Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Hahaha sawa wenye akili nyingi wa nchi hii, haya futeni huo mradi kisha leteni umeme wa gas na upepo na jua ili Tanzania ipae tuendane na kasi ya dunia.
Futeni tu miradi yote mana ni ya kifisadi tu mkuu.

Dooh masikini nchi yangu mimi, nisamehe sana Dambisa Muoyo kumbe ulikuwa sahihi.
Mataga unapitia kipindi cha mateso ssna
 
Huu upumbavu wa kumjadili mtoa hoja badala ya kujadili hoja ndiyo umetufikisha kwenye huu upumbavu unaolitafuna taifa. Hebu mpinge kwa hoja zake labda unaweza kuwa na mawazo bora zaidi, vinginevyo shut up.
Siwezi shut up kwa fara huyo! Alipokuwa waziri kilimshinda nini kumshauri Jakaya atengeneze vinu vya gas vya kufua umeme badala yake akabariki IPTL walipwe 150M kila siku!
 
Hata Ethiopia wanaojenga Bwawa kubwa la Umeme hapa Afrika nao wanapoteza muda??

Huko China na Ulaya bado wana Hydro Power Plant kubwa tu...nao vp wazijunje??

Acheni kuchotwa akili na WANASIASA MATUMBO

..ethiopia hawana gesi asili ndio maana wanatekeleza mradi wa umeme wa maji.

..cag anadai mradi wa stieglers hauna ripoti ya upembuzi yakinifu, pamoja na ripoti ya mazingira.

..kwa maneno mengine, tumewekeza matrillion ya fedha bila kuwa na taarifa za kutosha za faida vs hasara, pamoja na changamoto za mradi wa stieglers.
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi...
Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi...
Wanasema ukweli.

Umeambiwa na CAG upembuzi yakinifu ulifanywa miaka ya 70. Haukufanywa mpya kujiridhisha kwamba mradi una manufaa makubwa kiuchumi. Tatizo lenu munawaza kizamani!

Zingatia hoja ya mtu. Siyo kupinga tu.
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi...
China wasingejenga three gorges , mambo ya inga dam pia yangesitishwa.
Na ulaya kwa kuwa hawana source za hydro power wanatumia umeme wa Nyukilia
 
#BUNGENI: Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ameishauri Serikali kuachana na miradi ya uzalishaji wa umeme wa maji kwani unachelewa kuleta faida, "Hydro kukupatia faida uwe umewekeza hela nyingi na unahitaji miaka upate faida ndio umeme wa maji uwe bei ya chini.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma.

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

“Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

#sparklight_tv #sparklight_tvupdates
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.

NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki

Hawa si ndio walikuwa wanasifia "STEGOLAZI"?
 
Kwa ufahamu wangu, umeme wa maji ndio rahisi zaidi baada ya umeme wa nuclear. Angetoa takwimu bei ya unit moja ya umeme wa gesu inayozalishwa Tanzania kama kule Kinyerezi ni sh ngapi na ule wa maji kama kidatu/ hale ni shilingi ngapi.

Anadai eti itachukua miaka mingi kurudisha gharama, je hiyo gesi ya kusini imeisharudisha gharama? Tunapata faida? Au wawekezaji na mabenki yaliyotukopesha ndio wanafaidika? Miaka mingi ni mingapi kwa nini haitaj na kulinganisha na hiyo gesi anayodai ni michache,

Haya mashambulizi dhidi ya JPM inaonyesha yako coodinated, ukifuatilia kuanzia kule twita hadi kwa hawa jamaa. Inaonyesha yuko mtu anachezesha huu mchezo.
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.

NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki

Kukauka kwa mabwawa? Hata gesi mbona ina mwisho wake! Huyu ni Prof fake kabisa!
 
maprofesss
Umeme wa maji ndiyo nishaji yenye gharama nafuu duniani. Ukisikia mtu anajiita profesa anauponda cha kutilia shaka ni vyeti vyake tu.

Kwa hesabu ndogo tu Megawati 2,100 ni sawa na kilowati 2,100,000 Unit za umeme ni kilowati moja ikitembea kwa saa moja.

Sasa ukiwa na kilowatt milioni mbili na laki moja zikatembeza mitambo kwa masaa 24 unapata unit za umeme milioni 50.4. Ukiuza umeme huu kwa wateja angalau kwa unit moja shilingi 100

Mtambo unaweza kutoa mapato ya bilioni 5 kwa siku. Ukitoa mwezi mmoja kwa mwaka kwa ajili ya "maintenance" ukatembea miezi 11 unaweza kupata trilioni 1.7 kwa mwaka Tumeujenga kwa shilingi trilioni 7. Almost 5 years mradi kama utakuwa full operational unarudisha gharama.

Kama taifa lazima tujue wataalamu wetu ndiyo wamekuwa wakitupotosha na tatizo ni elimu yetu ndiyo mbovu.

Ukichukua mtu aliyesoma miaka ya 70, nchi haina wataalamu huku kwenye elimu ya chini, wanasema nyumba ni msingi hivyo ukikosa basic education huko juu mtu anaenda tu. So unaweza kuta mtu ni profesa but anafanya maamuzi au ushauri wa ajabu.

Labda tujenge mradi but mashine tusifunge megawati zote 2100 kwa kuwa kwa sasa hatuna soko la kutosha.

Kadiri tunavyoongeza ndivyo tutakavyoongeza kufunga mashine.

Umeme wa maji unategemea jiografia hivyo wengi hawatumii kwa kuwa jiografia haziwaruhusu.

Chukua mfano mdogo tu wa gari, Gharama ya kuendesha gari kwa kunua mafuta ndiyo gharama ya juu kuliko gharama ya kununua gari lenyewe.

Mmfano umenunua gari la milioni 12 kama ukiweka mafuta ya 20,000 kwa siku ndani ya mwaka utaweka mafuta ya 7,300,000 (milioni saba na laki tatu)

Ukikaa nalo miaka 10 utatumia mafuta ya milioni 73.

Lakini sasa anakuja mtu ana gari anauza milioni 16 lakini unaedesha kwa kutumia maji.

Ndani ya miaka 10 la mafuta kununua na mafuta ya uendeshaji ni milioni 85 wakati la maji ni milioni 16.73

Hivi ndivyo umeme wa maji ulivyo nafuu kulinganisha na umeme wa mafuta au diezeli.

Mashine zinazungushwa na maji hahuhitaji kununua nishati ya kuendesha.
Baba watanzania huwa tunadanganywa kulingana na wakati,hili la umeme wa gesi halijaanza leo lakini limetufikisha wapi, ulinganisho wa bei za umeme unaotokana na maji na gesi,MUHONGO watanzaniawa sasa sio kama wale wa kale huwezi kutudanganya tena,kumbe ndio maana mlikuwa mnajifukiza bungeni ili tusijue mnaongea nini! ndio maana yake hii sio kwa sasa tuko na wewe sambamba komea hapohapo, umeme wa kisasaaa bullshit.
Hydroelectric power is 0.85 cents per kilowatt-hour
In the U.S., hydropower is produced for an average of 0.85 cents per kilowatt-hour (kwh). This is about 50% the cost of nuclear, 40% the cost of fossil fuel, and 25% the cost of using natural gas.
 
Wazo lake ni Zuri sana,kutegemea umeme wa maji ni kujihatarisha hasa myakati za ukame mkubwa,tumesahau kuna kipindi tulitamani mvua za mabomu?
 
Back
Top Bottom