Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
Hata wale wajana sio wa CUF utaona watakapo ishia.
 
Na Mie Nahofia Ilo
 
Kikao kilichoketi 28,August kilitangaza kumfukuza uanachama Lipumba.
Ile ilikuwa planned baada ya kuwa amejiuzulu na akaleta fujo kwenye kikao kisichomhusu. Wewe ujiuzulu kwa barua si kwa maneno halafu urudi use m/kiti wa kikao wapi na wapi ?
 
Ujio wa Li-Pumba CUF unafurahiwa na Wana-Lumumba zaidi kuliko wana CUF wenyewe
 
Huu ndio ukweli na watafanikiwa...ni hatari sana
 
Maneno mengi ya nini wakati nimeshaweka proposal mezani?
 
Safi sana Profesa Lipumba fyeka wote hapo, safisha chama chake
 
Kile kikao kilichofanyika Ubungo Plaza mpaka Lipumba na Kundi lake wakaingilia kuvuruga kikao ilikua Zanzibar ile??
 
Sefu kaona urais wa Zanzibar haupati tena...kaamua kukivuruga chama upande wa Bara...

Wana CUF wa Bara msikubali maamuzi wa Chama yakawa yanafanywa na Wazanzibari peke yao. Nyie mnayo haki na chama kinao wanachama pande zote mbili.

Hakuna mtu aliyejitolea kukijenga chama kwa hali na mali kama Profesa. Msimuache peke yake Profesa katika hili...pambaneni na ikishindikana basi gawaneni mbao...CUF Zanzibar iongozwe na Sefu na Mtatiro na CUF Bara iongozwe na Profesa na Magdalena Sekaya..
 
Mkuu kwanza Wabunge wote wa Bara wako na Lipumba. Mtatiro yuko pekee na alitumika kama chambo cha kuaminisha watu wa bara.

Ila huu mchezo una maana sana kisiasa. Vyama vyetu huwa vina amua vitu kama havina vikao vya maamuzi. Ni mwaka CUF walishindwa kutoa maamuzi ya Lipumba kujuuzuru. Sasa ndo wanaona kuna nini ndani.

Huwa tunafanya kazi kwa mazoea sana.
Niliwahi kuuliza humu CUF Lipumba yuko peke yakeau ana wafuasi?

naona kumbe kina Mtatiro hawajui wanachofanya


Halafu Mtatiro nae kahamia Zanzibar?
 
Lipumba anao wafuasi.....asidharauliwe.....ndio maana kina Mtatiro wanakimbilia Zanzibar.

Suluhisho:
Seif na Lipumba wajifungie waongee kiutu uzima wayamalize.....wao ukitazama kwa ndani hawana ugomvi.
 
Wasomi wetu wanatumika vibaya.kwa mtindo huu tutabaki kuwa watu wa zama za mawe.
 
Kile kikao kilichofanyika Ubungo Plaza mpaka Lipumba na Kundi lake wakaingilia kuvuruga kikao ilikua Zanzibar ile??
Tunazungumzia ya sasa na sio ya kale...kwanini vikao vyote sasahivi ni Zanzibar?.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…