Profesa Assad amkabidhi ofisi CAG mpya, hakuona haja ya kupiga danadana

Profesa Assad amkabidhi ofisi CAG mpya, hakuona haja ya kupiga danadana

Mkuu nisingependa kumwaga ushahidi humu JF, baadhi yao ni waheshimiwa sana na sio vizuri kuanza kugeuka Cyprian Musiba, itoshe tu kwa ushahidi wangu huu wa kimazingira kuaminika.
Ha haha! Mbona unategesha upande mmoja tuu?kuaminika?
Ungesema itoshe kuaminika au kutoaminika! Maana Mimi ningechaguwa ushahidi huo wa kimazingira kuto aminika!
Ila NIMEKUELEWA.
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa

CAG apumzike aache kutafuta huruma ya Wananchi yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo Kila mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG

Muda wake umeisha apumzike amefanya kazi yake

Aache kutumika na wanasiasa wasaliti wa nchi
Zimbabwe watu kama wewe walifanya Mugabe aharibu nchi kwa kumchekea
 
Utafiti ulisema wengi wanaounga mkono CCM ni watu ambao hawakwenda shule kabisa, walioshia la saba na wachumia tumbo!
IMG-20180405-WA0006.jpeg
 
Kwani huna Comment Nyingine zaidi ya hii Mkuu? Naona kila uzi unaomhusu CAG mpya unaleta maneno haya haya.
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa

CAG apumzike aache kutafuta huruma ya Wananchi yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo Kila mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG

Muda wake umeisha apumzike amefanya kazi yake

Aache kutumika na wanasiasa wasaliti wa nchi
 
Assad kaiharibu na kuivunjia heshima sana hiyo ofisi.

Zitto kamuharibu huyu mzee..akalime sasa Unguja.

Viva Magufuril
Mzee Assad wala hana kinyongo na vilaza kama nyinyi...ni suala la muda tu watanzania watajua nyeupe na nyeusi!
 
Ndugai na yule kichaa mwingine wamefurahi sana sasa tutegemee kodi zetu kuanza kupigwa kiholela na hili gege la majizi linalojitia uzalendo. Hapa kazi ni wizi tu
Inauma sana mkuu...sasa tunaenda kumalizia International Airport Chato, kisha tunajenga uwanja wa mpira wa kisasa...hakuna wa kutukagua!
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa

CAG apumzike aache kutafuta huruma ya Wananchi yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo Kila mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG

Muda wake umeisha apumzike amefanya kazi yake

Aache kutumika na wanasiasa wasaliti wa nchi
Haya ni maneno ya mtu anayewashwa washwa
 
Hiki ni kitendo kilichofanyika bila kuchelewa , hajataka kuleta longolongo ili waseme kuna mafaili yametoroshwa .

Kila la heri Profesa Assad
******

Prof. Assad:
"Hii ni taasisi na makabidhiano ya taasisi yanaenda kwa maandishi, kwa hiyo makabidhiano kwa maandishi yatafanyika Dodoma kwa sababu ndiyo kule makao makuu yetu yalipo"

"Kazi ya CAG ni kusaini ripoti lakini ripoti unachukua wajibu wa kazi ya watu wengi sana, ambao waliifanya maeneo mbalimbali hapa Tanzania, kwa hiyo nukta yangu ni kuwatazama vizuri sana watu hawa"

"Kama kuna yeyote nilimkosea kwenye utendaji wetu wa kazi basi anisamehe na mimi kuna kuna mambo alinikosea nimemsamehe."

"Baada ya hapa mimi nitafanya kazi ya kulima kwa sababu miezi 2 iliyopita nilianza kuwekeza kwenye kulima, wakinihitaji watu wa Mjini nitakuja, kuhusu changamoto ni nyingi nimepitia mnataka niseme hapa nitatia ukakasi hakuna haja ya kutia ukakasi."

"Nimepokea ofisi hii kutoka kwa Uttoh miaka mitano iliyopita naamini sikufanya uharibifu wowote mimi naamini mabadiliko yanaweza kutokea, lakini yatokee kwenye namna ilivyopangwa vizuri."

CAG Kichere :
"Kama kutakuwa na mabadiliko yatafanyika kwa umakini mkubwa ili tusiharibu mfumo wa utendaji kazi."

"Nimefanya kazi TRA najua ugumu wa kukusanya mapato, nimekuja kulinda mapato, tena nitalinda kwa wivu mkubwa sana, sitakuwa na simile kwa watu wanaotumia mapato ya Serikali vibaya."

"Kama kulikuwa na mahusiano hafifu nitaimarisha mahusiano kati ya Ofisi ya CAG na Bunge."
Mungu ambariki ni muadilifu tutamkumbuka kwa uzalendo wake
 
Mada inahusu Kukabidhi ofisi acha siasa zako wapinzani wamefikaj apa mkuu?
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa

CAG apumzike aache kutafuta huruma ya Wananchi yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo Kila mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG

Muda wake umeisha apumzike amefanya kazi yake

Aache kutumika na wanasiasa wasaliti wa nchi
Kwani unateseka?
 
Back
Top Bottom