Nimeelewa vizuri sana dhihaka, na mie nikaongeza dhihaka, na baadaye nikasema "seriously". Naelewa vizuri hoja ya maadili na zinaa. Nikwambie kitu, tunatakiwa kuzama zaidi ili kupata SULUHU mujarab. Shida hapa ni zinaa, na hasa zinaa ya kizembe.
Sasa, mimba ni matokeo ya zinaa. Zinaa inahitaji wawili. Tunatakiwa kuadhibu wafanya zinaa, lakini sio kuvuruga maisha yao, na kwa hakika, hatutakiwi kuwanyima haki ya msingi. Hata muuaji aliyehukumiwa kifo, bado ana haki za msingi. Elimu ni haki ya msingi. Kumwadhibu msichana eti kwa kuwa ndio amekutwa na mimba, ni uvivu wa kufikiri. Mimba yenyewe tu ni adhabu tosha.