Prof. Tibaijuka: Uongozi wa Chama na wa Nchi ni tofauti, mission ya Mbowe haijakamilika

Prof. Tibaijuka: Uongozi wa Chama na wa Nchi ni tofauti, mission ya Mbowe haijakamilika

JE SAMIA HASSAN AJIUZULU URAIS 2024? ILI ABAKIE MWENYEKITI KUKIIMARISHA CHAMA ?​

HIstoria

Kwa nini Julius Nyerere alijiuzulu uwaziri mkuu​

Na leo mwaka 2024 chama Dola kongwe kimekosa ushawishi hadi kuvuruga uchaguzi wa TAMISEMI 2024
"Nyerere alijiuzulu uwaziri mkuu wa nchi Januari 1962 ili ajitoe kwa ajili ya kukiimarisha chama."

Alhamisi, Desemba 07, 2023

MAKALA MAALUM DOLA NA CHAMA

By William Shao
Mwandishi
Mwananchi

Dar es Salaam. Mwalimu Julius Nyerere alipoteuliwa kuwa Waziri Kiongozi wa Tanganyika Mei 1, 1961, alidumu katika wadhifa huo kwa siku 241 tu hadi alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, Desemba 9, 1961 Tanganyika ilipopata uhuru.

1733997759346.jpeg

Katika wadhifa wake wa uwaziri mkuu alikaa kwa siku 266 tu tangu alipoteuliwa hadi alipojiuzulu na kurudi kijijini kwake Butiama mkoani Mara.

Alipojiuzulu uwaziri mkuu na Rashidi Kawawa kuchukua nafasi yake, Nyerere alitoa sababu za kujiuzulu huko kuwa ni kwenda kujenga Chama cha Tanganyika Africans National Union (Tanu), lakini hiyo ndiyo ilikuwa sababu?

Hakukuwa na hakuna sababu yoyote ya kutilia shaka kile kilichotajwa na Mwalimu Nyerere kama sababu za kujiuzulu kwake uwaziri mkuu kwa wakati huo. Hata hivyo, kitendo cha Tanu kuimarika zaidi na kurudi kwake madarakani kama Rais wa nchi, kilifanya sababu alizozitaja zionekane halisi kuliko ilivyodhaniwa awali.

Kwa nini Nyerere alijiuzulu uwaziri mkuu?
Sababu kubwa aliyotoa Nyerere ya kujiuzulu kwake uwaziri mkuu ni kwenda kuimarisha chama.
Waandishi wawili, Florence Lemoine na John Strickland, katika ukurasa wa 137 wa kitabu chao, 'Government Leaders, Military Rulers, and Political Activists', wameandika kuwa "Nyerere aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Taifa hilo (Tanganyika), lakini akajiuzulu wiki chache tu baadaye kwa sababu ambazo hazikuwahi kuwekwa wazi."

Kitabu 'The Europa World Year: Kazakhstan—Zimbabwe, Book 2004', chapa ya 2004 katika ukurasa wake wa 4,094 kinasema "Nyerere alijiuzulu uwaziri mkuu wa nchi Januari 1962 ili ajitoe kwa ajili ya kukiimarisha chama."

Mwandishi wa historia, Godfrey Mwakikagile, katika ukurasa wa 28 wa kitabu chake, 'Tanzania Under Mwalimu Nyerere: Reflections on an African Statesman' aliandika Januari 22, 1962 kuwa, Alijiuzulu kama Waziri Mkuu na kumteua Rashidi Kawawa kuwa waziri asiye na wizara maalumu, kama mrithi wake.

Alisema amejiuzulu ili akakijenge chama alichosema kilikuwa kimepoteza mwelekeo.
Kitabu cha 'Yearbook of the Encyclopedia Americana' chapa ya mwaka 1965 kilichoandaliwa na Alexander Hopkins McDannald kinasema, "Nyerere alijiuzulu uwaziri mkuu ili kuongoza Tanu."

Hata hivyo, mwandishi Theodemidrovich Lugomola katika ukurasa wa 15 wa kitabu chake, 'Uhuru Ulioporwa', anasimulia kuwa kulikuwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Tanu siku 40 baada ya Uhuru wa Tanganyika.

Wajumbe walioaminiana walifanya kikao cha siri siku moja kabla ya kikao chenyewe kilichofanyika katika Hotel ya International kuzungumzia tetesi za tuhuma dhidi ya Mwalimu Nyerere za kwamba alikuwa amejengewa nyumba na Amir Jamal eneo la Kinondoni ili ampe uwaziri. Katika kualikana, mmoja wa waalikwa alikuwa Bibi Titi Mohamed.

Mwandishi huyo anadai kuwa habari hiyo ilibaki kuwa siri karibu kwa Watanganyika wote isipokuwa kwa waliokuwa wajumbe wa mkutano huo wa siri wa ndani hadi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Katibu Mkuu wa Tanu.

Inaelezwa kuwa Kambona hakuwa kwenye mkutano huo, lakini alifikishiwa taarifa na Bibi Titi, naye akazifikisha kwa Nyerere.

Baada ya siri ya mkutano wa siri kumfikia Mwalimu Nyerere, alilazimika kujiuzulu kabla ya kutakiwa kufanya hivyo.

Madai kama hayo yaliwahi kutolewa na Oscar Kambona, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Tanu wakati Nyerere akijiuzulu.
Baada ya kurejea nchini kutoka uhamishoni ili ashiriki mageuzi ya kisiasa baada ya kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa, Kambona alizungumza na waandishi wa gazeti la 'Wasaa' kwa kile alichodai kuwa ni kurekebisha historia 'ambayo haikuwa sawa' kuhusu kujiuzulu kwa Mwalimu Nyerere hata baada ya kula kiapo cha kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika.

Kambona aliwaambia waandishi hao kuwa sababu ambazo historia inasema kuhusu kujiuzulu kwa Nyerere si za kweli, bali alijiuzulu kutokana na tuhuma za kupokea rushwa ya nyumba kutoka kwa Amir Jamal.

Habari hiyo ilichapwa katika toleo la pili, namba 20 la Mei 1993 katika ukurasa wa mbele, wa tano na wa 11 chini ya kichwa cha habari kinachosomeka, "Siri ya kujiuzulu kwa Nyerere yafichuka.'

Pia, mwandishi Ronald Aminzade katika ukurasa wa 108 wa kitabu chake, 'Race, Nation, and Citizenship in Post-Colonial Africa: The Case of Tanzania' anaandika "Amir Jamal alimlipia Nyerere nauli ya kwenda Umoja wa Mataifa mwaka 1955.”

Kambona alikaririwa na Wasaa akisema: "Nakumbuka, tena nakumbuka vizuri sana kuwa Nyerere hakujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 1962 kwa sababu ya kwenda kuimarisha chama cha Tanu.

Fikiria Uhuru ulipatikana Desemba 9, 1961, kwenye Januari 22 Nyerere alisimama na kutamka mbele ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Tanu kuwa anajiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu ya kurudi kwenye chama ili kukiimarisha.

"Sababu hiyo haiingii akilini,” alisema Kambona. “Iweje Tanu iliyokuwa na nguvu ya kumwondoa mkoloni, baada ya siku zipatazo 40 imezorota kiasi cha kuhitajika msaada wa kuimarishwa.”

Alihoji: “Yaani Tanu kilichokuwa kina mshikamano wa wananchi wote waliodhamiria kuichukua nchi yao kutoka kwenye utawala dhalimu wa wakoloni imezorota siku 40 tu baada ya kupata uhuru? Hiyo haikuwa sababu ya Nyerere kujiuzulu uwaziri mkuu, ila sababu hiyo ilitumiwa na Nyerere ili kumkinga na aibu iliyotaka kumkuta, pamoja na kuwageresha Watanzania wasifahamu ukweli halisi wa mambo."

Kambona alisema kilichomshangaza ni kwamba Watanzania wengi waliikubali sababu hiyo bila kuitafakari, na vitabu vingi vya historia viliandika juu ya sababu hiyo.

Alidai kuwa yeye alikuwa Katibu Mkuu wa Tanu na Waziri wa Mambo ya Ndani wa wakati huo na kwamba alijua kuwa ukweli wa mambo haukuwa ule.
"Kikao (cha siri) kilikuwa na ushahidi wa kutosha wa kuonyesha kuwa Nyerere alijengewa nyumba na Jamal huko Magomeni, na kujengewa huko kulizaa fikra kuwa Jamal amemjengea nyumba Nyerere ili apewe uwaziri.

Hivyo wajumbe kadhaa wa Halmashauri Kuu ya Tanu waliamua kuzungumzia juu ya tuhuma hizo kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya TANU uliokuwa unafanyika Januari 20, 1962.

Alisema kwa kuwa walikuwa na ushahidi, kuna wajumbe waliomba kuungwa mkono na wenzao ili wamshtaki Nyerere mbele ya Halmashauri Kuu ya Tanu iliyokuwa ikutane Jumapili iliyofuata, Januari 21, 1962.

Kambona alisema katika mazungumzo yake na Nyerere, alimuuliza kuhusu suala la kujengewa nyumba na Jamal, Nyerere alikiri.

"Nilimwambia Nyerere amwite mdogo wake, Joseph (Nyerere), ili tujadiliane jambo hilo. Joseph alipoletwa, tukawa mimi, Nyerere, Bibi Titi na Joseph.

Nikamweleza Nyerere ni vyema yeye akajiuzulu mwenyewe kabla ya kulazimishwa kujiuzulu kwa tuhuma hizo, kwa hiyo mbele yetu Nyerere akakubali kujiuzulu lakini akaniuliza akishajiuzulu nani atapewa uwaziri mkuu na atatoa sababu gani ya kujiuzulu."

Kambona alidai alimwambia Nyerere kuwa wajumbe walimtaka yeye (Kambona) awe waziri mkuu, lakini akapinga hoja zao na kulikuwa na sababu nyingi za kupinga. Baada ya majadiliano ya muda fulani ndipo jina la Kawawa likaletwa.

Baada ya kumpata Waziri Mkuu, Kambona alisema, kihunzi kingine kikawa "sababu ya kujiuzulu."

"Ndipo nilimshauri Nyerere aueleze mkutano kuwa anajiuzulu kwenda kuimarisha chama cha Tanu, sababu hiyo ingekubalika kwa watu wengi.

Kwa hiyo Januari 20, 1962 kwenye ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri ya Tanu, katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano Nyerere alitangaza kujiuzulu kwa ajili ya kukiimarisha chama."

Je, sababu alizotoa Nyerere za kujiuzulu kwake ni za kweli? Ni vigumu kujua. Je, sababu alizotoa Kambona za kujiuzulu kwa Nyerere ni za kweli?

Nation Media Group © 2024
 
Sidhani kama CCM wanamfagilia Mbowe. Ameshapewa kesi za ugaidi, ameshawahi kuharibiwa biashara zake, ameshawahi kufungiwa akaunti zake za benki na ameshapigwa na vibaka hadi akawa anatembelea magongo.
Mr yoda pole sana, ktk mission ya kitaifa, mtu anapigwa mpaka risasi ya mguu, I'li tu kuwaminisha watu ( wajinga sembuse kupigwa virugu. Tafuta jicho la tatu mkuu, litakusaidia
 
PROF TIBAIJUKA: MISSION YA MBOWE HAIJAKAMILIKA!

“Nimemsikiliza huyu Katibu. Sidhani kama anafahamu haja ya kutenganisha Chama Tawala na Chama cha Upinzani. Anaongea kama aliyekariri mambo. Anatumia mfano wa Zitto Kabwe (@zittokabwe) kuachia ngazi.

Mbowe alielezea vizuri jana suala la Mission yake hata kama sisi wanaCCM tunayo yetu ya kumpinga. Sasa je aachie ngazi kwani kaikamilisha? Nyerere angeachia ngazi mapema hili Taifa lingeimarika?

Hivo mimi nadhani tunahitaji elimu zaidi ya uraia kutofautisha uongozi wa Vyama na uongozi wa nchi."

Prof Anna Tibaijuka (@AnnaTibaijuka) ameandika haya kwenye moja ya group la WanaCCM!
Mama ana vimacho vidogo kama senene.

Zile shule za Babra na ile ya Kitendaguro/Kibeta, wakati akiomba msaada wa kuzinenga, alieleza wafadhili kwamba wasichana watasoma bure. Yeye akaanza kuwatoza mamilioni ya shilingi
 
PROF TIBAIJUKA: MISSION YA MBOWE HAIJAKAMILIKA!

“Nimemsikiliza huyu Katibu. Sidhani kama anafahamu haja ya kutenganisha Chama Tawala na Chama cha Upinzani. Anaongea kama aliyekariri mambo. Anatumia mfano wa Zitto Kabwe (@zittokabwe) kuachia ngazi.

Mbowe alielezea vizuri jana suala la Mission yake hata kama sisi wanaCCM tunayo yetu ya kumpinga. Sasa je aachie ngazi kwani kaikamilisha? Nyerere angeachia ngazi mapema hili Taifa lingeimarika?

Hivo mimi nadhani tunahitaji elimu zaidi ya uraia kutofautisha uongozi wa Vyama na uongozi wa nchi."

Prof Anna Tibaijuka (@AnnaTibaijuka) ameandika haya kwenye moja ya group la WanaCCM!
Hapo Tibaijuka ameonesha u-prof wake vizuri, sasa tunaungana na prof kusema; kweli kabisa mission ya Mbowe CDM na kwa TAIFA nzima bado haijakamilika na hivyo Mbowe bado anapaswa kupewa nafasi akamilishe mission hiyo.
 
Chama dola kongwe chini ya mwenyekiti wa CCM Taifa, pia mbali ya kukosa ushawishi kisiasa, kimekosa mwelekeo wa kuongoza sera ya maendeleo. Hivyo ni muhimu mwenyekiti wa CCM taifa ajiuzulu kofia ya urais wa Jamhuri ya Muungano arudi ofisi za chama makao makuu kukijenga upya chama. Kofia mbili za uongozi kimefanya chama dola kongwe kudhoofika.

Naye classmate wa komredi Abdulrahman Kinana, Mzee Zonga Mafie asimulia jinsi chama dola kongwe kilivyokwama katika sera ya viwanda vikubwa

View: https://m.youtube.com/watch?v=QTh6x1Fr5pc

Mzee Zonga Mafie alikuwa akizungumza katika kikao cha Maandalizi ya Maandamano ya Amani leo Jumatatu Februari 5, 2024 kilichochoshirikisha BAVICHA kujiandaa kwa maandamano siku zijazo ..
 
Kujiuzulu kwa Kinana hakuna madhara kwa dola, ingawa mwenyekiti wa CCM Taifa Dr. Samia Hassan sasa atakuwa amelemewa majukumu ya kuwa Mwenyekiti na makamu mwenyekiti CCM bara, amiri jeshi mkuu, rais wa jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibarc(Tanzania) ...mteuzi wa nafasi zote za viongozi wa serikali

13 July 2024

DK 7 za KINANA AJILIPUA MBELE YA RAIS SAMIA , "tunalalamikiwa tuache rushwa"

View: https://m.youtube.com/watch?v=R1uNCHfBZGg

Akiongea mbele ya vigogo wa CCM walio viongozi serikalini akiwemo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Makamu Mwenyekiti wa CCM bara komredi Abdulrahman Kinana kabla ya kuandika barua ya kujiuzulu

Tutapata viongozi wabovu, sasa hivi wanaoomba uongozi wanaombwa rushwa anasikitika Abdulrahman Kinana.

Viongozi tusiendekeze rushwa tunapokwenda uchaguzi wa 2024 / 2025 na imani ya wananchi kwetu sisi CCM itapungua

Pia soma
- Kuelekea 2025 - Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia
 
Kweli kabisa hoja za Prof. Tibaijuka

Kujiuzulu kwa Nyerere, 1962​

Mwaka 1962 Nyerere alijiuzulu nafasi yake ya uwaziri mkuu ili kutumia muda wake wote katika kazi yake kama rais wa TANU. Kitendo hiki kinaonekana kuchochewa na hisia zake kwamba alikuwa amejitenga na cheo na kwamba alipaswa kujihusisha na kazi za kisiasa katika ngazi za chini ili kupata nafasi muhimu kwa TANU na kurejesha uungwaji mkono. ya watu. Zaidi ya hayo, alihisi kwamba serikali ilitambuliwa kupita kiasi naye kibinafsi na kwamba ilikuwa lazima kwa wenzake kujifunza kuendelea bila yeye. Muhimu zaidi, kwa maoni ya Pratt, ilikuwa ni hisia ya Nyerere kwamba alipaswa kuwasilisha kwa watu haja ya kufanya kazi kwa bidii na maoni kwamba kazi hiyo inampasa yeye kwa niaba ya Tanganyika badala ya kujitukuza. Nyerere alipendekeza kutoa muda wote kwa jukumu lililompa heshima ya mwalimu (mwalimu).

Nyerere alitumia muda mwingi wa 1962 akizunguka nchi nzima kusikiliza na kuzungumza na viongozi wa ndani wa TANU na cheo na faili, lakini hakuhusika na ujenzi wa shirika wala, kwa wakati huo, na kuongeza ushiriki wa TANU katika kutunga sera au utawala. Aliendelea kuchukulia serikali na sio chama kuwa ndio chimbuko la sera.
Kazi yake kuu ilikuwa kufundisha, ambayo aliifanya kwa mdomo na kwa maandishi. Katika vijitabu alivyotayarisha wakati huu alidai kuwa jamii ya Kiafrika ilikuwa na utaratibu wa kimaadili ambapo watu walijali wao kwa wao lakini kwamba utaratibu huu ulikuwa unatoa nafasi kwa umiliki wa fujo. Dhana hiyo ya utaratibu wa kimaadili wa kitamaduni wa Kiafrika inasisitiza dhana ya Nyerere ya ujamaa, ambayo, inazidi kuwa sehemu muhimu ya ujumbe wake. Lakini wakati huu alijishughulisha na taasisi za ujamaa bali na maadili yake, na hakujishughulisha na Umaksi au mawazo mengine ya Kizungu kuhusu ujamaa bali kile alichofikiria kuwa mizizi yake ya Ujamaa.
Kwa maoni yake, katika jumuiya za kitamaduni za Kiafrika, wanajamii waliitunza jumuiya hiyo, na jumuiya hiyo iliwajali wanachama wake. Watu binafsi hawakuwa na haja wala hamu ya kunyonya kila mmoja. Mitazamo hii ilibidi aihifadhi na kwa kiwango ambacho walikuwa wamepotea, walipatikana. Mnamo 1962 Nverere aliandika: "Ujamaa wa kweli ni mtazamo wa akili. Kwa hivyo ni juu ya watu wa Tanganyika ... kuhakikisha kuwa mtazamo huu wa ujamaa haupotei kupitia vishawishi vya kujinufaisha kibinafsi (au kutumia vibaya vyeo). wa mamlaka) .

Yaliyounganishwa na dhana hii ya msingi ya tabia ya msingi ya jamii ya kitamaduni ya Kiafrika yalikuwa mapendekezo ya sera ya jumla ya Nyerere: kwa sababu unyonyaji - kuishi kwa kazi ya wengine - haukuwa wa haki na unaharibu maelewano ya kijamii, unyonyaji kama huo lazima ukomeshwe. Kwa kweli katika jamii ya vijijini hiyo ilimaanisha mwisho wa umiliki wa mtu binafsi wa ardhi. Hii ilionekana kuruka mbele ya dhana ya awali kwamba wakulima wanaoendelea walipaswa kutiwa moyo na kwamba mafanikio yao, labda katika soko, yalikuwa kuwa mfano kwa wengine. Zaidi ya hayo, tofauti kubwa za mapato lazima zizuiwe. Msomi wa uchumi wa Asia na Ulaya hakupaswa kurithiwa na Mwafrika.
Jukumu la chama pia lilishughulikiwa, si kwa muundo na utendaji wa kina bali kuhusiana na mafanikio ya jamii yenye uadilifu na maadili. TAW ilikuwa ni kuwataka wanaTanganvika kufanya kazi kwa bidii, hasa ili kuondokana na umaskini, lakini ilikuwa kufanya hivyo kwa kuishi na kujifunza miongoni mwao, si kwa kuwawekea fikra zake. Viongozi zaidi wa TANU walipaswa kuruhusu, hata kuhimiza ukosoaji wa ndani.

Source : GlobalSecurity.org
Mmh! Umeandika but sijaelewa kabisa. Sijui lugha uliotumia ngumu au umakini wangu kuwa mdogo duh!
 
Sidhani kama CCM wanamfagilia Mbowe. Ameshapewa kesi za ugaidi, ameshawahi kuharibiwa biashara zake, ameshawahi kufungiwa akaunti zake za benki na ameshapigwa na vibaka hadi akawa anatembelea magongo.
Haya yote nayafahamu mkuu Yoda, siyo mageni kwangu, kama ilivyo kwa Tundu Lissu kumiminiwa risasi!

Lakini pamoja na yote hayo, ukitazama kwa fikra zilizo wazi jinsi Mbowe na Lissu wanavyo tazamwa huko ndani ya CCM huwezi kukosa kuona tofauti kubwa iliyopo kati ya hao wawili katika macho ya wana CCM (at least wanao jitokeza mbele na kuzungumza).
 
Huyu ni Prof! Mbowe hana Mission, anatekeleza mission ya chama. Mwanchama yeyote anaweza kuitekeleza.
 
Kweli kabisa hoja za Prof. Tibaijuka

Kujiuzulu kwa Nyerere, 1962​

Mwaka 1962 Nyerere alijiuzulu nafasi yake ya uwaziri mkuu ili kutumia muda wake wote katika kazi yake kama rais wa TANU. Kitendo hiki kinaonekana kuchochewa na hisia zake kwamba alikuwa amejitenga na cheo na kwamba alipaswa kujihusisha na kazi za kisiasa katika ngazi za chini ili kupata nafasi muhimu kwa TANU na kurejesha uungwaji mkono. ya watu. Zaidi ya hayo, alihisi kwamba serikali ilitambuliwa kupita kiasi naye kibinafsi na kwamba ilikuwa lazima kwa wenzake kujifunza kuendelea bila yeye. Muhimu zaidi, kwa maoni ya Pratt, ilikuwa ni hisia ya Nyerere kwamba alipaswa kuwasilisha kwa watu haja ya kufanya kazi kwa bidii na maoni kwamba kazi hiyo inampasa yeye kwa niaba ya Tanganyika badala ya kujitukuza. Nyerere alipendekeza kutoa muda wote kwa jukumu lililompa heshima ya mwalimu (mwalimu).

Nyerere alitumia muda mwingi wa 1962 akizunguka nchi nzima kusikiliza na kuzungumza na viongozi wa ndani wa TANU na cheo na faili, lakini hakuhusika na ujenzi wa shirika wala, kwa wakati huo, na kuongeza ushiriki wa TANU katika kutunga sera au utawala. Aliendelea kuchukulia serikali na sio chama kuwa ndio chimbuko la sera.
Kazi yake kuu ilikuwa kufundisha, ambayo aliifanya kwa mdomo na kwa maandishi. Katika vijitabu alivyotayarisha wakati huu alidai kuwa jamii ya Kiafrika ilikuwa na utaratibu wa kimaadili ambapo watu walijali wao kwa wao lakini kwamba utaratibu huu ulikuwa unatoa nafasi kwa umiliki wa fujo. Dhana hiyo ya utaratibu wa kimaadili wa kitamaduni wa Kiafrika inasisitiza dhana ya Nyerere ya ujamaa, ambayo, inazidi kuwa sehemu muhimu ya ujumbe wake. Lakini wakati huu alijishughulisha na taasisi za ujamaa bali na maadili yake, na hakujishughulisha na Umaksi au mawazo mengine ya Kizungu kuhusu ujamaa bali kile alichofikiria kuwa mizizi yake ya Ujamaa.
Kwa maoni yake, katika jumuiya za kitamaduni za Kiafrika, wanajamii waliitunza jumuiya hiyo, na jumuiya hiyo iliwajali wanachama wake. Watu binafsi hawakuwa na haja wala hamu ya kunyonya kila mmoja. Mitazamo hii ilibidi aihifadhi na kwa kiwango ambacho walikuwa wamepotea, walipatikana. Mnamo 1962 Nverere aliandika: "Ujamaa wa kweli ni mtazamo wa akili. Kwa hivyo ni juu ya watu wa Tanganyika ... kuhakikisha kuwa mtazamo huu wa ujamaa haupotei kupitia vishawishi vya kujinufaisha kibinafsi (au kutumia vibaya vyeo). wa mamlaka) .

Yaliyounganishwa na dhana hii ya msingi ya tabia ya msingi ya jamii ya kitamaduni ya Kiafrika yalikuwa mapendekezo ya sera ya jumla ya Nyerere: kwa sababu unyonyaji - kuishi kwa kazi ya wengine - haukuwa wa haki na unaharibu maelewano ya kijamii, unyonyaji kama huo lazima ukomeshwe. Kwa kweli katika jamii ya vijijini hiyo ilimaanisha mwisho wa umiliki wa mtu binafsi wa ardhi. Hii ilionekana kuruka mbele ya dhana ya awali kwamba wakulima wanaoendelea walipaswa kutiwa moyo na kwamba mafanikio yao, labda katika soko, yalikuwa kuwa mfano kwa wengine. Zaidi ya hayo, tofauti kubwa za mapato lazima zizuiwe. Msomi wa uchumi wa Asia na Ulaya hakupaswa kurithiwa na Mwafrika.
Jukumu la chama pia lilishughulikiwa, si kwa muundo na utendaji wa kina bali kuhusiana na mafanikio ya jamii yenye uadilifu na maadili. TAW ilikuwa ni kuwataka wanaTanganvika kufanya kazi kwa bidii, hasa ili kuondokana na umaskini, lakini ilikuwa kufanya hivyo kwa kuishi na kujifunza miongoni mwao, si kwa kuwawekea fikra zake. Viongozi zaidi wa TANU walipaswa kuruhusu, hata kuhimiza ukosoaji wa ndani.

Source : GlobalSecurity.org
Nyerere alikuwa msanii sana. Alijiuzulu uwaziri mkuu ili awe Rais na si vinginevyo. Kawaida nchi ikiwa jamuhuri inaongozwa na Rais, na 1962 ndipo Tanzania ilikuwa jamuhuri.
 
Nyerere alikuwa msanii sana. Alijiuzulu uwaziri mkuu iliawe Rais na si vinginevyo. Kawaida nchi ikiwa jamhuri inaongozwa na Rais, na 1962 ndipo Tanzania ilikuwa jamhuri.

Historia inasema mambo mengi pengine kina Mzee Butiku wanaweza kutuambia historia sahihi, ni kwenda kijijini kuweka mikakati ya kuimarisha chama kilichokosa ushawishi, au madai ya rushwa au ni kutaka kuwa rais wa Jamhuri ya Tanganyika
 
PROF TIBAIJUKA: MISSION YA MBOWE HAIJAKAMILIKA!

“Nimemsikiliza huyu Katibu. Sidhani kama anafahamu haja ya kutenganisha Chama Tawala na Chama cha Upinzani. Anaongea kama aliyekariri mambo. Anatumia mfano wa Zitto Kabwe (@zittokabwe) kuachia ngazi.

Mbowe alielezea vizuri jana suala la Mission yake hata kama sisi wanaCCM tunayo yetu ya kumpinga. Sasa je aachie ngazi kwani kaikamilisha? Nyerere angeachia ngazi mapema hili Taifa lingeimarika?

Hivo mimi nadhani tunahitaji elimu zaidi ya uraia kutofautisha uongozi wa Vyama na uongozi wa nchi."

Prof Anna Tibaijuka (@AnnaTibaijuka) ameandika haya kwenye moja ya group la WanaCCM!
Very good explanation.
 
Back
Top Bottom