Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”


Hicho ndicho kilichokuwa kinaendelea kwenye serikali ya Magufuli, hata wafanyabishara wengi hapa nchini walibambikiwa kodi, huku akijificha kwenye uzalendo fake.
 
Huu ni uthibitisho kwamba JPM alikuwa anaendesha nchi kwa ulaghai, utapeli, uzandiki, na propaganda. Alizungukwa na waongo na wanafiki, na yeye alipenda uongo na unafiki.
CCM wataendelea kung'ang'ania madaraka kwa sababu hiyo hiyo...taifa la Tanzania linaendeshwa kwa ulaghai, utapeli, uzandiki na propaganda. Huo ndio ukweli mchungu tunaotakiwa kuukiri kwa mapana yake.

Wakipisha tu wanajua watawajibishwa na hivyo wanahakikisha hawaondoki bila kwanza kuhakikisha wanawarithisha watoto na ndugu zao katika kujilinda. Ukweli una tabia ya kukataa kuzikwa, iko siku utainuka tu.
 
Walau tumepata kitu kikubwa, nakubaliana na Prof. Kabudi, though ana umaskini wa akili na mali, he has intellectual arrogance kubwa sana Prof . huyu.
Kumuita professor maskini wa akili ni kumvunjia heshima.
 
-Viongozi wetu,waliyumba,na hii inaleta sura mbaya kwa nchi yetu mbele ya makampuni/taasisi za kimataifa na wananchi wake.
-Viongozi ni vema wakawa wakweli na waadilifu kwa wanayoyasema au kufanya.
-Barick na makampuni mengine/taasisi zingine za kimataifa zinatuchukuliaje wa TZ?
-Je Barick wanaweza kuishitaki Serikali yetu / au kizazi chetu cha baadae, kwa dhamira ovu,ya kutaka kuitapeli kampuni yao, siku za usoni (baada ya kumaliza dhahabu yote)?
-Hakuna adhari za kisheria kwa kuweka masuala haya hadharani hivi sasa.

Ushauri
Viongozi wetu wawe waadilifu na waache kuchomekea fedha au maneno ya janjajanja.
 
Mkuu chiembe, umefunguka sana. Kunywa maji sasa upoe.

Pamoja na yote hayo nchi yetu imejaa wajinga, bado wanamkumbuka eti wanamuita Shujaa.

Alifanikiwa kupumbaza watu wengi kiasi kwa kuviteka vyombo vya habari. Wengi tulijua ni mlevi wa madaraka na mtu muongo. Ukishaona kiongozi hataki wakosoaji au uhuru wa vyombo vya habari, jua huyo kiongozi ni hatari.
 
Huyo atakuwa ni mfanyabiara mjinga. Cha juu ni lazima kiwe within the target ya bei yako. La siyo utafukuza wateja wako. Sasa hii ya Trillion 360 to Billion 700 itakuwa ni akili ya jalalani tu.
Hiyo ndiyo inaitwa "machinga mentality" iko Tanzania zaidi kama ile ya "mitumba mentality". Machinga wanakupangia bei kwa kutazama sura yako mnunuzi, pia wanafanya na wewe biashara kama vile hamtaonana tena. "Machinga mentality" kama ilivyo "mitumba mentality" inaendeshwa kwa mantiki ya "the lowest common denominator" kwenye jamii bila kujali inaathiri vipi ustawi wa maendeleo ya nchi ya muda mrefu ambao huwa unaendeshwa kwa mujibu wa "the highest common factor". Kama wasomi hawagundui tofauti hii na elimu yao pia inakuwa ya "Machinga and Mitumba Mentality" inataichukua Tanzania miaka si chini ya 30 kututoa hapa tulipo. Ndiyo maana mashujaa wetu sasa hivi ni watu waongo, wezi, wasanii, watu wa mipasho, waganga wa kienyeji na uozo kede kede uliopo. Itabidi aje Kiongozi kama malaika kuizindua Tanzania!!
 
Angekwepo JPM angethubutu kusema hivyo au angeendelea na msimamo wake?

Ndiyo maana wanasema Mwanasiasa hatakiwi kuaminika, hata kama wakisema muda huu ni Giza jitahidi utoke nje kuhakiki
 
Naona unabwabwa tu hapa kisa una chuki zako dhidi ya Lissu. Kama kinara wa majadiliano yale kwa upande wa Tz, Profesa Kabudi anakiri leo kwa kusema ile ripoti ilibeba uongo, uzushi na ulaghai, mimi na wewe ni nani tusikubali hayo?
Mbinu za majadiliano zinapaswa kubeba facts na sio hadithi za kutengeneza.
 
Angekwepo JPM angethubutu kusema hivyo au angeendelea na msimamo wake?

Ndiyo maana wanasema Mwanasiasa hatakiwi kuaminika, hata kama wakisema muda huu ni Giza jitahidi utoke nje kuhakiki
Asingethubutu kusema...
Angejaribu kusema angepotea au kutoweshwa tusijue alipo
 
Maana yake kuna kodi nyingi za wawekezaji na wafanyabiashara wanabambika tu
Mkuu suala la kodi kumbambika lilikuwa la kawaida sana..
Kuna jamaa alikuwa kwenye Task force ya Magufuli.. walikuwa kwanza wanacheki salio kwenye account..
Baada ya hapo unaandikiwa barua na kodi kubwa sana....

Hapo wanatengeneza mazingira ya kula cha juu.. Huyo jamaa kwa wiki alikuwa hakosi million 5 cash.. Kanunua viwanja vingi maeneo mbalimbali...
Sikuhizi namuona mara chache ila anaishi kwa mshahara tuu... Lile tangazo la March 2021 lilimmaliza kabisa na task force ilikufa
 
Asingethubutu kusema...
Angejaribu kusema angepotea au kutoweshwa tusijue alipo
Kwa kweli, manake yule mwingine alijaribu kusema sema akaishia kupata majeraha ya Risasi na isingekuwa Rehema za Mungu saivi tungekuwa tunaongea mengine
 
@Moderator tuasaidie hii post kuifanya pinned katika kila post itakayo mzungumzia Magufuli na awamu ya tano. Itawasaidia sana watu kuelewa wana jadili mtu au utawala wa aina gani

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kukiri kuwa hakuwa sahihi kuiita "JALALA" ORGANISATION TUKUKA SANA ALIYOITUMIKIA KWA MIAKA MINGI HADI AKASTAAFU, bado haoitoshi. Hekima ni kwamba anatakiwa sasa arudi tena kwenye organisation hiyo akawaombe msamaha viongozi wake waliopo kwa muda huu ikiwa ni pamoja na WAFANYAKAZI WOTE WA ORGANISATION HIYO

Kitu pekee nilichokishika mimi hadi leo kuhusiana na haya maswala ya mahusianao kati ya mtu na orrganisation ni mtu kukwepa sana kwa nguvu zake zote, ku-"CASTIGATE THE IMAGE OF AN ORGANISATION". Kitu hiki kiliwahi kusisitizwa sana darasani siku moja na mwalimu wangu wa Marketing Management Dr. LUCY MBOMA.
I REALLY HATE VERY MUCH THIS HABIT OF "CASTIGATING AN IMAGE OF AN ORGANISATION"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…