Haisaidii kivipi wakati ndio unaweza husika kwenye maamuzi. Na sio menejimenti Bali Bodi Ili hata investment decisions, Transfer pricing, Capital flights zote utaziona zinavyo flow so utalinda maslahi ya taifa.
I guess ulimaanisha Mwanyika? Huyo alikua muajiriwa wa Barrick wenyewe. Hapa tunaongelea Serikali kuwepo kwenye vikao vya maamuzi. Yes tutaibiwa ila at least tutakua na taarifa kuliko Sasa ambapo hata wakiunderestimate Mapato hakuna anayejua zaidi tunapewa mgao wa 16% kazi imeisha.
Heshima mkuu 'zitto junior'; lakini pamoja na kuelewa umahiri wako katika mswala ya namna hii, sijauona umahiri huo niliozoea kuuona katika mchango wako huu hapa.
Nadhani kulikuwa na kitu, msukumo pembeni uliokufanya uweke tu maneno haya hata bila ya kuongeza uzito wowote kwenye utatuzi wa swala husika.
Huo mstari wa kwanza, ukitaka kufanya hivyo, unatishiwa nyau, kwamba utakosa wawekezaji kwa kutokuwa na mazingira rafiki, na hili unalijua wazi maana yake ni nini!
Uko sahihi, nilikuwa na maana ya 'Mwanyka', asante kwa kunikumbusha kuhusu hilo, na pia ninakubaliana na wewe kwamba alikuwa ni mwajiriwa tu.
Lakini maana yake hasa ilikuwa ni ipi kumwajiri mtu kama huyo? Kuwatia usingizi wanaopigwa waone kwamba wanaye mtu wao huko huko ndani.
Mkuu 'zitto junior', kwenye maswala kama haya, kila mara nina'defer' kwa watu kama wewe, ili muweze kutufungua akili zaidi katika maeneo haya.
Nimejaribu kukumbuka mifano katika nchi za kiafrika ambazo tungeweza kusema kwamba pengine wanazo nafuu zaidi kuliko sisi kwenye maswala kama haya, lakini sioni mfano wa kuuleta hapa; labda Botwana na Namibia?
Lakini kwa hivi karibuni, akili zangu zimeaelekea zaidi Arabuni, Qatar, UAE, Saudi Arabia n.k., ambako kwa ufahamu wangu mdogo naona kama wao waliweza kuwa na utaratibu wa kuhakikisha kwamba mali zao zimetumika kubadili hali zao za maisha.
Sasa hapo ndipo ninajiuliza, wao walifanyaje?
Nimalize kwa kusema kwamba, hata sisi siyo kwamba hatukujaribu, kwa sababu ninajua Mwalimu Nyerere alinuia nasi tufaidike na raslimali hizi, kuna mambo yaliyofanyika iwe hivyo, lakini ilishindikana kwa kupigwa vita na hao hao wanaotupiga.
Ninaomba mkuu, ukitulizana vizuri, ninajua utaleta jambo zito zaidi kwenye mada kama hii kuliko hayo uliyoweka hapo juu.