Prof. Tibaijuka: Chato haina sifa kuwa Mkoa
POSHO ZA WIZARA YA FEDHA MWEZI MARCH,APRIL NA MEI.

Tarehe 31/03/2021 Shilingi 251,000,000/= (kazi maalum)

Siku hiyo hiyo tena tarehe 31/03/2021 Shilingi 198,000,000/=

-Mwezi April ilikuwa balaa.

Tarehe 08/04/2021 Shilingi 44,500,000/=

Tarehe 13/04/2021 Shilingi 155,295,000/=

-Tarehe 30 April nayo ilikuwa balaa

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 43,900,000/= (kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira)

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 14,400,000/=
(siku ya wanawake)

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 43,000,000/=

Mei mosi siku ambayo sio ya kazi.

Tarehe 01/05/2021 Mei Mosi asubuhi Shilingi 184,100,000/=

Tarehe 01/05/2021 Mei Mosi Mchana Shilingi 264,000,000/=

Tarehe 03/05/2021 Shilingi 146,500,000/=
(Kuandika mpango Kazi wa manunuzi watu 125 [emoji3])

Siku hiyo hiyo tena Shilingi 171,200,000/=(kuandaa nyaraka za bunge)

#WeMissYouJPM.
#Tunakukumbuka JPM.
 
Mwendazake alitaka kulifanya Chato kuwa jiji...bila kufuata misingi na taratibu....Mungu akampa sub dakika ya 52.
 
kawaida Hakuna vigezo vikubwa sana vya kuunda mkoa isipokuwa ni serikali kutaka kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuwafikia wananchi au kuwapunguzia gharama pale ambapo huduma hiyo huifuata mbali zaidi ya kilomita 200 kutoka wilayani kwenda mkoani...
Nani aende kujenga kiwanda chato mna akili Nyie kweli ?
 
Wakuu, naomba mnijuze. Hivi Chato inalingana na miji kama ya Bagamoyo, Manyoni, Kilosa , Kongwa au Itigi? Tukumbuke miji hii ilikuwa maarufu tokea ukoloni!!!!!!
 
Mama hajakosea. Huyu Profesa hatoi mawazo kwa kukurupuka hili jambo kalifanya analysis ya kutosha japo anachokoza mjadala kwa kudai kuwa anayejua vigezo avitaje.Hapa sio suala la madiwani kupendekeza.Kumbuka kuwa sio lazima kinachoamuliwa na wengi kiwe sahihi mambo mengine yamekaa kiushabiki.
Mimi huyo Prof aliposhindwa kuongoza Wizara ya Ardhi wakati wa JK nikamuondoa kwenye orodha ya Maprof. Pia alipopokea mgao wa pesa toka kwa Rugemalira sina imani naye tena!
 
sawasawa jiwe,naona umeamua kufufuka
Huyu naye atulie ale mafao naona anawashwa washwa..sisi tumeamua chato iwe mkoa yeye kina muuma nini?kwanza ni moja ya mafisadi papa wa nchi hii..asifanye tukubuke aliyoyafanya.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa uelewa wangu Chato haina vigezo. Tusidanganyane.
Kama kweli JF ni Jukwaa lenye hadhi tunayoitegemea, ningefurahi na kushukuru kupata 'a counter argument', juu ya mawazo haya yaliyowekwa hapa.

Hii ni nafasi nzuri sana ya namna ya kujadili na kubadilishana ,awazo kwenye jambo muhimu sana kama hili.
 
"Katika mazishi Wazee Chato walimuomba Rais Samia mkoa wakidai ni ahadi ya mtangulizi wake.kwa hekima akasema ataangalia vigezo.Kama Mbunge Mstaafu jirani Muleba Kusini najua vigezo havipo.Wazo halitekelezeki. Wazee jirani na sisi naamini tutapewa nafasi kushauri"Anna Tibaijuka....
Ingekua vizuri kama angeandika haya enzi za mwendazake

By the way, hivi zile hela za mbogamboga alirudisha?
 
Mimi huyo Prof aliposhindwa kuongoza Wizara ya Ardhi wakati wa JK nikamuondoa kwenye orodha ya Maprof. Pia alipopokea mgao wa pesa toka kwa Rugemalira sina imani naye tena!
Ni kipi usichokubaliana nacho katika mchango wake, hilo ndilo la maana kuliko kumzungumzia yeye kama yeye.
 
Aliyekuwa mbunge wa Mukeba huko Kagera Prof Anna Tibaijuka amesema Chato haina hadhi ya kuwa mkoa zaidi ya kuwa ni wazo la ubinafsi uliopitiliza.

Tibaijuka amesema kuanzisha mkoa wa Chato ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Kazi Iendelee!
 
Waugawe mkoa wa Geita ili kukifanya kijiji cha Chato kiwe mkoa, daah jaman eeeeh kuna mikoa ni mikubwa Kama Morogoro na Tabora lakin hawaon umuhimu wa kuigawa, wao wanakazania kuigawa Geita
 
Ni kipi usichokubaliana nacho katika mchango wake, hilo ndilo la maana kuliko kumzungumzia yeye kama yeye.
Mkoa hauanzishwi kwa kufuata vigezo alivyovitoa bali ni idadi ya wakazi, eneo na rasilimari. Watu wanawaza mji wa Chato tu badala ya kuunganisha eneo zima yaani kuanzia Kankonko hadi Karagwe ukijumuisha na hiyo Chato na pori la Burigi
 
Mkoa hauanzishwi kwa kufuata vigezo alivyovitoa bali ni idadi ya wakazi, eneo na rasilimari. Watu wanawaza mji wa Chato tu badala ya kuunganisha eneo zima yaani kuanzia Kankonko hadi Karagwe ukijumuisha na hiyo Chato na pori la Burigi
SAWA.

Mawazo kama haya ndio jibu sahihi kwa hoja zake, na siyo kumshambulia yeye kama ulivyofanya hapo mwanzo.

Binafsi, mimi bado nasimama na hoja zake kuhusu sifa za Chato kufanywa kuwa mkoa.
 
"Katika mazishi Wazee Chato walimuomba Rais Samia mkoa wakidai ni ahadi ya mtangulizi wake.kwa hekima akasema ataangalia vigezo.Kama Mbunge Mstaafu jirani Muleba Kusini najua vigezo havipo.Wazo halitekelezeki. Wazee jirani na sisi naamini tutapewa nafasi kushauri"Anna Tibaijuka

---
Anaandika PROF. ANNA K. TIBAIJUKA

Ramani inaonyesha Chato ni sehemu ya Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera. Kiuhalisia. Na kihistoria. Mengine ni kulazimishalazimisha tu.

Naendelea kusisitiza hakuna hoja yoyote ya kiuchumi kuunda mkoa wa Chato. La sivyo basi tuelimishwe.

Ila kama mnapenda siasa za upendeleo wa sehemu fulani ama kwa kuwa mkubwa aliwahi kuzaliwa pale au mtu apewe nafasi kwa sababu ni mtoto wa kiongozi endeleeni kuwabebesha wananchi mizigo ya kulipa kodi kusudi wateule wajichane. Period.

Kwanza ikumbukwe Mkoa wa Geita ulianzishwa kusudi Chato iwe Makao Makuu. Ikakosa vigezo. Geita mjini ikaonekana ndiyo yenye sifa za kuwa Makao Makuu ya Mkoa mpya wa Geita. Hii ilikuwa 2010. Sasa 11 years later Chato ati ina vigezo kuwa Makao Makuu ya Mkoa wake wenyewe? Are we serious with our development? Really? Na Rais wetu mpendwa SSH tunataka kweli kumtwisha zigo la kuamua jambo hili na controversy zake? Elimu haina mwisho. Mimi kama kuna vigezo naomba viorodheshwe. Labda ndiye sina taarifa. Ila so far Hoja ya kuwaletea maendeleo Kakonko, Biharamulo, Ngara na Muleba inayokatwa vipande ninazikataa. Mkoa unaweza kuleta maendeleo gani kwa Wilaya yake wakati Mkoa unategemea bajeti ya Serikali Kuu. Mkoa una mapato gani zaidi ya kutumia kodi? Lets be serious. Maendeleo yanatokana na uwekezaji na uwezeshaji kwa wananchi. Siyo watumishi wa Serikali tena baadhi bila maadili wanaweza kuishia kuwabugudhi wananchi badala ya kuwa msaada.

Njia pekee kumuenzi Hayati Magufuli ni kurekebisha mambo ambayo kama binadamu hakufanya vizuri. Mengine yote ni ubinafsi. Na kufifisha sifa zake katika historia ya nchi hii. Tumuache apumzike.

Miundombinu iliyowekwa Chato siyo kigezo kuunda mkoa hapo. Tuikamilishe na kuitafutia matumizi mbadala ya kitaifa. Mfano Airport ya Chato inaweza kufanywa Hub ya kilimo cha contract floriculture na horticulture...(kilimo mkataba cha maua na mboga) ili tuwe na ndege za mizigo kuja kubeba. Na maziwa .

Hospitali ya Kanda Chato.... naomba tutathmini kwanza maendeleo ya hospitali ya Mloganzila. State of the Art buildings only 40km away from Dar City Centre na Muhimbili. Mojawapo ya mafanikio makubwa ya Awamu ya nne. Lakini Angalia changamoto zake. Uhaba wa madaktari hadi leo. Sasa hao specialist doctors watakaokubali kuishi Chato mtawalipa fedha kiasi gani?. A hospital is not just buildings. Its manpower resources and the economy surrounding it. Katika dhana ya mipango miji na maendeleo ya makazi lazima vigezo vyote hivyo kuangaliwa. Kwa uelewa wangu Chato haina vigezo. Tusidanganyane.
RFA huwa wana kipindi cha busara za mlevi. Tumefikia kiwango cha kuhitaji busara za Tibaijuka kweli? Yaani bado ana akili ya kujua vigezo? taifa gani hili sasa!
 
Mkoa hauanzishwi kwa kufuata vigezo alivyovitoa bali ni idadi ya wakazi, eneo na rasilimari. Watu wanawaza mji wa Chato tu badala ya kuunganisha eneo zima yaani kuanzia Kankonko hadi Karagwe ukijumuisha na hiyo Chato na pori la Burigi
Jamani sisi wa kakonko hatutaki jamani mbona mnatutenganisha na kigoma yetu sisi sio km wale wanyama waliotolewa Serengeti kupelekwa buligi
 
Back
Top Bottom