Siyo kweli. Kuna scholars kama akina profesa Mawenya (jina lake ni Awadh Mawenya), Professor Shivji (jina lake ni Issa Shivji), na Professor Haroub Othman ambao walikuwa na clear scholarship records kuliko hiyo uliyoleta hapa; wote hao ni Waislamu. Infact Issa shivji ndiye aliyepiga critic kubwa sana kwenye professorial inaugural lecture ya Professor Kighoma Ali Malima. Siyo kila jambo tuliangalie kwa dini ya mtu. Dini ni imani ya mtu binafsi, siyo institution ya kitaifa. Mimi nikiwa UDSM Engineering nilikuwa na marafiki wengi sana ambao ni waislamu na wala walikuwa hawatumii dini zao katika kazi na mahusiano yao; in fact nakumbuka wawili waliishia kuoa wanawake amabao ni wakristo.
Kichuguu,
Naomba nianze na Prof. Awadh Mawenya.
Hapo chini ni jinsi nilivyomwandika Prof. Mawenya katika kitabu changu, ''Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama,'' (2020):
''Sheikh Abdallah Minhaj alipofika Machame alikuta tayari jengo la shule iliyojulikana kama Chagga Muslim School limesimama.
Shule ilikuwa imeshajengwa na walewale wanafunzi wa shule hii ndiyo walikuwa wanafunzi wa madrasa.
Wazazi wakahamasika kupeleka watoto wao shule na kwenye madras ya Sheikh Abdallah Minhaj pale msikitini.
[1]
Katika wanafunzi wake ambao walikuja kufika mbali sana ni Prof. Awadh Sadik.
Mwanafunzi wake huyu alishika nafasi ya kwanza katika hesabu kwenye mitihani ya Cambridge mwaka wake katika nchi zote za Jumuiya ya Madola.
Awadh Sadik Mawenya alikuja kuwa Mwafrika wa kwanza kuwa mkuu wa Idara ya Uhandisi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Shule hii imetoa wanafunzi wengi ambao baada ya kuhitimu shule ya msingi waliingia katika shule za serikali wakiwa na elimu nzuri ya dini yao na wakaja kuwa raia wema katika maendeleo ya nchi na wazazi wenye busara katika familia zao.
Baadhi ya wanafunzi hawa ni watoto na wajukuu zake mwenyewe Mzee Rajab.''
[1] Angalia jedwali la mchango wa kuendesha shule na madrasa 1949.
Prof. Issa Shivji tunafahamiana vizuri halikadhalika marehemu Prof. Haroub Othman.
Hapa katika kuwaeleza walimu wangu hawa wawili nataabika khasa kwa kuwa unawanasibisha na Uislam.
Uislam hauna nguvu ya kuweza kutumika popote katika sehemu za maamuzi si serikalini, si kwenye bunge si popote kwani huko kote hauna nguvu.
Wenye nguvu wanafahamika.
Ila nitakueleza kitu kimoja ambacho Prof. Haroub Othman alinieleza tena tumesimama nje ya Msikiti wa Ibadh baada ya yeye kusoma kitabu cha Abdul Sykes.
Alinambia alikwenda kumuona Mwalimu Nyerere na kitabu changu kwa kuwa kuna mambo mengi aliyosoma mle yalimfadhaisha sana.
Alitaka apate ukweli wa yale niliyoandika kuhusu Nyerere kutoka kinywani kwake Mwalimu.
Angalia picha hapo chini siku Prof. Shivji alipokuja nyumbani kwangu Magomeni Mapipa akiwa na Prof. Saida na Dr. Kamatha kunihoji kuhusu historia ya Mwalimu Nyerere wakati walipokuwa wanafanya utafiti wa kitabu cha Mwalimu.
Ilikuwa mwaka wa 2013.
Sitokuambia amesema nini kuhusu mimi katika kitabu cha Mwalimu.
Nakuachia usome mwenyewe.
View attachment 2233582