wa kadi. Watu wana kadi na mapenzi kwa vyama hata vitatu. CCM iwe makini wanatakiwa wasiwe na mazoea.

CHADEMA kimekaa muda mrefu kama chama cha siasa, sasa kimekuja kivingine kama MOVEMENT / VUGUVUGU 2025

anasema Prof. Mihanjo na anadadavua kwa kina :
  • 2015 CCM ilikuwa ipotee
  • Kanda ya Ziwa ilibeba CCM chini ya JPM
  • Rais wa sasa aliyeingia kwa ajali, awe makini sana
  • Rais aliyepo atapitia wakati mgumu March 2025 - June 2025
  • No Reforms No Election ni Hoja kubwa sana
  • Wapinzani wasiiache No Reforms No Election
  • Wananchi wamekosa matumaini maisha ni magumu
  • CCM kuwa madarakani miaka 60 ni fursa lakini ni changamoto kubwa kwa CCM
  • CCM inabebwa na structures, miundo mifumo onayoikibeba
  • Vijana ambao ndiyo wengi wanaona kuwa matatizo yote ya kukosa ajira, masoko na maisha magumu ni sababu ya CCM
  • Ikiwa vijana wengi watajitokeza kupiga kura 2025, itakuwa balaa kubwa kwa CCM
  • Mkutano Mkuu wa CCM kuvunja katiba yake kuteua mgombea uchaguzi na mgombea mwenza ni ulevi wa madaraka
  • Kuna vipindi katiba inakanyagwa, wakati wa Mkapa tunajua majina 5 yaiingia Halmashauri Kuu kuchaguliwa
  • Jakaya Kikwete asingepita ikabidi Mkapa acheze mchezo na alisaidiwa na 'vyombo' majina matatu yakapitishwa Salim Ahmed Sal8m , Jakaya Kikwetw , Prof. Mwandosya
  • Samia Hassan asingepita kuwa mgombea wa CCM January, ilibidi 'vyombo' wafanye namna kuvunja katiba
  • Kuvunjwa katiba ina athari mtambuka inagusa Kidiplomasia, kiulinzi na Kisiasa
  • Ndiyo maana No Reforms No Election imepata nguvu
  • Tundu Lissu anaongea lugha onayoeleweka na vijana, na anatakiwa kupanua wigo akusanye makundi yote
  • Tundu Lissu na viongozi wenzake CHADEMA waongeze hamasa vijana wajitoke kukiunga mkono CHADEMA na wajitokeze kupiga kura
  • CHADEMA wazungumzie matatizo ya Wakulima, Wavuvi, wafugaji wanafunzi wa vyuo ili kugusa mahitaji ya kila kundi
  • Tunaangalia stratejia za CCM na Wapinzani
  • Marafiki zangu Lowassa, Bernard Membe, mwalimu wangu Kingunga Ngombale Mwiru walijitoa CCM walinipigia simu kabla ya kuhama na kuekezea sababu zao ..
  • Tumeandika katika sekretarieti ..

Prof. Eginald P.A.N. Mihanjo. PhD, MA in History, BA (Hon.) Educ. (UDSM) amewahi kuwa Kaimu Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu, Mhadhiri mwandamizi ndani na nje ya nchi, Mkurugenzi wa mafunzo wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC kinachotoa mafunzo ya usalama -stratejia- ulinzi, mhadhiri Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Msumbiji Foreign Relation Kurasini.. pia ni mtaalamu wa Usalama, Ulinzi, Usuluhishi wa Migogoro kimataifa na kikanda ..

No reforms no election ndio habari ya maana na muhimu kwa usalama wa Taifa hili linaloongozwa na CCM iliyojaa wahuni,Malaya,wezi ,vibaka,mafisadi ,wahaini,wahujumu uchumi,wauaji ,watekaji na kila aina ya ubaya na uovu.Maadili yote ya CCM yalizikwa na Azimio la Zanzibar.CCM kimebaki copy na mle mmejaa vibaka na wezi watupu.kwenye hii no reforms no election CCM lazima kuisoma namba.
 
LHRC Watoa ufafanuzi kesi ya uhaini ya Tundu Lissu

View: https://m.youtube.com/watch?v=gCn8A6o0B-Y&t=206s

Mshtakiwa Tundu Lissu angeweza kuomba msaada wa kisheria kutoa kwa mawakili wa nje, ni haki yake kikatiba.

Pia suala la waangalizi nalo ni jambo la kawaida kama tulivyoona majaji wastaafu kutoka Kenya kufika Kisutu...

kuwepo wanaharakati Kisutu ambao ni mawakili kufuatilia mwenendo wa kesi ni suala zuri linaipa mahakama na mfumo wetu wa haki jinai hadhi ...
 
Prof. Mihanjo : CHADEMA kimekaa muda mrefu kama chama cha siasa, sasa kimekuja kivingine kama MOVEMENT / VUGUVUGU 2025
24 May 2025

Vukuto la Vuguvugu la Wanaharakati wa Afrika Mashariki [Sehemu ya 2]​


View: https://m.youtube.com/watch?v=xbzOcablrj8
Wanaharakati Bi. Agather Atuhaire, Bw. Boniface Mwangi, walizuiliwa nchini Tanzania na kisha kutupwa mipakani huku Atuhaire, Mwangi wanaonyesha dalili za kuumia, wakidai kuteswa rumande na vyombo vya usalama vya Tanzania.

Marekani yatoa wito wa Tanzania kuwajibika kutokana na ukiukaji wa haki za binadamu.

Rais Samia Suluhu Hassan atetea kutimuliwa, baada ya kuwekwa kizuizini kwa Wanaharakati wa Kiafrika ..
 
Rais aliyepo atapitia wakati mgumu March 2025 - June 2025

Uchambuzi wa Prof. Mihanjo na usemi wa luteni kanali Jakaya Kikwete kuwa labda kutokee jambo kubwa ndiyo kutaleta ugumu rais aliyepo madarakani kwa sasa kugombea Oktoba 2025 unaanza kuonesha dalili :

Askofu Gwajima aleta mtafaruku mkubwa ndani ya Chama Dola Kongwe na kuliyumbisha Bunge la Chama kimoja la Dodoma


View: https://m.youtube.com/watch?v=3cbwj4dRjKI

1748356312850.jpeg


1748356428061.jpeg
 
31 May 2025
Dodoma, Tanzania
  • 2015 CCM ilikuwa ipotee
  • Kanda ya Ziwa ilibeba CCM chini ya JPM
  • Rais wa sasa aliyeingia kwa ajali, awe makini sana
  • Rais aliyepo atapitia wakati mgumu March 2025 - June 2025
  • No Reforms No Election ni Hoja kubwa sana
31 May 2025
Dodoma, Tanzania

RAIS SAMIA ATOA MANENO MAZITO YALIYOJAA HISIA - "NAISALIMISHA NAFSI YANGU - KUN FAYA KUN"...


View: https://m.youtube.com/watch?v=4vKIw6WU2K0

Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kweli nasema mheshimiwa 'kun Faya Kun' hii maana yake mheshimiwa Spika naisabili nafsi yangu kwa Mungu, yanayotakiwa kuwa yatakuwa, ...
 

23 March 2025​

"Uwekezaji na ulinzi wa rasilimali za taifa ni tatizo" Dr Kasoga achukizwa na kusifia kila kitu​


View: https://m.youtube.com/watch?v=Gz0hJiemUbM
Dr. Lenny Kasoga mhadhiri wa uchumi . Pamoja naye utamsikia Mkurugenzi wa taasisi inayo jishugulisha na uangalizi wa shuguli za Bunge na mbobezi katika maswala ya uchumi.

Dr. Lenny Kasoga a retired lecturer and former Principal, College of Economics and Management Sciences · University of Bagamoyo, Tanzania
 
31 May 2025
Uchambuzi wa yaliyojiri katika Mkutano Mkuu wa CCM DODOMA 29 -30 Mei 2025

Dr Kasoga - Demokrasia mashakani, mkutano mkuu wa May 29 - May 30, 2025 Kila Kitu Kuitikiwa


View: https://m.youtube.com/watch?v=sY_FYWwUfvo
Madhaifu makubwa yajitokeza katika chama hiki dola kikongwe tawala asema Dr. Lenny Kasoga

  • Imebaki kushangilia tu
  • Hakuna kukosoana
  • Mijadala hakuna
  • Mgawanyo wa keki ya taifa haujadiliwi
  • Nchi imefunguliwa, lakini manufaa ya nchi kufunguliwa
  • Ngazi ya chini tawi, kata kuna ubabe ubabe mwingi
  • Watu wamejijengea ka himaya fulani, tofauti na misinhi iliyotumika wakati wa kudai uhuru
  • Viongozi hawatakiwi kufikiria kwa niaba ya watu wote, hakuna ushirikishwaji
  • Mapungufu au ulemavu wa kufifia demokrasia ndani ya chama hiki kikubwa kongwe, sasa unakomaa ndani ya CCM
  • Maonesho ya ki digitali bila kutoa nafasi ya kuuliza, kiasi mkutano mkuu umegeuka ni sherehe au tamasha maana hakuna maswali
  • Mgawanyiko upo ndani ya CCM ndiyo maana nafasi ya maswali ndani ya mikutano inazuiwa
  • N.k
 
Rais aliyepo atapitia wakati mgumu March 2025 - June 2025

Tanzania sasa imechafuka kupitiliza ya Boniface Mwangi wa Kenya , Agather wa Uganda, raia 83 wa kiTanzania ambao Bishop Josephat Gwajima anao ushahidi, ushahidi waliokusanya CHADEMA n.k
 
LHRC Watoa ufafanuzi kesi ya uhaini ya Tundu Lissu

View: https://m.youtube.com/watch?v=gCn8A6o0B-Y&t=206s

Mshtakiwa Tundu Lissu angeweza kuomba msaada wa kisheria kutoa kwa mawakili wa nje, ni haki yake kikatiba.

Pia suala la waangalizi nalo ni jambo la kawaida kama tulivyoona majaji wastaafu kutoka Kenya kufika Kisutu...

kuwepo wanaharakati Kisutu ambao ni mawakili kufuatilia mwenendo wa kesi ni suala zuri linaipa mahakama na mfumo wetu wa haki jinai hadhi ...


Asante kwa taarifa
 
05 June 2025
SASA NI MAPAMBANO YA WAZAZI DHIDI YA VIJANA WAO
Prof. Peter Kagwanja , Dr. Muluka watawala wa Afrika ya Mashariki wajue wao ni 5% ya idadi ya watu katika nchi zao


View: https://m.youtube.com/watch?v=rgbVafKxpzY
yaani wenye umri miaka 50 na kuendelea walio watawala wafahamu kundi kubwa la vijana wamechoka na tawala za kizazi cha baba na mama zao walio madarakani kwa sasa asema Peter Kagwanja

Sasa ni mapambano baina ya wazazi na watoto wao ikiwemo wajukuu. Tofauti na wakati wa uhuru ambapo adui yao alikuwa mkoloni kutoka uingereza katika nchi hizi zilizokuwa koloni za Kenya, Tanzania na Uganda.

Vuguvugu hili la 2025 ni baina ya vijana na wazazi wao hivyo vuguvugu hili halina mkoloni, udini au ukabila bali wazazi dhidi ya vijana wao waliochoka utawala mbaya ulioshindwa kutengeneza mazingira bora ya kupigana na umasikini, ujinga na afya asisitiza Prof. Peter Kagwanja

Dr. Muluka anaongeza watawala wasisubiri mapinduzi, ni bora wakatayarisha mazingira ya uhuru, haki na demokrasia ili vijana wakishinda uchaguzi waweze kuingia au wakishindwa wakubali kushindwa kwao ni halali hivyo hawataleta mapinduzi

Peter Kagwanja anasema mapinduzi yanagharama kubwa kwani kuna kungolewa kwa nguvu, halafu inafuata safisha safisha ya kuondoa waliokuwa watawala na kufuatia wanamapinduzi kulinda ...
 
Peter Kagwanja anasema mapinduzi yanagharama kubwa kwani kuna kungolewa kwa nguvu, halafu inafuata safisha safisha ya kuondoa waliokuwa watawala na kufuatia wanamapinduzi kulinda ...

Anafafanua profesa Peter Kagwanja kwa kina ubaya wa watawala kuchagua kungangania madaraka kwa ulaghai wote kiasi kuweka mazingira ya mapinduzi kuweza kutokea badala ya watawala kujenga demokrasia ...


View: https://m.youtube.com/watch?v=ObDsF_sJKWE
 
Back
Top Bottom