Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
Unajua huko mbele inabidi tufanyeyje? Ili kudhibiti ubora na sustatinability ya vyama vya upinzani, inabidi tuje tuongeze kipengele kwenye Katiba, kwamba kila inapofikia muda wa Uchaguzi Mkuu wapinzani wanapokuwa wananadi ilani zao za uchaguzi, kila chama kiwaeleze wanachi angalau objective moja, ambayo kitaitekeleza bila kukosa, ndani ya miaka mitano ijayo iwapo tu chama hicho hakitafanikiwa kuchukua dola. Kwamba vyama vya upinzani ambacvyo havitafanikiwa kuchukua dola, angalau navyo vitoe ahadi kwa wananchi ya nini vitanya ndani ya miaka mitano ijayo, kwa mfano kama:Chadema wanajidharau sana aiee!
Wanaamini hawawezi kufanya chochote isipokuwa mzungu tu.
Hizi akili ndio maana yule mgombea wao baada ya dili la urais kubuma akaona hawezi kuishi tz maana keshazoea kwa wazungu.
"Sisi CHADEMA, ndani ya miaka mitano ijayo tutajenga angalau kilomita moja ya barabara kwa kiwango cha lami, au vyumba 200 vya madarasa ya shule za Sekondari na/ Msingi, mahali popote pale ndani ya JMT.
Na ahadi hii watatakiwa kuja kuisema kama waliitekeleza au hawakuitekeleza kwenye kinyang'anyiro kinachofuata watakapokuwa wanomba ridhaa nyingine tena kwa wanachi kwa mara nyingine kwenye uchaguzi unaofuata.
Hii ni kwa sababu vyama vya upinzani kwa umoja wao, au kama chama kimoja kimoja hawashindwi kujenga angalau vyumba kadhaa vya madarasa ya shule za msingi, au kilomita moja au hata 10 tu za barabara kwa kiwango cha lami, ndani ya miaka mitano.
Kwa hiyo Kikatiba wanatakiwa wapewe majukumu ya aina hiyo ili nao wawe na kazi nyingine ya kufanya nje ya ile ya kukosoa Serikali tu pamoja na kukaa wanaorodhesha matatizo yaliyopo pasipo wao kushiriki kwa vitendo zaidi katika kutatua matatizo hayo.
Vyama vtakavyoonekana kutetereka katika kutekeleza majukumu kama haya, basi vitafutiwe namna nyingine kwa sababu vitakuwa havistahili kuwepo kutokana na ukweli kwamba uwepo wake utakuwa hauna tija yoyote kwa Taifa na hibvyo kwa wananchi wote wa JMT kwa ujumla