Profesa Kabudi aitambulisha dawa ya COVIDOL nchini Ufaransa, wenyeji wake waikubali na kuipokea

Profesa Kabudi aitambulisha dawa ya COVIDOL nchini Ufaransa, wenyeji wake waikubali na kuipokea

nitoe ushuhuda wa hii dawa! ni dawa nzuri japo inauzwa kwa gharama kubwa! imemponya mgonjwa wetu alikuwa na changamoto ya kupumua alikuwa anatumia oxyegen baada ya kuanza kutumia hii dawa kiukweli tulianza kuona mabadiliko ya mgonjwa na kila alipokuwa anapata nafuu sana
 
Nasikia wafaransa walipoipokea wakamwambia ainywe kwanza yeye alipoinywa wakaona ametumbua tu mimacho ameduwaa wakamwambia abaki nayo anywe chupa zote peke yake
 
Kama ni kweli, basi hii serikali yote ya Magufuli ni visebengo!
Mkuu umenifanya nicheke Sana, Ila nikapata kijiswali, Kwa nini unaogopa Vya kwetu kuvitangaza?

Kama kinaponya kunashida gani kukitangaza mkuu" Dawa Bora Ni Ile inayoponya Haijalishi Muonekano wake kwamba hauvutii, Ila kama inaponya, wazungu watupishe na chanjo zao
 
Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi amewaeleza watanzania waishio Ufaransa kuwa Tanzania imechukua hatua zote muhimu katika kupambana na Corona.

Prof Kabudi ambaye yuko ziarani nchini Ufaransa ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kutafiti na hatimaye kugundua dawa ya covido ambayo imesaidia wengi.

Prof Kabudi alitoa chupa ya dawa ya covido na kuitambulisha kwa wenyeji wake ambao waliipokea na kuipongeza Tanzania kwa hatua hiyo kubwa waliyofikia

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Makubwa mbona wanakimbilia hospitalini kwenye mitungi ya oxygen😀😀😀😀😀😀😀
 
Ina maana hawa vigogo wanaofariki kwa Corona hawapewi hiyo dawa?
 
Kwahivo ziara ya kikazi ilikua kupeleka huo mchanganyo wa pilipili kichaa?
 
kabudi, kabudi ,kabudi nimekuita mara tatu jifanye hujui kua dawa inayotakiwa kupigiwa chapuo ni BUPIJI...
 
Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi amewaeleza watanzania waishio Ufaransa kuwa Tanzania imechukua hatua zote muhimu katika kupambana na Corona.

Prof Kabudi ambaye yuko ziarani nchini Ufaransa ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kutafiti na hatimaye kugundua dawa ya covido ambayo imesaidia wengi.

Prof Kabudi alitoa chupa ya dawa ya covido na kuitambulisha kwa wenyeji wake ambao waliipokea na kuipongeza Tanzania kwa hatua hiyo kubwa waliyofikia

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Hata Ufaransa kuna Wasukuma ambao si Wafaransa ndo aliweza kuelewana nao maana kama maPhD wenzake, Prof Kingereza kimempita upande, Kifaransa ndo sifuri kabisa, Wafaransa lazima wanamshangaa kuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi iliyokuwa Koloni ya Waingereza. Ufaransa hakuna Mfaransa mjinga hata mmoja atayepokea dawa ya ugonjwa wowote kutoka Chato hata ikipitishiwa kwa Wasukuma wanaoishi Paris. Watanzania wajifunze lugha za Kimataifa wawe wa kimataifa!
 
Jealous is like a sand in your eyes,it can stop your eyes from seeing clearly,Covidol and Bupiji were all introduced in Tanzania,but as you are full of negativity to your government, you heard not.
Imetambulishwa tu hakuna data zilizotolewa kuhusu hiyo dawa imesaidia wangapi, waliosaidiwa wana umri gani, ina mafanikio ya asilimia ngapi, na hatujaambiwa mpaka sasa inasaidia waliopata huo ugonjwa au ambao hawajapata Covid. Kwa ujumla ni Kinga au Tiba.

Jealousy inaingiaje kivipi. Yaani wote tufe au.

Hata waliopona chupuchpu almanusra kama Mhe. mgeni pale Ben Mkapa na wengineo walipumwa hawajasema kama walliibwia hiyo.

Hawa wakubwa wakienda safari za nje wakipata kinga kimya kimya utajua ?

Hao Diaspora unadhani walikuwa hawajui hiyo kitu, sana sana angeenda profesor wa NIMR ingeeleweka.
 
Jealous is like a sand in your eyes,it can stop your eyes from seeing clearly,Covidol and Bupiji were all introduced in Tanzania,but as you are full of negativity to your government, you heard not.
Wampe waziri mpango
 
Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi amewaeleza watanzania waishio Ufaransa kuwa Tanzania imechukua hatua zote muhimu katika kupambana na Corona.

Prof Kabudi ambaye yuko ziarani nchini Ufaransa ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kutafiti na hatimaye kugundua dawa ya covido ambayo imesaidia wengi.

Prof Kabudi alitoa chupa ya dawa ya covido na kuitambulisha kwa wenyeji wake ambao waliipokea na kuipongeza Tanzania kwa hatua hiyo kubwa waliyofikia

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Hiyo covidol ndio ile yenye mchanganyiko wa pilipili kichaa tano au?
 
Back
Top Bottom