GE2025 Prof. Kabudi: Samia ametimiza aliyoshindwa Mwalimu Nyerere

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Yaani kumzidi Nyerere haiwezekani.
Au ndo mlioaminishwa Nyerere ni mtakatifu sana!?
 
Kwa hiyo hakuwa na kitu tofauti Cha kuongea....!?
Coz hata ningekua Mimi katika nafasi yake nisingeweza kumringanisha Nyerere na Kiongozi yoyote yule ama aliyekufa ama aliye hai ama atayekuja huko mbele.....!

Hawa Viongozi wa Sasa wangekua kwenye Nafasi ya Nyerere, wengi wao wasinge survive.....!

Kweli Kabudi alishindwa tu hata kusema yake anayoona mazuri Toka Kwa Samia bila kumringanisha na Nyerere...!?
 
Kujipendekeza kwa kiwango cha namna hii Ili upate cheo kunadidimiza ndoto za wasomi kuwa maprofesa.
 
Kabudi hasomeki aisee! Jalalani kubaya. Alimwita Magu mheshimiwa mungu. Kama Magu alikuwa mungu wake, ni rahisi tu kumfanya huyo kuwa mungu wake na kuanza kumsifu kwa nyimbo na mapambio.
 
Huyu huyu Mwl aliyetupereka shule bure akiwemo Kabudi !!. Aliyehakikisha watoto wa masikini wanasafirishwa bure (warranty) akiwemo Kabudi !!. Huyu Mwl aliyehakikisha hospitalini tunatibiwa bure.

Nyerere alishindwa mambo kwa sababu za uchumi mdogo wa nchi. Tofauti na sasa migodi na viwanda ni vingi, biashara nazo zimekuwa.

Huwezi Kulinganisha kichuguu na mlima Kilimanjaro
 
Prof. Kabudi ni mtu mwenye akili za juu sana kama unataka kujua undani wa rais aliye madarakani basi mtazame Kabudi, kama unamuona kama chizi hivi au ni mtu anaejipendekeza sana basi jiulize wakati wa Mkapa na Kikwete Kabudi hakuwepo??
 
UDSM wamfutie Uprofesa haraka. Wakichelewa chuo kinaweza shushwa hadhi yake.
 
Ndiyo maana mimi sikereki na wabunge ambao hawakusoma. Angalia sasa huyu “msomi” asivyokuwa na kitu cha kumtofautisha na wale ambao hawakusoma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…