Profesa Assad aliumia sana kuvuliwa u-CAG. Mpaka leo namwona bado ana chuki kubwa sana. Tatizo ni nini?

Hakujua kuwa kuna tofauti ya kuingoza nchi na kuna tofauti ya kuongoza taasisi. Ye taasisi aliifanya nchi yake yenye mamlaka zote. Kuna wakati katika mpango wa kubana matumizi alipunguziwa bajeti, aliwaka sana. Akasema watu wake watashindwa kwenda nje kwa ajili ya mafunzo na kujiendeleza. Kifupi aliamini ile ni taasisi huru isiyoguswa kwa lolote na yeye ndio rais wake.
 
Mara anataka kiongozi anayesikiliza, hivi kiongozi akisikiliza kila mtu tutafika.
Kuwasikiliza watu, wananchi waliokupa nafasi uliyopo ni jukumu muhimu kwako.
Ili uweze kuelewa waliyonayo na kuweza kuwajibu na kujua cha kutatua, watakiwa kuwa na mfumo/mifumo imara. Lakini sio kwa mtindo wa one man show.
 
Aliyemuumiza mbona nae kaumizwa?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Unajuaje anaumia?
 
Au midevu ndiyo matusi [emoji848][emoji1787]
Inter...
Ustaarabu ni kuuliza kitu usichokijua kwa adabu.

Mathalan ungeuliza, "Kwani kusema ""midevu"" ni matusi?"

Naam "midevu" ni lugha ya kutuniza.

Kutuniza kunakwenda sambamba na kutukana.

Haya mimi nakueleza kwa malezi niliyopata mimi kwa wazazi wangu.

Yawezekana kwenu haya si matusi.
 
Prof Asadi sio mtu wa hivyo kama unavyomfikiria, yaaani kwa nafasi yake ya uanazuoni lazima aseme na ashauri pale anapoona kuna haja ya kufanya hivyo.
Kama angekuwa mtu wa kusaka vyeo asingesimama imara kutetea kile anachoamini, huyu ni mtu wa dini na mtu anayejishusha sana.
Msomi mwenye msimamo na weledi wa hali ya juu.
 
Ndivyo tunavyotamani tuwe na taasisi huru
Zisizoingiliwa kirahisi kwa maslahi ya taifa haswa wakaguzi wa fedha zetu
Sio mtu anaingilia tu taasisi kwa maslahi yake binafsi
 
Aliondolewa kimagumashi sana
Yule kichomi ndugae sijui yuko wapi sasa?
Mwendazake kaacha athari kubwa sana na kuidumaza nchi yetu
Tutachukua hata miaka ishirini ili kuamka tena!
kwani hana alternative nyingine ya maisha isipokiwa u CAG, Kama alibweteka ndo imekula kwake!! madaraka ni kupokezana ,mbona mwenzie ndugai hakunji moyo !!? Mizee mingine hovyo kabisa!!
 
tangu ndugai ame step out,hatujaona akihangaika mitandaoni au redioni kutoa maneno ya kinyaa Kama mzee assadi,yaani mzee hatulizi ubongo ukatulia ,tangu aondoke wamle kichwa kwenye uCAG anahangaika kila siku kubwata mitandaoni ,atulize kichwa ,maisha yaendelee.
 
Hayo ni mawazo yako tu.
 
Bila kusema, yatarudia mengine...
 
Wigwa,
Una ushahidi wa haya usemayo?
Ushahidi uko wazi. CAG ni nafasi ya kuteuliwa kwa vipindi visivyozidi viwiwli vya miaka mitano mitano, siyo ya kuteuliwa kwa miaka kumi kama ambavyo Assad alivyotaka. Assad amewahi kusema kuwa anachukia kusikia kuwa yeye ni CAG mstaafu kwani anataka atambuliwe kuwa ni CAG aliyesimamishwa kabla ya muda wake, which does not make sense. Uteuzi wa CAG uko kwenye mamlaka ya rais ambaye atateua CAG kila baada ya miaka mitano, anaruhusiwa kumteua yule yule aliyepo kwa mara nyingine (kama hajamaliza vipindi viwili) na vile vile anaweza kubadilisha akaweka mwingine.

Ni kwa vile Magufuli alifariki, ni vigumu kujua kuwa alikuwa amepanga kumpa kazi gani tofauti na ya u-CAG kwa vile alikuwa anapenda sana wasomi kama Nyerere. Alimfukuza Andengenye hadharani lakini baadaye akamfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Aliwahi kuwafukuza akina Simbachawene na Mwigulu tena hadharani kabisa lakini baadaye akawapa kazi nyingine.

Huyu Assad aliumia sana na mpaka leo inamuumiza badala ya kuamini kuwa Mungu akifunga mlango mmoja atafungua mwingine. Wasomi hujivunia mafanikia yao na kuyaacha yajitangaze yenyewe, hawalalamikii kuonewa. Enstein alifelishwa Doctorate mara tatu na profesa wake Minkowski lakini baada ya kutoka hapo, maisha yakaendelea kama tunavyomjua Einstein leo. Watu dhaifu huwa na tabia za kulalamika wakidai kuonewa kila siku.
 
Mohamed Said siyo mtu wa Tanga, fanya utafiti dogo, unaaibisha wazazi kukupeleka shule lakini ujinga haujatoka kichwani....[emoji3]
 
Kichuguu...
Huo ndiyo ushahidi wako...

Hapana shida.

Sasa mimi nikisema kuwa labda kinachokuhangaisha ni hasad na chuki nini jibu lako?
Inaelekea hukuelewa jibu langu kwa vile nilichanganya mambo mengi, ila ushahidi kamili ni huu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…