Profesa Lipumba ashangazwa na Rais Samia kumuachia mtu aliyekula njama katika wizi wa shilingi zaidi ya bilion 300 za Escrow kwa kutoa bilion 26 tu

Duh! Miongoni mwa vitu alivyokuwa akishtumiwa JPM hapa ni kuwafunga hao akina Seth, leo maza kamtoa Seth nje, watu hao hao wameanza kumgeuka maza kwa kitendo hicho cha kumtoa Seth.

Ngoja nimshauri mama labda atasikia: Mama hakuna chochote alichofanya JPM ambacho hakikupaswa kufanywa kwa mazingira ya nchi yetu ilivyokuwa. Na ukifikiri waliokuwa anti-Magufuli wanakusifia genuinely, hilo litakuwa kosa la kwanza tena kubwa kimkakati. Wanakusifia kama Chatu amvutiavyo mbwa, na mara tu uingiapo kumi na nane zao watakurarua bila huruma. Kama walifanya hivyo kwa miti mibichi, je kwako wewe mti mkavu itakuwaje? Stuka!

Sisi tupo tu hapa tunakucheck moves zako zote.
 
Wanaomlaumu Lipumba kupambana na Maalimu Seif ndani ya CUF hawamjui vizuri Maalim. Maalim ndiye alitemsaliti Jumbe, na Maalim ndiye aliyeuza ramani kwa kukubali kuingia ndani ya Serikali ya Hussein Mwinyi licha ya Mauaji na wizi wa kutisha wa kura ambao CCM waliufanya mwaka jana.

Lipumba aliamua kugangamala bdani ya CUF baada ya kukasirishwa na kitendo cha Maalimu kuamua kumuunga mkono Lowasa akishirikiana na Juma Duni hulu akimbypass yeye kama mwenyekiti wa chama. Hiyo ni dharau na Lipumba aliamua kukunjua makucha ili apewe heshima yake!.
 
Lipumba aende mahakamani
 
Cha kujiulza hizo 200 Bil zimerudishwa kweli ama ni changa la macho tu? Wadanganyika safari hii kazi mnayo.
 
Mama Samia ndio kamuachia huyo Habinder? nilidhani kaachiwa kwa vigezo vya Plea bargain? Halafu acheni roho za chuki na ukatili, kama mnaamini aliiba hela za uma serikali yenu iliyokua chini ya huyo mungu mtu wenu ilishindwa nini kudhibitisha na kumtia hatiani? Mngemhukumu na kumpa adhabu mnayoona anastahili na sio kumweka mtu mahabusu miaka minne eti uchunguzi unaendelea! mnachunguza nini miaka minne kama sio udhaifu, uzandiki, uonevu, chuki na roho za kishetani! kama mtu kaiba unahitaji miaka minne ya nini kuchunguza

Mambo mengine ya kipumbavu sana ndio maana mungu alisikia kilio chetu sisi tusiopenda chuki na ushetani

Mwacheni Mama achape kazi na mtulie kama wengine tulivyotulia wakati nchi ikiendeshwa kwa chuki na U#45$$!
 
Habinder kakiri kosa, kwa hiyo ni kweli aliktenda kosa
 
Mzigo ulitoka wewe
“Mzigo ulitoka”hilo unajua wewe

Sisi wananchi tumeambiwa hii ni cospiracy

Lipumba kasema hii ni conspiracy

Wanasheria (hujiita learned brothers) wamesema hii ni conspiracy

Ukishtakiwa kwa conspiracy ya mauaji ina maana hakufa mtu.

Angekufa ungeshtakiwa kwa mauaji, murder case!

Singa Singa alijipanga kupiga lakini hakufanikiwa, inaitwa conspiracy, kula njama.
 
Habinder kakiri kosa, kwa hiyo ni kweli aliktenda kosa
Hata ingekua mimi ningekiri kosa hata kama sina kosa... Haiwezekani mtu ukae mahabusu miaka minne eti uchunguzi unaendelea? unachunguza nini Miaka minne? na kwa nini umshike mtu wakati bado huna ushahidi? Huwezi kuniweka jela miaka minne bila hukumu wala kudhibitisha kosa langu, Kama kukiri kosa ndio njia pekee ya mimi kua huru nitakiri tu.. its that simple, na msijitoe akili na kushabikia tawala za kidhalimu zisizojali sheria wala haki za binadamu!
 
Sio wakati wote watu ni wabaya.ata hao uliowasema kwa jinsi mfumo wa nchi ulivyo ata wao wanaweza wasiwe na mchango mkubwa bila kwanza kufanya mapinduzi ya mfumo wetu wa utendaji kama nchi.Ata uko ccm sio viongoz wote ni wabaya lakini hawawezi kufikia matarajio makubwa kwa hali kama hiyo niliyoitaja.Sasa swala lakufanya mapinduzi yakimfumo sio swala la mtu moja mmoja mmoja.
 
Lipumba nae haeleweki mbele wapi nyuma wapi.

Leo kaongea hivi kesho ataongea lingine
 
Confidence wanayotaka wawekezaji wengi sio utawala wa sheria kama anavyobainisha profesa. Confidence wanayotaka ni uwepo wa hali ya kuwawezesha wao kuvunja sheria za nchi za uwekezaji bila kushikwa. Hali ya wao kuweza kuepa kodi hali ya wao kuweza kuhonga hali ya wao kuweza kufanya udanganyifu bila ugumu. Kwa hivyo wawekezaji waliyokuepo kwa magufuli hawajumlishi hao wababaishaji. Hao ndio wale nzi mzee mwinyi alisema ukifungua milango na madirisha wanaingia. Mmojawapo wa nzi ni huyo kalasinga aliyetia hasara mabilioni. Aliingia enzi ya jk. Sasa mama samia anamtoa kwa kulipa shs milioni 200 wakati kachota shs bilioni 350 Utawala wa mama utaona kalasinga na wababaishaji wa kila aina wakija kwa fujo kuwekeza.
 
Naona unatetea ufisadi wa ESCROW
 
Kwani Lipumba alikuwa wapi wakati hizo hela zilikuwa zinabishaniwa bungeni? CCM walisema ni hela za IPTL. Seth kanunua IPTL na kachukua hela zake. Aliibaje hela benki kuu? Alivunja benki na kuondoka nazo? Huu ni usanii tu wanatufanya watoto wadogo. Wampe wenyewe hela halafu warudi mlango wa nyuma na kutuambia Seth kaiba hela!!!!
 
Mnufaika wa pesa za wizi naye anahesabika kuwa ni sehemu ya wizi
 
Prof na wewe tunakudai bado usifikiri tumesahau zile mlikuwa mnakwapua mkishirikiana na ofisi ya msajili mnagawaniana pale magomeni NMB.
 
Mnufaika wa pesa za wizi naye anahesabika kuwa ni sehemu ya wizi
Mlimpa wenyewe. Mbona nyie mko huru? Ingependeza sana waliosema ni hela ya IPTL, waliotoa kibali cha kutoa hizo hela, na waliozitoa kumpa wote mgeunganishwa tungesema kweli kuna justice. Mumpe wenyewe halafu mseme kaiba?
 
Mlimpa wenyewe. Mbona nyie mko huru? Ingependeza sana waliosema ni hela ya IPTL, waliotoa kibali cha kutoa hizo hela, na waliozitoa kumpa wote mgeunganishwa tungesema kweli kuna justice. Mumpe wenyewe halafu mseme kaiba?
Alikamatwa yule ili awataje wenzie, Samia kamuachia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…