Prof Shivji: Nini kifanyike ili kujitoa kwenye mkataba wa DP-World?

Prof Shivji: Nini kifanyike ili kujitoa kwenye mkataba wa DP-World?

Naapa, ningelishangaa sana kama nisingelikuta jina la huyo jamaa munayemfitini miaka na miaka
kikwete ni jizi, fisadi, dalali wa rasilimali zetu, mtu asiefaa kwa lolote!

alianza akiwa waziri wa madini
 
Sijui haws watu watu walikua wanafikiri nini maana wamefanya jambo la kijinga na ovu sana kwa uhai wa nchi halafu jambo baya zaidi hawataki kuachana nalo wanaendelea tu kudanganya wananchi.
Kaka unaijua ndoano au mshale? Waulize wavuvi na wawindaji
 
Baada ya hotuba ndefu nimenukuu haya machache kutoka kwa Prof Shivji juu ya nini kifanyike ili kujitoa kwenye mkataba huu wa kinyonyaji wa DP- World. naandika kama anavyo sema:-

"Kwa ujumla kwa kuhitimisha, mkataba huu sisi wanasheria tunauita honoracy provisions na tukikubaliana hivyo je kuna njia gani ya kujitoa kwenye mkataba huu? Hii sitorudia kusema kwa sababu the destiny ilikuwa ni bunge kuto ridhia mkataba huu lakini kwa sasa na kwa busara zake bunge limeona mkataba huu unafaa na limesha uridhia.

Njia ya pili imependekezwa na chama cha wanasheria na Mzee Warioba, aliposema kwamba tuurekebishe mkataba huu na tufute vipengele vinavyo lalamikiwa. Je njia hii inawezekana? (haiwezekani!) kwa mkataba huu mshirika wako ni lazima akubali ndipo marekebisho yafanyike.

Kama alivyosema Bwana Richard (mzungumzaji aliyetangulia.) kwamba kama mshirika ananufaika na kifungu hiki hatoweza kukubali kurekebisha. Na hata ukisema anakubali je mkataba huo sasa baada ya kurekebishwa utarudi tena bungeni? kwa sababu huo ulio rekebishwa utakuwa haukupitishwa na Bunge!

Jambo jingine nilisikia kwenye clip kutoka kwa Dr. Slaa akisema kwamba kuna muda wa mwaka mmoja kujitoa akinukuu ibara ya tano ya mkataba huu. Nafikiri amekosea tafsiri ya jinsi alivyosoma mkataba huu, ibara ya 5 inasema tu kwamba kama katika muda wa miezi 12 baada ya kusainiwa kwa mkataba na endapo kama hawajakubaliana kupitia project agreement na negotiation, serikali ya Tanzania itakuwa na uwezo wa kutafuta proporsal sehemu nyingine, haisemi kabisa kujiondoa.

Njia ya tatu ya kuingia mahakamani kama wenasheria wengine walivyofanya hapa kuna matatizo. Kama tunavyojua mahakama zetu zinachukua muda mrefu sana kufanya maamuzi, pale kesi itakapo kuja kusikilizwa muda utakuwa umepita na wahusika watakuwa wamesha saini project agreements, mahakama itashindwa kufanya maamuzi ya haki baada ya muda huo kupita na kwakuwa uamuzi wake kwa kipindi hicho hautakuwa na maana yeyote. Ndivyo watakavyo sema.

Njia mojawapo sijui kama wenzangu wamefikiria hiyo, kwenda kufile case na kuomba inaction ili kuzuia serikali kusign any proporsal about agreement mpaka pale kesi ya msingi iwe imeamuliwa, inategemea kiasigani wataweza kuwasilisha hoja zao lakini kisheria inawezekana hiyo. Swali ni je, utakapoingia mahakamani utakuwa unachallenge nini? Huwezi ukachallenge mkataba (IGA) bali utakuwa unachallenge azimio la bunge kwamba ni unconstitutional kwasababu limeridhia mkataba ambao ni unconstitutional. Kwahiyo azimio la bunge liwe ni unconstitutional kwa kuridhia mkataba ambao ni unconstitutional, I hope itakuwa vizuri.

Njia nyingine ambayo inawezekana kabisa, Mheshimiwa waziri mkuu amesema watafanya amendment lakini kama nilivyosema haiwezekani. Bunge laweza kupitisha azimio kurevorke azimio lake la kwanza na bunge lina mamlaka sovereignity power ya ku unvoke it's status. Wabunge wanaweza sema baada ya kusikiliza wananchi wetu tumeona kuwa azimio hilo halikuwa sahihi na tunalifuta inawezekana kabisa na kama azimio likifutwa hakuna rectification na kama hakuna rectification mkataba umefutwa, sasa njia hii pekee inawezekana.

Ni kwa kiasigani wananchi wataweza kuwashinikiza wabunge wao kuwalazimisha wakae tena bungeni warevorke azimio hilo na kufunga huo mjadala inategemea na uwamuzi wao wananchi. Kusema kweli bunge haliko chini ya Dubai hata sheria za kimataifa haziwezi kuli zuia ndio maana ya sovereignity of parliament kwa hivyo uamuzi wa Bunge utaheshimiwa.

Jambo la mwisho kama ninavyopenda kusema kuhusu mchakato mzima wa ubinafsishaji. Kila mara ubinafsishaji unahalalishwa kwa kusema kwamba sisi kama serikali hatukuwa na tija katika uendeshaji wa shirika hili, hiki ni kisingizio na kimetumika kubinafsisha mashirika yaliyokuwa yanaleta faida, nani anataka shirika linalotia hasara? Kuna sekta nyeti katika uchumi huwezi kuweka mikononi mwa watu na bandari ni sekta nyeti mojawapo, huwezi kuiweka mikononi mwa watu kwa sababu mbalimbali.

Mali yetu yote tuna export kupitia bandari, madini yetu yote yanapitia bandarini, mali yote tunayoleta kutoka nje yetu na ya wengine inapitia bandari na mali zenyewe ni sensitive. Sasa huwezi kuweka hiyo bandari mikononi mwa private company bila ya wewe kuwa na control na all say power hujui wataforward nini kupitisha ama watafaidika nini na huwezi kuzuia.

Kama kuna tatizo la ufanisi ni bora kuajiri management kutoka nje, ingawa itakuwa chini yetu kama vile Dubai wanavyoajiri watu kutoka nje kwani lazima ubinafsishe? Na hii sio ukodishaji kama watu wanavyosema ni ubinafsishaji kwa sababu unaweka control mikononi mwa private company bila ushindani kinyume na katiba ya nchi.

Kwa upande wangu mi naona kuna sekta nyeti za uchumi ambazo ni lazima zibaki mikononi mwa serikali na bandari ni moja wapo, fedha ni muhimu na nishati ni yatatu. Unaweza kubinafsisha hoteli au maduka lakini sio bandari wala sekta ya fedha, hata ukiruhusu mabenki binafsi lakini ni lazima uwe na commercial bank ya serikali ni lazima." Amesema Prof Shivji kwenye mjadala huo.

Lakini TPA ndio wamesababisha hili suala, hakuna ufanisi kiasi imetumika kama loophole kubinafsishwa. Na sio TPA angalia ATCL, TRA, TTCL kote huko ufanisi ni zero kabisa sijui taasisi zetu Zina shida gani. Ifike kipindi ajira za utumishi ziwe na KPI mtu asipofikia lengo automatically afukuzwe kazi au awe demoted bila hivyo watu ni business as usual maana wanajua hakuna wa kuwagusa.
Unayoyasema yangewezekana tu kama wanaoteuliwa kuyaongoza hayo mashirika wangekuwa wanachaguliwa kitaalam, kwa kushindanishwa waziwazi mbele ya umma, (public vetting). Hapo wangeweza kupewa key performance indicators ambazo zingetokana na annual plan inayoonyesha nini wanatakiwa ku-achieve. Sasa viongozi wa sekta muhimu kama hizo wanachaguliwa kwa kufuata utashi wa kisiasa na undugu, KPI zitakuwa zimetundikwa wapi?
 
Tumeonekana kituko na Moja ya Taifa la hovyo kabisa kama si wendawazimu!!!

Wabunge Wanapitisha kitu cha hovyo kabisa namna hii hata pasipo-kujadiliwa Kifungu KWA Kifungu!?

Kifungu cha 23 ni mwendawazimu pekee Anaweza kukikubali👇👇👇
 

Attachments

  • Screenshot_20230621-201509.png
    Screenshot_20230621-201509.png
    39.5 KB · Views: 2
  • Screenshot_20230621-201611.png
    Screenshot_20230621-201611.png
    37.2 KB · Views: 1
  • Screenshot_20230621-201742.png
    Screenshot_20230621-201742.png
    37.1 KB · Views: 1
Maneno meeengi mkiambiwa muandamane hamtaki
 
Tujitoe tu kutoka kwenye mkataba huu HARAMU!! Ni bora tuwe na mgogoro kama walivyo Djibouti dhidi ya DP WORLD. Tukapambane Mahakamani
Ujitoe na Nani we boya. Wananchi kupitia Bunge tumeridhia kila sentensi kwenye mkataba. Asanteni Waheshimiwa Wabunge Kwa umoja wenu
 
Tukitoe twende wapi ?!!!

Hivi Dr.Slaa aliihoji TICTS ilipanza kazi zake miaka 22 iliyopita?!!!

Vipi kuhusu Swiss Port pale uwanja wa ndege?!!!

Tatizo wamejaa maneno maneno tu ambayo huwa hayaivishi mboga jikoni.....

#SiempreJMT[emoji120]
 
Wakimaliza kuchukua Bahari na maziwa tuwauzie na Mito na chemi chemi zote wawekeze.

Maana wao ni wataalam wa kuwekeza sana
Ya ndotoni mwako...

Katika huu mkataba na DPW hakun a kumilikishwa ARDHI......

#SiempreJMT[emoji120]
 
Tujitoe tu kutoka kwenye mkataba huu HARAMU!! Ni bora tuwe na mgogoro kama walivyo Djibouti dhidi ya DP WORLD. Tukapambane Mahakamani
Hakuna kurudi nyuma....

Tungeanza kujitoa katika mkataba na ACACIA......

#SiempreJMT[emoji120]
 
Tukitoe twende wapi ?!!!

Hivi Dr.Slaa aliihoji TICTS ilipanza kazi zake miaka 22 iliyopita?!!!

Vipi kuhusu Swiss Port pale uwanja wa ndege?!!!

Tatizo wamejaa maneno maneno tu ambayo huwa hayaivishi mboga jikoni.....

#SiempreJMT[emoji120]
Point. Hakuna kujitoa mpaka mwisho
 
Huyu mama ni muhimu akawa na Baraza la watu wenye akili wakamshauri tuwache kuhonga chawa Ili tuu kujiingiza kwenye matatizo ,kwa sasa sidhani kama tuna Imani na bunge maana hawatujali sisi kama wananchi CCM imefikia pabaya na hii ikifanyika waje na hoja kwenye uchaguzi 2025 ....#uchawanikansainayotutafunapolepole
Yaani unawaita washauri wa Rais kuwa ni chawa ?!!![emoji15][emoji15][emoji1787]

Umevuka mipaka.....

#SiempreJMT[emoji120]
 
Tutakuwa kitovu cha madawa ya kulevya, kwasababu yataingia bila ya sisi kuwa na uwezo wa kuzuia.
Madawa ya kulevya yanaongozwa kuingizwa marekani kila uchao pamoja na kuwa na DEA na vyombo lukuki.....

Unatuletea "illusions" zako hapa ?!!!

Kwani mkataba na TICTS uliyaongeza madawa ya kulevya nchini ?!!!
 
Back
Top Bottom