Prof. Tibaijuka: Uongozi wa Chama na wa Nchi ni tofauti, mission ya Mbowe haijakamilika

Prof. Tibaijuka: Uongozi wa Chama na wa Nchi ni tofauti, mission ya Mbowe haijakamilika

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
PROF TIBAIJUKA: MISSION YA MBOWE HAIJAKAMILIKA!

“Nimemsikiliza huyu Katibu. Sidhani kama anafahamu haja ya kutenganisha Chama Tawala na Chama cha Upinzani. Anaongea kama aliyekariri mambo. Anatumia mfano wa Zitto Kabwe (@zittokabwe) kuachia ngazi.

Mbowe alielezea vizuri jana suala la Mission yake hata kama sisi wanaCCM tunayo yetu ya kumpinga. Sasa je aachie ngazi kwani kaikamilisha? Nyerere angeachia ngazi mapema hili Taifa lingeimarika?

Hivo mimi nadhani tunahitaji elimu zaidi ya uraia kutofautisha uongozi wa Vyama na uongozi wa nchi."

Prof Anna Tibaijuka (@AnnaTibaijuka) ameandika haya kwenye moja ya group la WanaCCM!
 
Wanaongea kutokana na wanayo yaona. Kama wanapigana vijembe wao wafanyaje. Tuwe wapole kwani kwenye mapambano kuna fitina. Hata wandani wanakuwa kama yuda tunao tu. Situnawaona jama.
 
PROF TIBAIJUKA: MISSION YA MBOWE HAIJAKAMILIKA!

“Nimemsikiliza huyu Katibu. Sidhani kama anafahamu haja ya kutenganisha Chama Tawala na Chama cha Upinzani. Anaongea kama aliyekariri mambo. Anatumia mfano wa Zitto Kabwe (@zittokabwe) kuachia ngazi.

Mbowe alielezea vizuri jana suala la Mission yake hata kama sisi wanaCCM tunayo yetu ya kumpinga. Sasa je aachie ngazi kwani kaikamilisha?

Je Nyerere angeachia ngazi mapema hili Taifa lingeimarika? Hivo mimi nadhani tunahitaji elimu zaidi ya uraia kutofautisha uongozi wa Vyama na uongozi wa nchi”

Prof Anna Tibaijuka (@AnnaTibaijuka) ameandika haya kwenye moja ya group la WanaCCM!
🤔🤔🤔
 
Ni makada wa CCM wameamua kufanya vituko tu wakishirikiana na mchungaji Msigwa
Kuna nyakati huwa inakuwa vigumu kujuwa kwa nini wana CCM wengi humfagilia Mbowe zaidi. Nadani kuna jambo mahali.

Ina maana CHADEMA ya Mbowe siyo tishio sana kwa CCM?
Ni lazima patakuwepo na sababu maalum ya kuwepo kwa hali hiyo!
 
Kwa sasa kwa ccm Bora mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa chadema kuliko lissu, huo ni ukweli.Ccm wanajua namna ya kucheza na mbowe wanammudu.
 
Kwenye uongozi wa chama Kuna mission ya mtu binafsi au ya chama?
Chama ni watu na viongozi ni watu wanaotekeleza mission ni watu kama nyie mnavyoimba mapambio ya mama yenu.

Mama kajenga reli,
Mama kajenga shule,
Mama kajenga barabara,
Mama kaipeleka timu Afcon.
 
Kuna nyakati huwa inakuwa vigumu kujuwa kwa nini wana CCM wengi humfagilia Mbowe zaidi. Nadani kuna jambo mahali.

Ina maana CHADEMA ya Mbowe siyo tishio sana kwa CCM?
Ni lazima patakuwepo na sababu maalum ya kuwepo kwa hali hiyo!
Sidhani kama CCM wanamfagilia Mbowe. Ameshapewa kesi za ugaidi, ameshawahi kuharibiwa biashara zake, ameshawahi kufungiwa akaunti zake za benki na ameshapigwa na vibaka hadi akawa anatembelea magongo.
 
Mbowe ahakikishe 2025 chama kinashika Dola,

Atakuwa amemaliza mission Kisha aachie ngazi Kwa amani kabisa.
 
Back
Top Bottom