Prof. Kitila: Tanzania haitayumbishwa kwa sababu ya mabeberu kutunyima misaada, labda watafute vikwazo vingine

Nyuma gani
 
Tzn haijawekewa vikwazo vya kiuchumi,visa restrictions zimewekewa Nchi zote za Afrika.
 
Mkuu,
Hana jibu katika hili, miradi mingi ipo hoi, wakandarasi hawalipwi...hasa wazawa ambao mitaji yao sio mikubwa wanaumia sana, mabarabara mengi ni mahandaki, njia za dar nyingi zimefumuliwa ila ziko palepale hakuna progress.

Ni kweli hatupendi misaada, ila je tunaweza kujisimamia, mbona miradi mingi imelala?
 
Kwani kabla ya misaada miradi mingi ilikuwa imeamka? Haikulala?

Kutekelezwa Kwa miradi kinategemea upatikanaji wa pesa.
 
Anachoongea yeye ni tofauti na anachoongea aliyemteua.
 
Kujibu hoja za uzushi wa wakandarasi Huwa nawaambia hivi
1.Umewahi kuona wakandarasi wameacha kuomba kazi? Na kama hawaachi unawezaje kuwa site kama haulipwi?

2.Kama hawalipwi site wanafanya nini? Huu sio mradi?

Acheni ujinga na uzushi wa vijiweni huko Kwa machadomo.

View: https://www.instagram.com/p/DbTR4TriNm9/?igsh=MWh4bGxpczNxMnVnMw==
 
Kenya ipo ulaya?

Je imewekewa visa restrictions kama Tanzania?

Vipi kuhusu South Africa?
Nimesema Nchi nyingi san.zimewwkewa visa restrictions na je Kuna ulazima gani wa kwenda huko? Kenya na South ndio nani? Hao wanaouana Kwa sababu ya njaa na unemployment?
 
What a professorial rubbish.
 
Uprofesa wake sijui ni wa nini wakiweka vikwazo hata biashara ya kusafirisha abiria baadhi ya Nchi ATCL haitakwenda,biashara ya madini na utalii itayumba hawa watu vitu vidogo hivi wanashindwa kuelewa na bado wanajiita maprofesa sio kweli..
 
Kwani kabla ya misaada miradi mingi ilikuwa imeamka? Haikulala?

Kutekelezwa Kwa miradi kinategemea upatikanaji wa pesa.
Kwahiyo unaona sawa kusema bajeti ni trilioni 60, fedha za ndani lakini hadi unafunga mwaka wa Serikali unakuta umekusanya trilioni 34 huku fedha yote imekwenda kwenye matumizi ya kawaida badala ya miradi ya maendeleo?

Ni sawa na kwako, unapata mshahara lakini hela yote unamalizia kwenye kulipa Kodi ya nyumba/kula n.k

Hata hela ya kununua kiwanja/kujenga/kuanzisha mradi wa kufuga kuku unakosa 🙌
 
Huyu mtoa mada amechagua kuongea uongo kama Kitila mwenyewe

Suala la Uchumi linatakiwa lionekana Wazi

Sasa unasema bajeti yako ni trilioni 60 fedha za ndani lakini hadi unamaliza mwaka wa fedha husika, umefanikiwa kukusanya asilimia 58 pekee huku fedha yote inakwenda kulipa mishahara pamoja na kujaza mafuta ya atcl kwaajili ya wao kusafiri nje
 
Hawa ndio wale maprofedha wa jalalani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…