Profesa Mkenda aapa kutotoa vibali vya kuagiza sukari

Hivi hakuwa bungeni, mbona hakusimama kumuunga mkono mpina au hakupewa nafasi.
Wabunge wa Tanzanai huwa wanapitisha vitu bungeni na kuviunga mkono halafu wanatoka nje na kwenda kuvikandia.
 
Huyu si minister? Anaifahamu "doctrine of cabinet solidarity"?
 
Mnhuuhh..kuna muda unafiki UNAFIKI unauma nyinyi ..
WAcha tuoneee!??
 
Walipeleka majungu akaondolewa
 
Huyu si minister? Anaifahamu "doctrine of cabinet solidarity"?
Ukiwa mcha MUNGU huwezi kuwa na solidarity na wezi, mataeli na Wala rushwa.
Ni Bora ukose hiyo ministerial appointment lakini conscience yako iwe huru na kesho uingie mbinguni.
Bashe ameikosesha serikali Kodi zaidi ya nusu trilioni, halafu anaangalia tu.
Eti cabinet solidarity.
Wewe ule rushwa ya mabilioni halaffu niwe na solidarity na wewe?
 
kwahiyo bashe alipowekwa pale, akaamua kuvunja sheria.
 
Mmeanza kupata akili hata hiyo Sukari yenyewe haijawahi kuwa adimu wahuni wanatengeneza hilo swala haiwezekani Eswatin wachome sukari iliyozidi muda wa matumizi karibu tani za kutosha harafu eti Tanzania kila msimu ni adimu tuu..acheni uongo wenu hapo Uganda na Zambia sukari ni kama unga wa Sembe haujawahi kuwa adimu..
 
Mbona hii ni video ya Siku nyingi munawekaje hapa Kama evidence ya sakata la sukari la juzi. Lakini so Hawa Hawa tulikuwa tunawabeza kutokuwa na msimamo na walikuwa wananongwa kumridhisha bosi wao wa wakati huo? Sasa je hamuoni hata hizi kauli zaie zilikuwa Zina mridhisha bosi yule, na hasa ukicheki kwenye Lile sakata bosi anahusishwa na kupewa maekari ya ardhi na Hawa wazalishaji wa ndani. Nawapenda wazalishaji wa ndani, Ila kutumia video ya muda mrefu Kama ushahidi wa tukio la Leo ni upotoshaji wa makusudi, na vipi haliwezi kuwa kosa kisheria? Lakini wewe mpotoshaji huoni Kama unatupa wakati mgumu kukuamini na kuamini dhamira yako?
 
nadhani wameweka ili kuonyesha kwamba, serikali imeondoa watu wazuri kilimo, wakaweka wasiofaa kama huyo anayegombana na mpina.
 
Kilo moja ya sukari brazil bei ya leo wananunua shilingi 520 za kitanzania, hivo wahuni wanatupiga pesa ndefu sana
 
nadhani wameweka ili kuonyesha kwamba, serikali imeondoa watu wazuri kilimo, wakaweka wasiofaa kama huyo anayegombana na mpina.
Kwa kipimo kipi Cha uzuri wa mkenda, kwa kuua zao la mahindi kwa kuzuia wafanyabiashara wa nje kuja kununua? Kuua mounts kwa kuzuia wateja wasije kununua? Mkenda hakufanya lolote kwenye kilimo, Bora hata Bashe anajaribu, anaweza kuwa na mapungufu yake, lakini so kwa picha hii inayojaribu kujengwa kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…