Profesa Assad aliumia sana kuvuliwa u-CAG. Mpaka leo namwona bado ana chuki kubwa sana. Tatizo ni nini?

Profesa Assad aliumia sana kuvuliwa u-CAG. Mpaka leo namwona bado ana chuki kubwa sana. Tatizo ni nini?

Hata afya yake imezorota sana anaoenakana kuwa na maumivu makubwa.

Huyu Assad ni msomi mzuri tu na anaweza pata kazi sehemu mbalimbali ila shida nadhani ni mihemko, jazba na chuki vinamfanya aumie. Anapaswa akubali tu kuwa ilikuwa ni wakati wake kupisha wengine asibebe uchungu wa kuona alidhalilishwa sana.

Atajiumiza bure mtu mwenyewe aliyefanya hivyo ni Marehamu so a-move on tu maisha yaendelee asikunjane moyo.
Kawapiga Sukuma gang kunako penuewe
 
Sasa unauliza tatizo nini wakati Mwanzo ushasema.. we jamaa vp,, kwanza akilal@mika Kuna shida gani wakati uhuru wa kuongea anao..!!!
 
Alidhalilishwa sana na yule 'mungu mtu' na yule bwana 'mburuza miguu'
Taaluma yake ndio ilikuwa inaongea lakini kwa hao wawili walitawaliwa na ujinga
 
Hata afya yake imezorota sana anaoenakana kuwa na maumivu makubwa.

Huyu Assad ni msomi mzuri tu na anaweza pata kazi sehemu mbalimbali ila shida nadhani ni mihemko, jazba na chuki vinamfanya aumie. Anapaswa akubali tu kuwa ilikuwa ni wakati wake kupisha wengine asibebe uchungu wa kuona alidhalilishwa sana.

Atajiumiza bure mtu mwenyewe aliyefanya hivyo ni Marehamu so a-move on tu maisha yaendelee asikunjane moyo.
uzuri wa kila kitu ukutane nacho kwanza ndo utajua kuwa kwann kanga ana manyoya
 
Na bahati mbaya sana kwake HARUHUSIWI kikatiba kuajiriwa na taasisi yoyote inayokuwa audited na CAG!
Anayekagua fedha za Sweden, Finland na Norway kwenye mradi wowote huku Tanzania ni ASSAD!
Avarage kwa mwezi anapa around 42,000 USD! Kwa hii hela hawezi kuwa na njaa
 
Tatizo letu kila jambo la kusemea nchi,anaeongea anaonekana na chuki binafsi,hiviii nani anapaswa kuiongelea Tanzania tukawa na Amani nae?

Daudi mfalme,wakati anampiga Goliath, Saul alimsifia sanaa,kijana mdogo ameweza kuwapa ushindi.

Lakini alipoanza kumkosoa kuhusu namna anavyotawala,akawa adui wa nchi. Tukitaka kufanikiwa kama nchi ni vyema tujifunze kumsikiliza mtu nini anaongea kuliko kuangalia wapi ametokea. Tanzania ni yetu sote.
Sasa mkuu ndio iwe mtu msomi na degree zako za uchumi kutwa unakesha kumuwaza Marehemu...kweli jamani
 
Hata afya yake imezorota sana anaoenakana kuwa na maumivu makubwa.

Huyu Assad ni msomi mzuri tu na anaweza pata kazi sehemu mbalimbali ila shida nadhani ni mihemko, jazba na chuki vinamfanya aumie. Anapaswa akubali tu kuwa ilikuwa ni wakati wake kupisha wengine asibebe uchungu wa kuona alidhalilishwa sana.

Atajiumiza bure mtu mwenyewe aliyefanya hivyo ni Marehamu so a-move on tu maisha yaendelee asikunjane moyo.
Sukuma gang at work. Yule mungu wenu alikuwa chizi
 
Hiyo CV umeirudia mara kadhaa ukidhani ni kubwa sana bila hata kuangalia scholarship content yake.

Consultancy report ni sehemu ndogo sana ya scholarship kwani ni matumizi ya standard knowledge katika kutoa jawabu ya swala lililopo mezani. Ingekuwa kila consultancy report ni sifa kuu ya scholarship ya mtu basi consultant engineers wote duniani wangekuwa na sifa zaidi ya Assad kwani ndiyo kazi zao za kila siku.

Uandishi wa vitabu kwa kufanya compilation ya information ambayo tayari ipo duniani ila kwa kutumia ama lugha rahisi au kwa kuipangilia vinginevyo pia ni sehemu ndogo tu ya scholarship.

Scholarship inapimwa kwa contribution ya new knowledge, ambayo inaweza kufanywa kwa kutumia papers au monographs ambapo content yote ni mpya. Vitabu ulivyoonyesha hapo vyote ni compilation ya known information na wala havifikii sifa ya kuwa research monograph.

Iwapo Assad angewa ni scholar mkubwa kama unavyota kuaminisha umma, asingekaa kuwa Senior Lecturer wa UDSM kwa miaka 11 katika institution ambayo hupandisha vyeo kila baada ya miaka mitatu, na kutumia miaka 10 kupata doctorate kutokea Masters degree. Yeye ni mtu wa kawaida tu.
Kichuguu,
Unajua politics za Tanzania unapokuwa Muislam?

Ikiwa wewe ni mkweli hutokosa kujua kuwa nchi ina tatizo kubwa inapokutana na watu wa aina ya Dau, Assad na Njozi.
 
Hata afya yake imezorota sana anaoenakana kuwa na maumivu makubwa.

Huyu Assad ni msomi mzuri tu na anaweza pata kazi sehemu mbalimbali ila shida nadhani ni mihemko, jazba na chuki vinamfanya aumie. Anapaswa akubali tu kuwa ilikuwa ni wakati wake kupisha wengine asibebe uchungu wa kuona alidhalilishwa sana.

Atajiumiza bure mtu mwenyewe aliyefanya hivyo ni Marehamu so a-move on tu maisha yaendelee asikunjane moyo.
Mama mteue Assad awe Balozi au mwenyekiti wa Bodi
 
Siyo kweli kwamba anaweza kupata kazi popote ingekuwa hivyo angeshasepa, hawa watu huwa mnawa overrate sana.

Kwa hali ya kawaida kama kweli ni Profesa na amebobea kwenye fani yake angerudi Chuoni kufundisha na Chuoni simaanishi Tanzania ni oversees lkn siajabu hana credentials za kupewa chair popote na ndio maana anajibizana na kusutana kila siku hana kazi ya kufanya hata tu kuandika vitabu vya fani yake hafanyi, yuko soo petty kama mtoto!
Profesa ana hasira alichofanyiwa na hayati Magufuli, ana nongwa fulani akiona kama vile alinyanyaswa na kudhalilishwa, hajaweza kusamehe.
 
Yawezekana Hegemony ya Uprofesa ndiyo inamtesa! Ukibeba vyeo kichwani badala ya uungwana na kujishusha lazima uteseke!
 
Anayekagua fedha za Sweden, Finland na Norway kwenye mradi wowote huku Tanzania ni ASSAD!
Avarage kwa mwezi anapa around 42,000 USD! Kwa hii hela hawezi kuwa na nja
Nimepiga hesabu ya US Dollar 1 = TZ Sh. 2300. Hivyo 42000 X 2300 = 96,600,000/=. kwa mwezi. Halafu anaendesha IST!!!!!
 
Kichuguu,
Unajua politics za Tanzania unapokuwa Muislam?

Ikiwa wewe ni mkweli hutokosa kujua kuwa nchi ina tatizo kubwa inapokutana na watu wa aina ya Dau, Assad na Njozi.
Siyo kweli. Kuna scholars kama akina profesa Mawenya (jina lake ni Awadh Mawenya), Professor Shivji (jina lake ni Issa Shivji), na Professor Haroub Othman ambao walikuwa na clear scholarship records kuliko hiyo uliyoleta hapa; wote hao ni Waislamu. Infact Issa shivji ndiye aliyepiga critic kubwa sana kwenye professorial inaugural lecture ya Professor Kighoma Ali Malima. Siyo kila jambo tuliangalie kwa dini ya mtu. Dini ni imani ya mtu binafsi, siyo institution ya kitaifa. Mimi nikiwa UDSM Engineering nilikuwa na marafiki wengi sana ambao ni waislamu na wala walikuwa hawatumii dini zao katika kazi na mahusiano yao; in fact nakumbuka wawili waliishia kuoa wanawake amabao ni wakristo.
 
Na wewe thibitisha kinyume chake. Leo tutapingana humu ingawa sote ni wamoja. Maana hata mimi nilipata mwaliko kama wako kuwa tuje mtetea kwa ile ID yangu nyingine.
Mimi nimeanza kukuuliza uthibitishe ulichodai. Thibitisha.

Pia, mimi sina mzigo wa kuthibitisha lolote, kwa sababu sijatoa madai yoyote.
 
Siyo kweli. Kuna scholars kama akina profesa Mawenya (jina lake ni Awadh Mawenya), Professor Shivji (jina lake ni Issa Shivji), na Professor Haroub Othman ambao walikuwa na clear scholarship records kuliko hiyo uliyoleta hapa; wote hao ni Waislamu. Infact Issa shivji ndiye aliyepiga critic kubwa sana kwenye professorial inaugural lecture ya Professor Kighoma Ali Malima. Siyo kila jambo tuliangalie kwa dini ya mtu. Dini ni imani ya mtu binafsi, siyo institution ya kitaifa. Mimi nikiwa UDSM Engineering nilikuwa na marafiki wengi sana ambao ni waislamu na wala walikuwa hawatumii dini zao katika kazi na mahusiano yao; in fact nakumbuka wawili waliishia kuoa wanawake amabao ni wakristo.
Kichuguu,
Naomba nianze na Prof. Awadh Mawenya.

Hapo chini ni jinsi nilivyomwandika Prof. Mawenya katika kitabu changu, ''Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama,'' (2020):

''Sheikh Abdallah Minhaj alipofika Machame alikuta tayari jengo la shule iliyojulikana kama Chagga Muslim School limesimama.

Shule ilikuwa imeshajengwa na walewale wanafunzi wa shule hii ndiyo walikuwa wanafunzi wa madrasa.

Wazazi wakahamasika kupeleka watoto wao shule na kwenye madras ya Sheikh Abdallah Minhaj pale msikitini.[1]

Katika wanafunzi wake ambao walikuja kufika mbali sana ni Prof. Awadh Sadik.

Mwanafunzi wake huyu alishika nafasi ya kwanza katika hesabu kwenye mitihani ya Cambridge mwaka wake katika nchi zote za Jumuiya ya Madola.

Awadh Sadik Mawenya alikuja kuwa Mwafrika wa kwanza kuwa mkuu wa Idara ya Uhandisi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Shule hii imetoa wanafunzi wengi ambao baada ya kuhitimu shule ya msingi waliingia katika shule za serikali wakiwa na elimu nzuri ya dini yao na wakaja kuwa raia wema katika maendeleo ya nchi na wazazi wenye busara katika familia zao.

Baadhi ya wanafunzi hawa ni watoto na wajukuu zake mwenyewe Mzee Rajab.''

1653168572005.png

[1] Angalia jedwali la mchango wa kuendesha shule na madrasa 1949.

Prof. Issa Shivji tunafahamiana vizuri halikadhalika marehemu Prof. Haroub Othman.

Hapa katika kuwaeleza walimu wangu hawa wawili nataabika khasa kwa kuwa unawanasibisha na Uislam.

Uislam hauna nguvu ya kuweza kutumika popote katika sehemu za maamuzi si serikalini, si kwenye bunge si popote kwani huko kote hauna nguvu.

Wenye nguvu wanafahamika.

Ila nitakueleza kitu kimoja ambacho Prof. Haroub Othman alinieleza tena tumesimama nje ya Msikiti wa Ibadh baada ya yeye kusoma kitabu cha Abdul Sykes.

Alinambia alikwenda kumuona Mwalimu Nyerere na kitabu changu kwa kuwa kuna mambo mengi aliyosoma mle yalimfadhaisha sana.

Alitaka apate ukweli wa yale niliyoandika kuhusu Nyerere kutoka kinywani kwake Mwalimu.

Angalia picha hapo chini siku Prof. Shivji alipokuja nyumbani kwangu Magomeni Mapipa akiwa na Prof. Saida na Dr. Kamatha kunihoji kuhusu historia ya Mwalimu Nyerere wakati walipokuwa wanafanya utafiti wa kitabu cha Mwalimu.

Ilikuwa mwaka wa 2013.
Sitokuambia amesema nini kuhusu mimi katika kitabu cha Mwalimu.

Nakuachia usome mwenyewe.

View attachment 2233582
 
Hata afya yake imezorota sana anaoenakana kuwa na maumivu makubwa.

Huyu Assad ni msomi mzuri tu na anaweza pata kazi sehemu mbalimbali ila shida nadhani ni mihemko, jazba na chuki vinamfanya aumie. Anapaswa akubali tu kuwa ilikuwa ni wakati wake kupisha wengine asibebe uchungu wa kuona alidhalilishwa sana.

Atajiumiza bure mtu mwenyewe aliyefanya hivyo ni Marehamu so a-move on tu maisha yaendelee asikunjane moyo.
Hivi hana pesa hata milion 250 hana?
 
Back
Top Bottom