Prof. Janabi: Nakula mara mbili kwa siku

Prof. Janabi: Nakula mara mbili kwa siku

Watu wanapenda,kusikia Yale wanayo yapenda,lakini Dr kwa uzoefu wake katika kada hii anashauri watu kufanya reforms katika maswala ya lishe. Maana mpaka Dr J ameamua kuja na kusisitizia juu ya maswala haya ya lishe ameona kuna mambo yanaweza kuzuilika mapema kama tutaamua kufanya reformation katika maswala ya lishe. Leo tarehe 21 /2/2024 saa tatu usiku utakuwa live TBC watu hawana budi kutenga mda na kumsikiliza.
 
Kabisa kabisaaa.
Kama anakula hivyo, ya nini ku publicise? Yeye ale tu na sisi atuache tule tuwezavyo maadam afya zinaturuhusuu
Yaani hawa watu wanatuvuruga
Kama mwili wangu unataka kwanini niupangie?
Nakula mpaka chocolate so what
Kipendacho roho dawa asitupangie
Hawa ndio wanawakataza watoto pipi badala yake sijui wale shubiri 😄
 

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema katika maisha yake na kile anachoishauri jamii anamaanisha na kukiishi.

Amesema kwa siku anapata mlo mara mbili, na kila mlo unapishana kwa saa kadhaa, akijieupusha kula mara kwa mara.

Prof. Janabi ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam, kwenye mahojiano maalum na vyombo vya habari.
Duh, huyu atastaafu lini ?
 
Me kwanza Naogopaga kumtizama maana anatisha. Ukiambiwa ni Professor, Then Mkurugenzi Mkuu. Utachoka.
 
Huyu mzee kuna vitu anatupotosha sana binafsi simtilii maanani tangu alipotoa kauli sukari si muhimu
Sukari pekee yenye manufaa mwilini ni ile inayopatikana kwenye vyakula vya asili kama matunda, miwa, nk..

Sukari ya kununua dukani ni kama sigara tu, haina faida hata moja, ina madhara tu..

ARE THERE ANY BENEFITS TO EATING SUGAR?
Added sugars don't add any positive benefits to your diet, while naturally occurring sugars are often found in foods that give you the health benefits of fiber, water, and nutrients.
30 Mar 2017.

WHAT ARE THE DANGERS OF DRINKING SUGAR?
Frequently drinking sugar-sweetened beverages is associated with weight gain, obesity, type 2 diabetes, heart disease, kidney diseases, liver disease, tooth decay and cavities, and gout, a type of arthritis..
 

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema katika maisha yake na kile anachoishauri jamii anamaanisha na kukiishi.

Amesema kwa siku anapata mlo mara mbili, na kila mlo unapishana kwa saa kadhaa, akijieupusha kula mara kwa mara.

Prof. Janabi ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam, kwenye mahojiano maalum na vyombo vya habari.
Anafanya kazi gani sasa ya kuhitaji kula mara tatu? Suala sio kula mara ngapi, swala ni kula kile unachohitaji tu, sio zaidi.., sasa njaa inauma hadi unataka kuzimia badi tu ujikaze, what for? why?
 
Ulaji mbaya pia unajaza choo, unakuta mtu anashusha kilo mbili chooni kisa tu alikula chakula kingi, choo kitaachaje kujaa haraka? Nidhamu ya kula haipo, kwenye sherehe pale bufee mtu anachukua kila chakula na kujaza sahani na atarudia tena. Aibu hana anafika mpaka mwisho wa bufee zenye msururu mrefu wa vyakula vingi. Ulaji wa aibu sana unaibisha mabosi wa kazini kwako wataona una njaa kali na huwa huli vyakula hivyo unafakamia tu
Mkuu umeongea kwa uchungu sana
 
Nasikia wagonjwa wa Figo wameongezeka, hasa Vijana sasa hivi ni kutokana na utumiaji wa Pombe na ulaji mwingi wa Wanga !! Tumieni maji…. Kusafisha Figo kwa Wiki mara tatu, Bill ni @300,000+
 

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema katika maisha yake na kile anachoishauri jamii anamaanisha na kukiishi.

Amesema kwa siku anapata mlo mara mbili, na kila mlo unapishana kwa saa kadhaa, akijieupusha kula mara kwa mara.

Prof. Janabi ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam, kwenye mahojiano maalum na vyombo vya habari.
Mara mbili, hiyo ni milo ipi maana tunatakiwa kula milo mitano kwa siku, yaani chai asubuhi, chai saa nne asubuhi, chakula cha mchana, chai saa kumi alasiri na chakula cha usiku ili utumbo uwe kwenye umbile lake.
 
Kuna jamii ya wakulima wao kulakula sana ni fahari sana. Wanakula vyakula vingi kwa wakati mmoja. Inasemekana hubugiza watoto wao wachanga madawa ya kienyeji ili kupanua matumbo yao wale chakula kingi kusudi miili yao iwe mikubwa. Ugali wenyewe tu unapikwa mkubwa halafu ni mgumu tena wa mtama. Hiyo jamii inasifika kwa kula sana eti wawe wakubwa, giant. Ukiwapa chipsi ni kama unawatania watailamba na hawatashiba. Utaratibu wao kupika na kula ni wa ajabu sana. Hawa suala la nidhamu ya kula hawalijui. Wake zao kutwa nzima ni kupika tu, mara viazi, mara ugali, mara makande, mara nyama, mwendo ni kulakula tu njaa hawaijui
 
Asubuhi anakula tango moja na mayai mawili ya kuchemsha .na maji glass 4.jioni saa 11 anakula kipande cha boga na sangara aliechemshwa na limao na kitunguu .anashushia na juisi ya anapiga na glas4 za maji
Nitakufa,kwa hii ratiba...kila,mtu afanye analoweza
 
Ushauri sio kwamba hautasikika kwa Watanzania bali hautatumika.

Angejikita zaidi kuitisha seminar za Viongozi wetu.

Kuwaelimisha kuhusu Lishe itakayowasadia kuongeza Uwezo wa kufikiri. Ingesaidia sana kwenye Uongozi wao ivo Kuboresha maisha ya watu.

Hali duni ya Wananchi inawapelekea Kutokuwa na uhakika wa kuwapata milo.

Sasa hawa unaanzaje kuwapa Ushauri wa kukitumia ambacho Hawana Uhakika wa kukipata?
 
Back
Top Bottom