Profesa gani huyu anayelalama kwa ajili ya cheo cha kuteuliwa kwa miaka mitano sasa; inaonekana atalalama hadi kaburini. Ni kama vile alikatishwa mipango yake ya mbeleni kwenye cheo hicho kabla hajaanza kuitekeleza. Labda alikuwa hajaanza kula vya kutosha akanyang'anywa tonge ghafla. Angesoma sheria zote za bunge akawa anazijua. ALitolewa madarakanai kwa kufuata sheria ya Bunge. Mahakama ilisema kuwa sheria hiyo ya Bunge haikuwa halali, lakini ndiyo sheria iliyokuwepo wakati anasimamishwa. Angekuwa na busara ya kutosha angepinga sheria ile kabla haijafanya kazi dhidi yake badala ya kumlaumu mtu aliyeitumia dhidi yake.