Prof. Muhongo asema kuwa hii habari ya 16% Share kwenye Madini huenda tumeliwa!

Yaani wewe unadhani kwamba Kampuni za Madini zinapotupiga serikali zao hazijui au hazibariki hizo ishu kwa mlango wa nyuma?.
Hao lao moja!. Ni jukumu letu kujibeba, kujisimamia!
Serikali inatakiwa kuibeba sekta binafsi kupitia wananchi ili ipambane na makampuni ya nje.
Ni ukweli ulio wazi kuwa watumishi wa serikali hawana uwezo wa kifikra kupambana na makampuni ya nje.
Kinachowabeba na matumizi ya nguvu za kisheria tu.
Maandishi na nadharia za serikali kupitia maprofesa hayamaanishi kupata faida zaidi ya sifa za kisiasa.
Utendaji halisi kwa uwepo wa watu wetu kwenye utekelezaji ndiyo utakatupatia faida na siyo makubaliano ya maandishi.
 
STAMIGOLD zamani Tulawaka. Yaweza kuwa mfano wa unachokiwaza.
Sawa kabisa![emoji122][emoji122][emoji106]
Mwenye shida ya Gold, Tanzanite, Diamond....Atakuja Atakuta tumechimba wenyewe viko dukani na bei ya kila madini Tumebandika!; au Tunatangaza mnada wa hadhara!
 
Uwezo wanao !!

Labda UTASHI ndio bado !!
 
Boswana mbona wameweza kufaidika na madini yao ??!!
Tunashindwaje kujifunza kutoka kwao. ??!!

Nakumbuka Profesa kabla hajaingizwa kwenye siasa kwenye awamu ya JK , alipokuja TZ akitokea Umoja wa Mataifa alikokuwa akifanya kazi siku moja nilimsikia redioni akihojiwa alisema kama Nchi imeingia kwenye mikataba ya madini ya kinyonyaji yaani ya kupunjwa tunaweza tukawasiliana na kitengo kimoja huko Umoja wa Mataifa kinachosaidia Nchi zilizotumbukia kwenye mikataba ya kinyonyaji ili zipate haki zao zinazostahili !

🙄 cha kushangaza siku iliyofuatia nilisikia statement tofauti kabisa na ile ya jana kutoka kwake!! Kuanzia pale statements zikawa ni za kisiasa tu !!

Kwahiyo sio kweli kwamba kama Nchi bado hatujui tufanye kipi ili madini yetu yawe na tija katika uchumi wa Nchi !! Bali tumeamua tuwe hivyo sisi wenyewe.


Kupanga ni kuchagua tusidanganyane !! 🙏🙏🙏
 
Profesa niliyemsikia akihojiwa redioni sio huyu tunayemzungumzia hapa kwenye hii thread!
 
Naomba nikujibu kwa kutumia mfano wa jeshi;
Jeshi linaweza kugawanywa makundi mawili makuu;
1. Wapiganishaji
2. Wapiganaji

Likikosekana kundi la pili, hapo hakuna jeshi.
Wapiganishaji hawawezi kujisifu kama hawapo wapiganaji.
Sasa, viongozi wa serikali bila sekta binafsi ni sawa na wapiganishaji wanaojisifu kushinda vita bila wapiganaji (fikra potofu kabisa).
Serikali lazima iwe na mkono wake kwenye utekelezaji kupitia sekta binafsi yenye kuunganishwa na usalama wa taifa (Intelligence Agency).
Changamoto kubwa itakuja kwenye kutofautisha usalama wa taifa na usalama wa viongozi wa serikali wanaopambana na wapinzani wa kisiasa.
 
TISS mko wapi? Mbona nchi inapotea?
Umenikumbusha!; nahìsi waundaji magari wametuhujumu..[emoji56][emoji24][emoji24]
Mzinga Project ndio bado imepona
MADE IN TANZANIA [emoji122][emoji122][emoji122][emoji123][emoji106]
 

Attachments

  • IMG-20230430-WA0009.jpg
    62.4 KB · Views: 1
Tatizo haendi na mambo yake kule anakuta kila kitu
 
Kwani tunapigwa kwa sababu hatujui au tunapigwa kwa sababu wasimamizi wetu wanapata chochote kutokana na kupigwa kwetu ?
 
Umenena !!
 
Shida yake yuko CCM ... Mnafiki tu vile yuko back benches . Alipokuwa front hakuna kitu alifanya..
 
Kwa nini Sheria inayolazimisha Wawekezaji wa Madini kuweka share kwenye soko la hisa la Dar haifanyiki?
 
Kwa bahati mbaya wote hawaielewi dhana ya free carried share wangeeelewa wangekubali kuwa waliweka kifungu hicho toka sheria ya madini ya 2010.
Free carried share (interest)means the interest derived from holding shares of which the holder enjoys all the rights of a shareholder but has no obligation to subscribe or contribute equity capital for the shares
Maana yake ni kuwa kwa migodi yote iliyoanzishwa baada ya kutumika kwa sheria ya madini ya 2010 Tanznia inapata 16% bila kuwekeza hata senti moja. Kwa vyote vile haiwezi kulingana na 50% share equity ambayo Tanzania inapaswa kutafuta pesa za kuwekeza. Kwa hiyo Mh. Heche 2018 na Prof. Muhongo 2023 hawako sahihi
 
Kwa nini Sheria inayolazimisha Wawekezaji wa Madini kuweka share kwenye soko la hisa la Dar haifanyiki?
Kwani
1. wakiweka utanunua
2. Wamweka kwenye masoko mengine kama una nia unaweza kununua popote acha porojo
 
Duh!

Naheshimu sana mawazo kama haya mkuu 'SYLLOGISTI'.
Umetoa ufafanuzi mzuri sana, pamoja na kwamba sina uwezo wa kudadavua taratibu za uhasibu wa huko tunakopigiwa.

Ila mchango ninaoweza kutoa hapa ni kwamba, sisi ilitakiwa tuwe tumejizatiti katika maswala kama haya ya huko wanakotupigia.
Tunao vijana wasomi wazuri tu ambao tungekuwa tunawatumia katika maswala haya haya, ya kudadavua taratibu hizo za EU..., na kuwa wajuvi kabisa. Hapa hakuna 'rocket sciences' yaoyote. Ni ujuha wetu tu wa kujiweka katika hali ya unyonge.

Na hawa washenzi wanapoona ujinga wetu huu, wanafurahi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…