Chato haina sifa hiyo na hata uwanja wa ndege pale zilitumika fedha za watanzania vibaya.
Mfano siku ya mazishi ya mwenda zake, watu tuli lala Kahama, Katoro Geita na hata wengine Mwanza na Shinyanga kutokana na kinacho pendekezwa kuwa mkoa kukosa huduma muhimu. Leo wana taka mkoa.
 
Mwenye uwelewa na vigezo hapa atusidie ili tujue kwa mujibu wa sheria ya Jamuhuri mkoa unatakiwa uwe na sifa zipi
Ati vigezo 🙂 ....kigezo kimojawapo ni 'wazee wanataka mkoa' basi. Ni kama kiuteuliwa cheo kigezo ni kuwa mtoto wa kada mstaafu/aliyeondoka ili 'riziki' iendelee kuingia kwenye malago yaleyale.

Binafsi sio mpenzi wa kusoma vitabu lakini nalazimika kukitafuta kitabu cha hayati Shaaban Robert ili kujua aliposema nchi ya kufikirika alimaanisha kitu gani. Haiwezekani mbali na utashi wa mkoa lakini kwenye jamii hii kuna mbunge hajui kuwa bunge ndicho chombo huru cha kuisimamia serikali bali anapendekeza kuundwe kingine huku mkuu wake akikana kupitisha sheria aliyoipitisha kwa mbwembwe
 
Kuna haja ya kurekebisha Katiba yetu haraka iwezekanavyo. Yaani kila alikotoka mkuu fulani inalazimishwa uwe mkoa, kwa faida ipi watakayoipata? Basi kila watu na Kanda zao wajipe promo maeneo yao yawe mkoa. Morogoro yenyewe kubwa, Kigoma na Tabora zote bado ni kubwa, bila kusahau Kagera ni kubwa sana, kwa nini usianzishwe mkoa wa Biharamulo bali ni Chato? Kwa nini?
 
We Mama sindo ulitupandishia Kodi za ardhi bila huruma? Au nakufananisha
 
Nyerere Nae angesema Butiama, Makutano Na Ikizu uwe Mkoa??
 
Kanda ipi kungali na Bugando?
Kanda ni hadhi tu technically ni hospitali ya rufaa. Kwa ivyo uwepo wa Bugando kanda hiyo sio kigezo wa kutokuwa na nyingine inategemea hospitali inahudumia watu wangapi.

Ndio maana hapo unaona nimeweka criteria ni population density and being centre of gravity.

Chato aina watu hao na wala sio centre of Gravity; hospitali ya kanda (rufaa) maeneo yale inahitajika Geita mjini kwa sababu kwanza population yake karibu 1 millioni yenyewe tu, bado inaweza hudumia watu kutoka Mwanza, Mara, Chato, Kigoma na maeneo ya Bukoba.

Sehemu zingine zenye sifa ya kuwa centre of gravity either Bukoba, Kigoma au Tabora; kuhudumia hiyo population, lakini siyo Chato.
 
Hiyo Bukoba wakati inapewa hadhi ya makao makuu ya mkoa ilikuwa ni pori tu lakini leo ni mji mkubwa.

Mama Tibaijuka wala asiwe na hofu Chato itajengeka kadri muda unavyokwenda.
Pengine unachapia, hujui historia ya Mji wa Bukoba (1892).
 
Hivi huwa mna nini vichwani mnapotoa statements kama hizi! Wewe ni Samia? Na ikiwa mkoa aibu utaziweka wapi?
Na wewe vipi izo aibu utazuweka wapi hicho kimkoa chenu kisipotangazwa?
 
hapana,mama ana haki ya kutoa maoni yake kwanza kama raia,pili kama mbunge mstaafu ambaye eneo la jimbo lake linahusishwa na na mpango huo na tatu kama mtaalam wa mipango miji ambaye alikua Mkurugenzi Mkazi wa UN Habitat.

Asifumbwe midomo kwani kuwa na wajukuu wa kulea si hoja ya kumfanya asishauri kile alicho nacho kichwani mwake.
 
Naomba niwe mtu was mwisho kusema...
Hakuna na hakutakua na mkoa was chato.
 
"Iwapo nia ni kuunda mkoa unaosogeza huduma jirani na wananchi ni busara mkoa huu kuundwa kwa kuweka makao makuu Biharamulo.

Hara hivyo sioni maana/mantiki ya wakazi wa wilaya za Ngara na Kakonko kuvuka wilaya ya Biharamulo wakienda Chato ambayo ni wilaya itakayokuwa pembeni mwa mkoa huu mpya.

Mkoa huu badala ya kunufaisha wakazi wake wengi, utawaumiza.

Pia sioni manufaa atakayoyapata mkazi wa Buseresere na Katoro kwa kuwa ataongeza umbali wa kwenda makao makuu ya mkoa.

Hata hivyo nashauri serikali badala ya kuwaza kuongeza mikoa, ijikite kupunguza ukubwa wa vijiji na kata.
Hili liende sambamba na kuwarahisishia utendaji wa kazi zao viongozi wa vijiji na kata kwa kuwapa usafiri, vifaa vya kazi kama kompyuta mpakato, simu zinazoweza kupata matukio [picha] vema.

Hapa Ngara kwenye kata ya Muganza, umbali kutoka Kitongoji cha Nyakafandi hadi makao makuu ya Kijiji chao cha Mukubu ni km.15.
Kutoka kitongoji hicho hadi makao makuu ya kata ni zaidi ya km.30.

Mtendaji wa kata na kijiji hawana usafiri wowote.
Huko hakuna umeme.
Wangeweza kusaidiwa kupewa umeme wa jua kwenye ofisi zao ili wachaji simu zao ambazo Kwa sehemu kubwa zinafanya kazi za ofisi.

Wananchi hatuna hitaji la mikoa na wilaya.
Tunahitaji zaidi huduma bora za vijiji na kata.

Ikumbukwe miaka michache iliyopita ukubwa wa vitongoji uliongezwa badala ya kupunguzwa.
Kuna sehemu mitaa/vitongoji vitatu viliungwa kuwa kimoja.
Mzigo uliongezeka."
 
Hiyo Bukoba wakati inapewa hadhi ya makao makuu ya mkoa ilikuwa ni pori tu lakini leo ni mji mkubwa.

Mama Tibaijuka wala asiwe na hofu Chato itajengeka kadri muda unavyokwenda.
Ilikua wakati huo na vigezo vya wakati ule vilitosha kufanya Bukoba kuwa Makao makuu ya mkoa na Ziwa magharibi kuwa mkoa
 
 
Haka kabibi nako mbona kana kiherehere hivyo!? Kama haina sifa si waipe hizo sifa ili wanachato wapate huduma za kimkoa karibu nao atiiiiiih 😜!
 
Nakubaliana na wewe na kama itawapendeza zaidi basii,makao makuu ya mkoa yawe Nyakanazi ambapo patakua centre hata zaidi ya Biharamulo.

Tunajua kama watakubaliana na ukweli huu ni wazi watakua na nia ya dhati ya kuhudumia wananchi.
 
Tatizo lenu akina Tibaijuka na wenzako mkiwa kwenye system mnakuwa vipofu hamuoni, wenye macho (wapinzani) wakisema mnasema wanatumika na mabeberu, mkitoka kwenye system uziwi unawatoka na upofu unawakimbia.

Haya yote wakati Magufuli yupo mulikuwa hamuyaoni na mulikuwa hamuyasemi, wapinzani wakisema wanatekwa na kupigwa risasi na ninyi mnashangilia utafikri aliyepigwa risasi ni mbwa koko, Magufuli kafa ndio mnasema na kujifanya kuwa mnauchungu na wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…