Serikali inatakiwa kuibeba sekta binafsi kupitia wananchi ili ipambane na makampuni ya nje.Yaani wewe unadhani kwamba Kampuni za Madini zinapotupiga serikali zao hazijui au hazibariki hizo ishu kwa mlango wa nyuma?.
Hao lao moja!. Ni jukumu letu kujibeba, kujisimamia!
Ni ukweli ulio wazi kuwa watumishi wa serikali hawana uwezo wa kifikra kupambana na makampuni ya nje.
Kinachowabeba na matumizi ya nguvu za kisheria tu.
Maandishi na nadharia za serikali kupitia maprofesa hayamaanishi kupata faida zaidi ya sifa za kisiasa.
Utendaji halisi kwa uwepo wa watu wetu kwenye utekelezaji ndiyo utakatupatia faida na siyo makubaliano ya maandishi.