Prof Jay: Ferooz akiwa wa moto sana alikuwa hagusiki yaani uvimbaji kama wote

Prof Jay: Ferooz akiwa wa moto sana alikuwa hagusiki yaani uvimbaji kama wote

Wakiwa njiani baada ya kukubaliana na Prof Jay kuwa kuna show wanaenda kupiga mkoa flani, Ferooz ghafla akamwambia Prof Jay kuwa naona miyeyusho hii safari kama vipi nageuza [emoji23][emoji23] Akiwa na wapambe wake wakageuza zake nakurudi mjini nakumuacha Prof. Kwenye mataa kitu ambacho

kilimuumiza prof Jay, mko mnaenda Morogoro na mwana mnafika Kibaha mshikaji anakwambia narudi Zangu Dar bila sababu ya msingi inaumiza kiasi gani? Ferooz alikuwa wamoto sana nyakati zake nakumbuka wakati ‘Starehe’ inatoka tulikuwa tunashindana nani kaiona mara nyingi video kwenye

TV sababu ilikuwa ni nyimbo ya Taifa(hadi leo) haijawai tokea wimbo wa magonjwa ukaopendwa sana na watu kubang nao huku ukisindikizwa na Verse kali kutoka kwa Prof. Jay ikikamilisha ngoma kuwa tamu zadi kuliko mvinyo ulikokaa takribani miaka 30 kutoka kiwanda cha Dodoma wine

Wasanii wengi wazamani walipiga sana hela sema kilichowasumbua ni ulimbukeni na starehe za mjini, mtu aliamini Akila milioni 4 leo kesho simu ya promota itaita tena aende kupiga vimeo, kwa mujibu wa Soggy Dog anadai kuwa Mr.Nice alikuwa

anatembea na pesa kwenye buti yani anakula bia bar ghafla anasema “bia za hapa mbaya twenzetu tukale bia Arusha” Soggy akiomba aende home akachukue Nguo Mr. Nice anacheka anamwambia hela zipo kwenye buti tutanunua Arusha.[emoji23]

Producer mkongwe Master Jay anadai kwa macho yake alikuwa ana shuhudia mwindi ‘Mamu’ akiwakabidhi milioni 100 wagosi wakaya kama ‘first inastallment’ ya mauzo ya album na kuna wakati walinunua Gari lake cash hapohapo baada ya kumshawishi kuwa anauza bei gani gari lake [emoji23][emoji23]

Msanii mmoja kutoka kundi la Wagosi wakaya ‘Dokta John’ aliwai kusema kwenye moja ya interview kuwa ni kweli walichezea pesa na anajutia hilo.

Ile kauli kuwa wasanii wazamani hawakupiga Pesa inaweza kuwa ni kweli ukilinganisha na leo ila sio kwamba pesa hawakupata kabisa.

Nature miaka ya nyuma alikuwa anatembelea benzi na inasemekana alikuwa akilimiliki Tax kadhaa mitaa ya Temeke, Matonya alijenga hotel Tanga, miaka 2004 kuna msanii wakike alikuwa anamiliki Zaidi ya

milioni 500 bank. Miaka ya hivi karibuni wasanii wamekuwa hawategemei tena album kama mwanzo bali show na mauzo ya mtandaoni kama miito ya simu,Youtube na mitandao ya streaming bila kusahau deal za makampuni mbalimbali.

Muziki wazamani ulishikiliwa na watu wachache Ila sasa muziki unashikiliwa na recording label kubwa, msanii as individual akitusua bila management kwanza ni ngumu pili kuna maslai yake mengi atakuwa anayakosa.

Label na management kubwa ndio future ya muziki wa bongo.

-Mwisho
#SanukaNaChapo
Credit: Ngomeni & The Bartender.

View attachment 2270725
Kuna siku nimekutana na freooz na picnic arusha anachekacheka tu 😀😀malaya wanamkimbilia na wahuni wanampa offer za bia
 
Labda Billion ya Zimbabwe sio ya Tanzania tena kwa miaka ile, tupeni break sie,
Niliamini maana nimeshamsikia master Jay na p funk wanatoa ushuhuda wa pesa walizoona wasanii wakilipwa, na wasanii wenze pia mfano Soggy wamesimulia Maisha ya Nice
 
Back
Top Bottom