Kwa nini Kabudi anapenda kumdanganya Rais kila apatapo nafasi? Hivi kesi ya Mkulima tulishinda wakati deni lilikuwa palepale?
Kule ni taratibu zilikosewa na watu hata humu JF walionya sana kuwa tunafunika moto kwa kuufunika kwa jivu. Wanasiasa nao walionya wakaitwa mabeberu Jr, wakanyamaza. Serikali ikaanza matambo kama ya kijiweni eti ilipeleka PhD ngapi sijui, wakapongezana hadi Bungeni na magazeti yao yote.
Tunasema tena, tumejikita kupeleka mambo yetu kishamba sana na sifa za kijinga lakini yakiharibika tunataka RAIA wote eti wasikitike na hilo batch la watu wa hovyo. Hapana, ujinga huo ni wenu wenyewe na sasa sijui kama mkulima hata lipwa tena.