Amefanikiwa kuzipata akili zake
 
Huu mkoa hauna tija.
Kazi na iendelee kwa mambo mengine yenye tija kwa ustawi na mustakabali wa nchi.
 
Yaan nimekuelewa vizuri sana hapa aliposema ( Njia pekee kumuenzi Hayati Magufuli ni kurekebisha mambo ambayo kama binadamu hakufanya vizuri. Mengine yote ni ubinafsi. Na kufifisha sifa zake katika historia ya nchi hii. Tumuache apumzike.

Miundombinu iliyowekwa Chato siyo kigezo kuunda mkoa hapo. Tuikamilishe na kuitafutia matumizi mbadala ya kitaifa. Mfano Airport ya Chato inaweza kufanywa Hub ya kilimo cha contract floriculture na horticulture...(kilimo mkataba cha maua na mboga) ili tuwe na ndege za mizigo kuja kubeba. Na maziwa . )
Unajua Mama ni msomi sana hivyo hata anachoongea lazima tuwaangalie vizuri.

Kweli kabisa chato haiwezi kuwa Mkoa bado sana sana sana.
 
Uzinduzi ulifanyika lini mbona iyo hospital ya wilaya ipo tok kitambo tukio la mwisho ilikuwa ni kuweka jiwe la msingi kwenye hospital ya rufaa ya kanda iliyojegwa CHATO nadhan nipo sahii
Uko sahihi mkuu, kuna hospitali ya wilaya ambayo ni kongwe na kuna nyingine kubwa zaidi ya rufaa kikanda inajengwa hapo Chato.... Haijakamilika.
 
Basi wilaya zote ziwe mikoa zijengeke kadri muda unavyoenda
Hiyo Bukoba wakati inapewa hadhi ya makao makuu ya mkoa ilikuwa ni pori tu lakini leo ni mji mkubwa.

Mama Tibaijuka wala asiwe na hofu Chato itajengeka kadri muda unavyokwenda.
 
apumzike ile muharibu nchi. hatuwezi kufanya ujinga ili kumfurahisha marehemu
 
Wapo viongozi wa aina hii nchi hii, tena wengi sana
Hakuna kiongozi atakubali kupoteza rasilimali fedha za umma eti kujenga makao makuu ya mkoa chato.
 
Serikali isipowekwa wazi vigezo vinavyotumika kuunda mikoa ugawanyaji wa mikoa utaendelea kuwa utata mtupu
Tunaomba orodha ya sifa zinazotakiwa kwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kufuzu kuitwa mkoa. Tukizipata hizo sifa itaturahisishia kujua kama Chato inakidhi vigezo kwa sasa ama la!
 
Hiyo Bukoba wakati inapewa hadhi ya makao makuu ya mkoa ilikuwa ni pori tu lakini leo ni mji mkubwa.

Mama Tibaijuka wala asiwe na hofu Chato itajengeka kadri muda unavyokwenda.
Kwanza Chato irudi Kagera then ule mkoa wa Geita ufanyiwe tathimini upya. Kulazimisha ujinga. Naungana na Prof Tibaijuka kwenye hili.
 
Kama huo ndio utaratibu basi kila wilaya itakuwa mkoa
 
Wazee Wa Chettle Mupo
Mnaona Sasa Hivi Watu Wale Wale Wanawakataa Kweupe
Kuku Wanaona πŸ˜†πŸ˜…πŸ˜„πŸ˜ƒπŸ˜‚πŸ˜πŸ˜€
 
Tufahamishe sifa za eneo kuwa mkoa
 
Vigezo vya eneo kuwa mkoa ni vipi?
 
Kijiografia unaposema kuanzisha mkoa wa chato na chato iwe makao makuu ili kusogeza huduma karibu na wananchi huo ni uongo wa kupingwa kwa nguvu zote,

kama tuko serious Nyakanazi ndio eneo liliopo katikati ya Biharamulo, Ngara, Kakonko na Wilaya ya Bukombe,

kwanini isiundwe wilaya ya nyakanazi kisha tukatengeneza mkoa wa nyakananzi utakaoundwa na wilaya za Biharamulo, Nyakanazi, Ngara, Kakonko na Bukombe?

kwanini tunagangania chato kutoka kakonko na ngara kwenda chato bado ni mbali sana,


kama ajenda iliyopo ni kuwasogezea wananchi huduma za karibu basi uanzishwe mkoa wa nyakanazi ila kama kuna ajenda nyingine ya kijinga basi endeleeni na chato yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…