Prof. Muhongo asema kuwa hii habari ya 16% Share kwenye Madini huenda tumeliwa!

Kuwa na uwakilishi bado halijawa takwa la kisheria kwa mujibu wa sheria yetu ya madini. Sheria inabidi irekebishwe ili hilo liwe lazima,mwekezaji atake asitake!
 
Kuhusu "kuliwa", hilo lipo wazi; lakini hata hiyo kuwa ndani ya "management" haisaidii chochote!
Haisaidii kivipi wakati ndio unaweza husika kwenye maamuzi. Na sio menejimenti Bali Bodi Ili hata investment decisions, Transfer pricing, Capital flights zote utaziona zinavyo flow so utalinda maslahi ya taifa.
Akina Mnyika si walikuwa ndani ya management' ya Acacia, tukawa tunapigwa hadi Acacia' wenyewe 'guilty conscious' ikawalemea!
I guess ulimaanisha Mwanyika? Huyo alikua muajiriwa wa Barrick wenyewe. Hapa tunaongelea Serikali kuwepo kwenye vikao vya maamuzi. Yes tutaibiwa ila at least tutakua na taarifa kuliko Sasa ambapo hata wakiunderestimate Mapato hakuna anayejua zaidi tunapewa mgao wa 16% kazi imeisha.
 
Yaani wewe unadhani kwamba Kampuni za Madini zinapotupiga serikali zao hazijui au hazibariki hizo ishu kwa mlango wa nyuma?.
Hao lao moja!. Ni jukumu letu kujibeba, kujisimamia!
 
Tulipo sasa kimkataba ni pazuri sana kuliko wakati wa swahiba wake JK.
Punguza utoto, hivi unajua TPDC ilipewa 20% ya hisa kwenye kuchimba gesi ya mnazi bay. Sasa JPM anakuja na 16% mnashangilia? Mbona nchi Ina wajinga wengi. Umeambiwa Tanzanite one tuna zaidi ya hiyo asilimia 16% Sasa kivipi Tena JPM kaboresha. Yale Yale tu zaidi tumerudi chini.
pia JPM alienda mbali zaidi kwa kuweka sharti la kuwa na kampuni ya pamoja ya ubia katika mafini mfano kampuni ya Twiga.
Hata Gesi ilichimbwa kwa ubia, na ndio hapo tuna 20% nani aliyekudanganya subsidiaries au joint venture zimeanza na JPM?. Mbaya zaidi kawapa 84% zote huku hatuna hata board member ndio upuuzi gani huo?
 
Sisi watu wa kupigwa tu, na sasa zinapigwa zinamwagwa Zanzibara tusubiri tu kuendelea kupigwa mpk tukome.
 
Sasa mnyika na zero yake ya form six anajua Nini. Si watamburuza tu
 
Huyu prof ninikilimtoa marambili katika wizara hii itumuamini akisemacho nahisi katika maprof vishoka wamo nahuyu anaweza kuwa ni
 
Huyu Prof. Muhongo alikuwa waziri na hakufanya vizuri, yawezekana hata yeye aliwahikushiriki Kwa namna Moja ama nyingine kwenye mikataba mibovu anayosema. Yaani huyu ni msomi ila sio kiongozi mzuri
 
JPM hakuanzisha mikataba mipya alirekebisha mikataba hiyo hiyo upande wa madini ambayo hao uaowasifia wakina Muhongo na JK ndio waliyoiingia hakukuwa na kampuni ya ubia katika madini kati ya wawekezaji na serikali lakini JPM aliweza kuingiza hicho kipengele. Baada ya marekebisho yaliyofanywa na JPM mapato ya mafini yaliongezeka maradufu na hata sasa yako juu, Hiyo ni empirical evidence JPM aliexcel katika madini na data za mapaao zipo na zimekuwa zikisomwa kila mwaka bungeni. Hiyo 16% ni undiluted share ambayo ni ziada ambayo tunapata licha ya mapato mengine tunayopata na kufanya tunachopata kuwa kikubwa zaidi.

Mokataba ya gesi kuanzia ujenzi wa bomba la gesi hata uchimbaji wenyewe ulifanyoka kimagumashi na baadhi ya sheria za gesi zilipitishwa kwa hafi ya dharura kipindi bunge linaenda kuvunjwa na mikataba ya uchimbaji gesi ikaingiwa haraka haraka wahusika wakachukua chao. Hizo share 20% unazodai TPDC walipewa ni free share? Ni undiuted share?

JPM alitaka sana kurekebisha mikataba ya gesi lakini jinsi ilivyoingiwa alishimdwa na akaona risk ya kushtakiwa na kulipa matrilioni ikabidi aiache jinsi ilivyo.

Frankly speaking katika gesi tumepigwa mno kuliko katika madini japo mikataba illingiwa mostly na utawala wa
Jk.
Kama mikataba ya gesi ingekuwa mizuri umeme ungeuzwa bei ndogo sana na hata products toka katika viwanda vyetiu zingekuwa competetive.

Kazi za JPM zitabakia kuwa classic.
 
Hii vita ni Ngumu mno, Bila sheria na Kanuni ngumu pamoja na Technogy , tutabaki tunapiga kelele kama Mbwa Wa Agip.

Hawa wenzetu sio wajinga , wanaongea lugha moja anzia Watengeneza Mitambo wao (Australia, Canada +South Africa)
Ukijiona mjanja kwa kupewa 16% za umiliki jiandae kupigwa kwenye Operation Cost+ Construction cost. Utaletewa vitu vingi hata usivyovihitaji(Dumping area).

Mie nadhani ni wakati muafaka Sasa Serikali ijitahidi kuunda Kampuni yake itayofanya EPCM katika kila mgodi mpya utakaojengwa hapa huku ikisaidian na Local Content toka Tume ya Madini, ili kuweza kuisaidia serikali kuzuia mianya yote ya Kupigwa.
Mfano mzuri wa hiki nachokiongea ni Mgodi wa SINGIDA GOLD MINE unaomilikiwa na Shanta Mining Company ltd.
Uliojengwa na Watanzania kwa Asilimia 98%.

Timu ile ichukuliwe na serikali ikafanye EPCM zote za Migodi mipya ili kulinda maslahi ya Taifa.

Kinyume na hapo hiyo 16% itabaki kuwa maneno , maana ili kuipata hiyo lazima utoe Mtaji , Gharama za Uendeshaji , kisha salio ndio 16% ije kwetu.
Hata top management ingekuwa na Waswahili tutapigwa tu kwa kuongezewa Gharama za Manunuzi.
 
Hao waaminifu tunawapate? kama Ubunge tu watu wanadanganya itakuwa hao watu chief.
 

Ukiona nchi ni Maskini jua "wavaa miwani myeusi" hawana uwezo!
 
Muhongo anazungumza hayo kwa sababu yeye kwa sasa hayupo kwenye inner circle ya Asali !! Mwalimu alikataa madini yasichimbwe mpaka watanzania wengi wapate elimu ya juu ili wajue nini wanatakiwa wafanye kuhusu madini yao !! Lakini kinyume chake ndicho kinachofanyika eti wanajifanya hawajui nini wafanye pamoja na elimu walizopewa kwa gharama za Nchi !!

Mungu anawaona wote waliohusika katika hujuma za mali ya watu masikini wa Nchi hii !!


Hawatapata peace of mind katika maisha yao yote wao pamoja na vizazi vyao vitakavyokuwa vinatumia mali zilizopatikana kwa kuhujumu mali za Nchi hii !! Mark my words !! πŸ™πŸ™πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…