FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Kwani mke wa tatu kweli? Wa kwanza na wa pili wako wapi?Hata akiwa mke wa nne....what's wrong with that?
Utake usitake yeye ndie raisi wa JMT mwenye jinsia ya kike.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani mke wa tatu kweli? Wa kwanza na wa pili wako wapi?Hata akiwa mke wa nne....what's wrong with that?
Utake usitake yeye ndie raisi wa JMT mwenye jinsia ya kike.
Ila alichosema ni ukweli..karne hii kuanza kuangaika na umeme wa maji ni kupoteza muda tu
wadau wameshaanza tathmini ya namna ya kupiga pesa za SGR, kama tiyari zilikuwa zishakusanywa kwaajili...Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi
Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.
Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.
Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma
Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.
Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.
"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.
Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.
NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi
Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka
CCM acheni unafiki
Umeme wa maji ndiyo nishaji yenye gharama nafuu duniani. Ukisikia mtu anajiita profesa anauponda cha kutilia shaka ni vyeti vyake tu.
Kwa hesabu ndogo tu Megawati 2,100 ni sawa na kilowati 2,100,000 Unit za umeme ni kilowati moja ikitembea kwa saa moja.
Sasa ukiwa na kilowatt milioni mbili na laki moja zikatembeza mitambo kwa masaa 24 unapata unit za umeme milioni 50.4. Ukiuza umeme huu kwa wateja angalau kwa unit moja shilingi 100
Mtambo unaweza kutoa mapato ya bilioni 5 kwa siku. Ukitoa mwezi mmoja kwa mwaka kwa ajili ya "maintenance" ukatembea miezi 11 unaweza kupata trilioni 1.7 kwa mwaka Tumeujenga kwa shilingi trilioni 7. Almost 5 years mradi kama utakuwa full operational unarudisha gharama.
Kama taifa lazima tujue wataalamu wetu ndiyo wamekuwa wakitupotosha na tatizo ni elimu yetu ndiyo mbovu.
Ukichukua mtu aliyesoma miaka ya 70, nchi haina wataalamu huku kwenye elimu ya chini, wanasema nyumba ni msingi hivyo ukikosa basic education huko juu mtu anaenda tu. So unaweza kuta mtu ni profesa but anafanya maamuzi au ushauri wa ajabu.
Labda tujenge mradi but mashine tusifunge megawati zote 2100 kwa kuwa kwa sasa hatuna soko la kutosha.
Kadiri tunavyoongeza ndivyo tutakavyoongeza kufunga mashine.
Umeme wa maji unategemea jiografia hivyo wengi hawatumii kwa kuwa jiografia haziwaruhusu.
Chukua mfano mdogo tu wa gari, Gharama ya kuendesha gari kwa kunua mafuta ndiyo gharama ya juu kuliko gharama ya kununua gari lenyewe.
Mmfano umenunua gari la milioni 12 kama ukiweka mafuta ya 20,000 kwa siku ndani ya mwaka utaweka mafuta ya 7,300,000 (milioni saba na laki tatu)
Ukikaa nalo miaka 10 utatumia mafuta ya milioni 73.
Lakini sasa anakuja mtu ana gari anauza milioni 16 lakini unaedesha kwa kutumia maji.
Ndani ya miaka 10 la mafuta kununua na mafuta ya uendeshaji ni milioni 85 wakati la maji ni milioni 16.73
Hivi ndivyo umeme wa maji ulivyo nafuu kulinganisha na umeme wa mafuta au diezeli.
Mashine zinazungushwa na maji hahuhitaji kununua nishati ya kuendesha.
Professor msomi? Kwa hiyo mtu akiwa professor anakuwa na akili kushinda watu woteHuyu ni Professor Msomi ana hakika na anachokisema. Enzi hizo hakuweza au aliweza akatupwa kwenye Recycle Bin.
Dooh nimecheka saana haya watu wanafufuka mmoja moja wanaaanza upya kuchomoa makucha yao.
Hawana tena cha kuhofia mana enzi za shamba la bibi zinarudi kila mtu anaanzisha ubunifu mpya wa kupiga pesa.
Huyu ni Muhongo bado namsubiri Ngereja naye atakuja na lipi.
Na muda si mwingi tutasikia Accacia nayo imefufuliwa upya na kupewa mgodi huko geita kwasababu nchi inahitaji zaidi wawekezaji kuliko wao wanavyo tuhitaji.
role model wetu Kama taifa kawhata Ethiopia??? Unataka tuige mifano kwa waliofeli kama sisi???Hata Ethiopia wanaojenga Bwawa kubwa la Umeme hapa Afrika nao wanapoteza muda??
Huko China na Ulaya bado wana Hydro Power Plant kubwa tu...nao vp wazijunje??
Acheni kuchotwa akili na WANASIASA MATUMBO
Wakati anasema imepitwa na wakati China leo wameanza kujaza maji kwenye the second largest Hydropower Dam !
Niliwahi kusema siku Magufuli anatoka madarakani, hasa iwapo huo mradi wa SG utakuwa haujakamilika utatekelezwa. Yale ambayo yalikuwa dhahiri kwangu yameanza kutokea.
Je ni kwanini niliwaza hayo? Kimsingi nilijua nchi hii haina sera wala mipango, bali kuna maslahi ya rais aliye madarakani na genge lake. Wakati vwa JK tuliimbishwa umeme wa Gas kama wendawazimu, na yakapigwa mashahiri yote. Tuliambiwa umeme wa gas ukikamilika tutakuwa na 5,000mg+. Cha ajabu wakati tukiimbishwa hayo mapambaio, Magufuli alikuwa waziri tena akawa anaunga mkono mradi ule. Alipoingia madarakani akaona hana maslahi binafsi na umeme wa gas. Akaona afanye mradi wa umeme kwa maji tuliokuwa tunaambiwa matatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Hii yote ni ili apate maslahi binafsi yeye na genge lake. Ndio hapo unasikia sijui taarifa ya upembuzi ni ya 1970 nk.
Sasa tuje kwenye ukweli, hivi unawezaje kuanzisha mradi mpya wa umeme ili kupata 2,115mg kwa 6.5t, unaacha umeme wa gas ambapo ungeweza kupata 5,000mg? Je angeweka 3t kwenye gas asingepata hizo 2,115mg, na 3.5t akiziweka kwenye viwanda?
Uyo sio tu professor mbali nimshauri mwandamizi ngazi ya dunia yaani top ten ya mabingwa Kwenye maswala ya NISHATI kwaio anachokiogea anaijua vizurProfesa afanye utafiti zaidi kuhakiki ufahamu wake, umeme wa maji ni moja ya njia zinazopigiwa debe sasa duniani ikiwa ni katika sera za kutunza mazingira na kutupunguza emission of cabonidioxide gas kutokana kutumia fossils fuels ikiwemo natural gas..
Umeme wa gas inachangia kwa kiasi kikubwa katika janga la global warming.
Hii ni miradi inaitwa WHITE ELEPHANTS. Unaweza ukaimaliza lakini isikupe Desired Return on Investment.
Kwa mfano SGR hata ikimalizika kwenda huko Rusumo sijui ambako tuna target mzigo wa Rwanda, bado haina faida kwa vile throughout ya Rwanda ni less than 800k metric tons per annum.
Mzigo wa ndani ni very insignificant kwa vile Magufuli hakuwa na vision. Anajenga reli huku anaua sekta binafsi. Amefirisi akina Yusuf Manji, amewatisha kina Mo Dewji kwa kuwateka, amesababisha vifo vya akina Mufuruki na Shamte kwa chuki zake, Je anategemea local traders gani wasafirishe mzigo kwenye SGR?
Hiyo Stiglers Gorge ni upotevu wa Matrilioni ya hela tu kwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi ndiyo adui mkubwa wa hydro electricity. Kamwe hawezi kupata hizo megawatt 2100 kama alivyotamba kwenye maradio na matv.
Ameshia kuharibu baioanuai ya selous tu na kuteremsha hadhi ya pori tengefu
KAtika yote aliyozungumza hili tu la umeme wa gesi ndo umeona ni jambo muhimu? Nilivyosikiliza sikusikia unachozndika hapa. Hiyo aliigusia tu! Naona kila muwekezaji ana msemaji nchini sasa! Hadi huku kwenye blogs. Tumewachoka na uzembe wenu!Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi