Profesa Kitila Mkumbo amepewa Uwaziri ili kukamilisha mpango wa bandari kwa DP World?

Profesa Kitila Mkumbo amepewa Uwaziri ili kukamilisha mpango wa bandari kwa DP World?

NAFIKIRI TUSIPOTOSHANE PASI NA SABABU.NIMEPITIA SPEECH YAKE AKIWA BUNGENI NAFIKIRI ALIONGEA VITU ZIZURI SANA VYA KUZINGATIA UNAPOINGIA MKATABA BAINA YA MTU ,TAASISI AU NCHI.YEYE NI MTANZANIA TENA MTANGANYIKA.LABDA AWE YUDA UISKARIOT.

TUMWACHE AFANYE KAZI

CCM ,2030 TULETEENI PROF HUYU KWENYE UCHAGUZI
 
"Chama cha Mapinduzi (CCM) kilibadili mwelekeo wa kisera za kiuchumi na kisiasa miaka ya 90's, mojawapo ya mabadiliko ya kisera za kiuchumi na kibiashara ni kuachana na Serikali kuhodhi nyenzo za uchumi kama ilivyokuwa hapo kabla"- Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Miaka ya 90's Chama cha Mapinduzi (CCM) ilitoa maana ya ubinafsishaji hauna maana ya serikali kukabidhi mali za umma kwa watu binafsi au watu.
Ubinafsishaji maana yake ni :-
1. Kuuza baadhi ya hisa za kampuni ya umma kwa wawekezaji binafsi
2. Kuingia ubia na makampuni au watu binafsi wa ndani au nje ya nchi
3. Kukodisha kampuni ya umma kwa watu binafsi au watu binafsi" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kamwe asingeweza kuruhusu kuingiza azimio humu bungeni ili kuuza bandari lakini wabunge wote hawa wasingeweza kupokea azimio la namna hiyo" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Baada ya taarifa za uwepo wa mkataba wa uendelezaji wa bandari wananchi wengi waliingia hofu, na sisi kama wabunge ni lazima tuzipokee hofu hizo, kuzielewa na kuzishughulikia hisia na hofu za wananchi wetu" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Azimio lililopo bungeni halihusu kuuza bandari, azimio linahusu uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari. Chama cha Mapinduzi (CCM) kisingeruhusu serikali yake kuingiza bungeni azimio la kuuza bandari" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Katika uwekezaji wowote kunakuwa na hofu, hata wakati wa kubinafsisha NBC kulikuwa na hofu na wapo walisema NBC imeuzwa. Mwaka 2005/2006 wakati nikiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tulimega eneo kwa ajili ya kujenga Mlima City, tuliambiwa chuo kikuu kimeuzwa lakini tulisimama imara sidhani kama kuna Mtanzania leo analalamika kuhusu Mlimani City" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Azimio lililopo bungeni linahusu kuanzisha mahusiano ya kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai, tukisharidhia ndio serikali inakwenda kufanya kazi yake ya kawaida ya kuingia mikataba. Hadi hapa tulipo hatuna mkataba kati ya TPA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania) na Kampuni ya DP World" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Kifungu cha kwanza cha mkataba kinaelezea maeneo ya uwekezaji, uwekezaji utafanyika kwa bandari ya Dar es Salaam lakini akifanya vizuri serikali inaweza kumualika aende kwenye maeneo mengine" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Wapo wanaosema mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) hauna namna ya kurekebisha, mkataba unarekebishika kwa kupitia ibara ya 22 ya mkataba huu" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Eneo la mifumo ya TEHAMA ni eneo nyeti na linahusu usalama wa nchi, nashauri na kuwaomba sana watu wa TCRA na serikali mtandao lazima wawepo na wasiachiwe wawekezaji peke yao." - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Nchi yetu ni miongoni mwa nchi ambazo zimebahatika kuwa na waasisi, msingi mkubwa ambao Marekani waliachiwa na wanaulinda ni uhuru wa watu wao. Sisi tuna waasisi wawili Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume na msingi waliotuachia ni umoja na ni lazima tuulinde msingi huu. Nchi yetu ni ya kidemokrasia hivyo tukitofautiana tutofautiane kisera lakini tusivunje misingi yetu ya umoja" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Mimi natoka wilaya ya Iramba person mkoani Singida lakini ni mbunge wa jimbo la Ubungo, hilo limewezekana kutokana na umoja wa nchi hii, kuna nchi wabunge wao ni wabunge wa makabila. Na natamani watoto na wajukuu wangu mimi wawe wabunge Pemba miaka ijayo na wa kutoka Pemba waende kugombea ubunge Bukoba" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

Niwaombe wanasiasa na sisi viongozi tuepuke kauli ambazo zinagusa misingi mama (ya umoja), tutofautiane kisera" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Watanzania hawapingi uwekezaji wa bandari wanataka mikataba iwe mizuri, wataalamu mzingatie hilo ili uwekezaji katika bandari uwe na tija" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo.
 
Lazima wataweka wazi ili kuondoa sintofahamu.

Huku mitaani hali ni mbaya sana kama kuna adui anataka tupigane alete tu shehena ya mabazooka.
Popo katika ubora wako.

Anyway, sikushangai, maana hata FISI ana JINSIA mbili, tena zote active.

Baba FISI baada ya miaka kadhaa, waeza mkuta keshatiwa ujauzito.
 
Tuliwahi kuandika hapa JF kuwa hakuna uteuzi au utenguaji unaofanyika kwa bahati mbaya au nzuri, kila uteuzi na utenguaji wa rais hapa Tanzania ni mpango kamili na mkakati mahususi wa muda mfupi, kati au umrefu.

Pia soma >

Kuna jambo fulani niliwahi kudokezwa siku nyingi kidogo kuhusu Profesa Kitila Mkumbo kwenye utawala wa mama nikabakia kushangaa na kusubiri kuona kama kweli litatokea ili niamini. Niliambiwa Kitila Mkumbo angeondolewa kwenye nafasi ya uwaziri (kama geresha ili kuwafumba macho watanzania) halafu baadaye atarejeshwa tena mambo yakiiva!

Unaweza usiamini sana, lakini fahamu tu, katika utawala wa mama, Professa Kitila Mkumbo ndio dalali muhimu wa mapatano katika deal la uuzwaji wa bandari za Tanganyika kwenda kwa waarabu wa Dubai. Muarabu wa Dubai anamuelewa vyema tangu mwanzo Profesa Kitila kwenye hili deal na kwa hali ilipofikia sasa (moto unaowaka chini kwa chini) kwa gharama zote Profesa Kitila imebidi apewe tena majukumu mahususi kumpooza muarabu mezani ili mambo yaende kama awali.

Ili kufanya mambo yaende sawa, kuondoa hatari ya siri kuvuja ovyo na kupunguza miruzi mingi, imebidi haraka sana suala la Mipango liondolewe kutoka wizara ya fedha na suala la uwekezaji (ambalo tayari mchakato wake ulishakamilika ili kulihamisha) liondolewe kutoka viwanda na biashara ili kuundwa kwa wizara mpya ya mipango na uwekezaji, kisha iwe chini ya ofisi ya rais na waziri apewe Profesa Kitila Mkumbo!

Kama tulivyozoea kumuona Profesa Kabudi akiwa mchenga wa deal za Magufuli kipindi kile cha issue za madini na siasa za kidiplomasia, tutegemee kumuona Profesa Kitila na deal za uuzwaji wa Bandari kwenda uarabuni.

Watu wengi wanadanganywa kuwa hili suala la uuzwaji wa bandari limeanza mwaka huu, kiufupi mikataba halisi ilishafanyika tangu mwaka jana, na deal lilianza kutengenezwa tangu mwaka juzi Profesa Kitila akiwa ni waziri husika.

Pia wapo watu wanadhani Profesa Kitila ni mpya kwenye hiyo nafasi, lakini kiuhalisia alishawahi kuwa waziri ofisi ya rais (uwekezaji)hapo kabla tena akiteuliwa na Magufuli. Mwisho kabisa wapo watu wanaodhania kuwa Profesa Kitila amepewa hiyo nafasi kwa kuwa amekuwa mtetezi muhimu wa serikali kuhusu sakata la bandari kuuzwa kwa muarabu, basi watu hao huenda wako sahihi kwa 100%. Siri ya mtungi aijuaye kata!

Kaa mkao wa kula, kuna mengi yatafuata!


Ila CCM wanatukosea sana sana, nenda pale Sabasaba uone uchafu na udini unaofanywa na yule Mama pale Sabasaba, Kila siku anasafiri na Rais Samia.
Taasisi inakufa, wameenda pale mawaziri na makatibu wakuu ila wameshindwa kumuomba aliyemteua amuondoe. She is Samia's best friend.

Yaani kama Samia anashauriwa na MTU kama yule basi KAZI IPO, wanakazi ya kununua Madera na shopping 🛍️ Kila akisafiri. Usitegemee lolote
Nilipomuona alivyochangia Bungeni Siku Ile ya kujadili Mkataba nilijua huyu Profesa anasaka Uwaziri. Hongera zake alizicheza Karata zake Vizuri. Alimponda Mbowe na CDM kuwa wanagawa Wananchi . Yeye katoka Iramba ni Mbunge Ubungo. Bado akawa anaalikwa kila pa kuondoa utata WA Mkataba. Raha kweli kuundiwa Wizara Mpya.
 
Nimeambiwa umepewa cheo Ili uwe fungate ya kukamilisha TANGANYIKA kuuzwa kwa waarabu

Umeunganishwa na rafiki yako kutoka kile chama cha upinzani ili upate uwaziri


Utafurahia kwa muda tu hayo mapesa ya kuhongwa
 
Nimeambiwa umepewa cheo Ili uwe fungate ya kukamilisha TANGANYIKA kuuzwa kwa waarabu

Umeunganishwa na rafiki yako kutoka kile chama cha upinzani ili upate uwaziri


Utafurahia kwa muda tu hayo mapesa ya kuhongwa
Fact check??
 
Back
Top Bottom