Profesa Ndalichako: Wanafunzi waliopata mimba kuendelea na masomo kwa njia mbadala

Profesa Ndalichako: Wanafunzi waliopata mimba kuendelea na masomo kwa njia mbadala

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Wizara ya Elimu imesema kuwa inaandaa utaratibu wa kuruhusu wanafunzi waliobeba mimba wakiwa masomoni kuendelea na masomo kwani ni haki yao ya msingi.Haki hiyo ya msingi inatajwa kuzuiwa kipindi cha uongozi wa awamu ya tano.


Profesa Joyce Ndalichako amesema haya...

Kwenye upande wa watoto wa kike, serikali iko makini kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu na ndio maana kupitia fedha za mkopo wa Benki ya Dunia) tumetenga fungu kwa lengo la kumuendeleza mtoto wa kike.

Tumeweka utaratibu kwa watoto waliopata ujauzito kuendelea na masomo yao kupitia njia ya elimu mbadala, kama ameacha akiwa kidato cha kwanza anaweza kusoma kupitia njia ya elimu mbadala na akifaulu mtihani wa kidato cha pili aturudi katika mfumo wa kawaida

Kama mtoto wa kike aliacha shule akiwa kidato cha tatu, kisha akifanya mtihani wake na kufaulu mtihani wa kidato cha nne, atapata fursa sawa na kupangiwa shule sawa na yule aliyekuwa shuleni kulingana na ufaulu wale waliokuwa shuleni


ndalichako.jpg

My take: Sasa sio ushu kumbebesha mimba mwanafunzi maana atasoma tu.

USSR
 
Jamani haya maswala ya wanafunzi kurudi kusoma upo tangu siku nyingi.Na endapo akiingia kiongozi akaacha kufuata huo waraka ni kawaida tu. Madhara yake mashirika ya kimataifa hayawezi kusaidia miradi ya maendeleo ya nchi hadi uruhusu hiyo sekula. Kwa hiyo waziri hawezi kuzuia sekula labda rais .Na akizuia kuna kuwa na madhara ya kiuchumi
 
Kama ni haki yake ya msingi ni vyema pia wangetizama haki za mtoto. Ni vyema mtoto akapata malezi ya baba na mama na pia kiliniki ni vyema mama mjamzito akaongozana na mzazi mwenzie kwa ajili ya ushauri hivyo itakuwa sio vyema mwanaume apelekwe jela miaka 30 huku mama akiteseka na ujauzito na baadae ateseke na mtoto hii inaweza kumuathiri kisaikolojia mama na mtoto kwa kukosa matunzo ya baba. Embu fikiria ni uchungu kiasi gani mama atakaoupata kusikia mpenzi wake amefungwa jela miaka 30. Wanasaikolojia mtisaidie hapa
 
Kwanini serikali isihakikishe wanaolewa kwa kugharimia harusi zao hukohuko shuleni?
Hiyo ni ngumu kidogo. Tuseme serikali inaratibu na kugharamia ndoa za hawa wasichana wahanga. Si itaonekana wagharamie pie ndoa za wavulana, ili kutenda haki? But seriously, siyo haki kusitisha masomo kwa msichana kisa amepata ujauzito. Huo ni unyanyasaji uliopitiliza. Mindset aina hii ni za kibaguzi, kiume na kibinafsi
 
Hiyo ni ngumu kidogo. Tuseme serikali inaratibu na kugharamia ndoa za hawa wasichana wahanga. Si itaonekana wagharamie pie ndoa za wavulana, ili kutenda haki? But seriously, siyo haki kusitisha masomo kwa msichana kisa amepata ujauzito. Huo ni unyanyasaji uliopitiliza. Mindset aina hii ni za kibaguzi, kiume na kibinafsi
Nisaidie: sheria inazuia kumpa mimba au kufanya ngono na mwanafunzi? Mwenye uwezo wa kuzuia mimba ni mwanamke, inakuwaje wanakubali kupata mimba? Wabakaji wahukumiwe, hawa wasichana vihele hele wanao wakonyeza wanaume wapewe lift na hela za chips wachukuliwe ni wabakaji.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
MATAGA utawasikia "Oyeeeeee serikali ndio hii, Mabinti zetu lazima wasome" hii ni 2021

Lakini somewhere 2016-2017 " Oyeeee huyu ndio raisi, hatuwezi kusomesha Malaya, watawafunza watoto wetu umalaya, Hapa tumepata Raisi'

Shenzi kabisa
Hakika mataga, akili zipo nyayoni.
 
Wataendelea na masomo wakiwa na mimba au baada ya kujifungua? Kama ni baada ya kujifungua, maelekezo ya wizara ya afya ya mtoto kunyonyeshwa kwa miaka miwili yamefutwa? Haki ya mtoto kuzuiwa kunyonya ili mzazi arudi shule ina angaliwaje? Wanafunzi wa kike kupimwa mimba mashuleni mwongozo umefutwa? Waliofungwa kwa kuwapa wanafunzi mimba wanatolewa Magerezani? Asante kwa kunisikiliza.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Soma vizuri maelezo ya Waziri.

Hawa watoto wahanga wa mimba za utotoni, wanaandaliwa utaratibu wa kuwawezesha kurudi masomoni baada ya kuzaa. Mpaka tuone huo utaratibu, ndiyo tunaweza kujua faida na hasara zake.

Kilicho muhimu, ni kuwa baada ua hao watoto kupatwa na janga la mimba, wanapata elimu.
 
Back
Top Bottom