Profesa Ndalichako: Wanafunzi waliopata mimba kuendelea na masomo kwa njia mbadala

ndio maana huwa nasema,wanaharakati wengi hawana nia njema na jamii wanayodai kuisemea.wengi wana ajenda zao,either baada ya kununuliwa,au wanatafuta umaarufu kupitia jamii.

mtu anakwambia fimbo ni malezi ya kijiama kwa mtoto,anazungumza hivyo huku anajua kuna watoto wanakulia mbagala na mwananyamala kwa kopa,bila mzazi kuwa serious ni msiba kwa mtoto.

hili la mimba pia kuna watu wanataka waingize wengine mkenge kizembe tu,tunaandaa kizazi kipi ambacho mtoto hapitii usichana wake!!!
kizazi kipi ambacho mtoto anakua anamwona mama yake anamnyonyesha baada ya kuvua uniform??tunaandaa taifa la hovyo sana hapo baadae.
 
Watoto wa kike kuendelea na masomo baada ya mimba kwa upande wangu ni sawa kwa sababu wanaowapa mimba after all wao wanaendelea na kazi na masomo pia maana mara nyingi unakuta hawafahamiki na anayefahamika ni yule tu anayepata ujauzito. Ukiamua kwamba idadi hii ya (pengine unayosema asilimia 1) kuendelea kutopata elimu kwa sababu kuwa wamepata mimba baada ya miaka fulani utakuta kwamba idadi kubwa ya wanawake watakuwa wamekosa elimu siyo tu ya msingi, bali pia ya sekondari na chuoni. Sioni ni kwa nini wanaopata mimba wasiendelee na masomo kwa sababu hakuna madhara yoyote, ila tu ni faida kwamba watapata elimu.
 

tuna vyuo vya fani mbali mbali na hata vya ufundi stadi kwa ajiri ya watu kama hawa,si kweli kwamba wanafukubwa 100% na kunyimwa haki yao ya kupata elimu milele.

wanaotoa mimba hawafahamiki sababu wanakimbia au kujificha kifungo,isingekuwa hivi labda tungekuwa tumetenda haki kwa utashi wa kila mmoja wao.ndio maana sisi kama wakaka wa makamo tunasubiri tamko rasmi la kisheria ili tuanze kutetea haki za wawekaji mimba pia,na haki za watoto kupata malezi ya pande mbili.

hiki tunachopigia harakati ni ni sawa na kuamini tunawapa watoto kuku kila siku tukiamini tunawapenda sana,kumbe watashindamwa kuishi kwa mchicha ikikosekana.
 
Mimi siongelei kwa sababu ya uanaharakati, ila kwa sababu sijapata sababu ya msingi kwa nini wasiendelee na mfumo wa elimu kama wengine wanavyofanya. Na kama wanaweza kwenda kwenye hivyo vyuo vingine, kwa nini wasiendelee na mfumo wa elimu ulivyo? Tatizo ni nini?
 
Reactions: SMU
Jambo jema. Watoto ni wetu na wajibu wa kuwapa elimu ni wetu. Taifa kuwapa elimu bora watoto/wananchi wake ni jambo lenye maslahi kwa taifa.

Usipowapa elimu (kwa kuwa wana mimba/wamezaa), hakumkomoi huyo mtoto aliyepata mimba, bali taifa na mtoto atakayezaliwa. Elimu na maarifa ni faida kwa taifa.

Kuna nyakati mpaka najisikia aibu. Yaani mpaka WB watuwekee sharti la kusomesha watoto wetu wenyewe ndio tuone umuhimu wake? Suala la kuwapa elimu na maarifa watoto wetu halipaswi kuwa mjadala kwa watu wanaofikiri vema! Faida zipo so obvious. HAKUNA hasara yoyote katika kuwapa elimu watoto WETU....bila kujali status zao.
 
Tuanze kuchukua hatua kama wanaume na tubailishe attitude zetu.

Wanaume tujiangalie. Ukijijua wewe ni mwanaume achana na kutongoza vitoto chini ya miaka 18. Ikiwezekana chini ya 20 usiwaguse. Wabaki watoto kwa watoto na hao tushirikiane kama jamii kwa ujumla kuwaelemisha. Sasa unakuta mtu mzima anatamani watoto na anashindwa kujizuia na uwezo wa kuwashawishi anao (wanamuogopa, wanamheshimu, anawapa lifti, pesa nk..), tatizo linakuwa gumu kumaliza kwa hali hii. Naona ni mwanaume wa ajabu ajabu ndiye anaekula vitoto under 18. Tukijirekesha itasaidia sana

Wasichana wakipta mimba waruhusiwe kuendelea na masomo watakapokuwa tayari maan bado ni sehemu yenye mchango kubwa kwa jamii ila pia tushirikiane wote kupunguza au kutokomeza mimba kwa watoto kwa kuanza kwa kutokuwatia.
 
Hatujawahi kutumia akili vizuri;
. Mtoto wa kike anabakwa anapata mimba
Na shule anafukuzwa...tunamkomoa nani?
Kwanini asipewe nafasi kujutia makosa asome ajikwamue?

Hii ni sheria kandamizi iondolewearaka

Hivi hawa mabint wanaopata mimba huwa wanabakwa[emoji22][emoji38][emoji849]..
Ushakuta mzazi anahangaika na bint atulie aachane na ngono ila hasikii kabisaa mzazi anapiga kelele za kila aina ila hasikiii mara kapata mimba inakua kabakwaa duuh!!![emoji38][emoji38]
 
Mkuu watu wanaohangaisha wanafunzi wa kike ni sisi wanaume, na sisi wanaume ndio tunataka wasirudi shule, tujitafakari
 
Mkuu watu wanaohangaisha wanafunzi wa kike ni sisi wanaume, na sisi wanaume ndio tunataka wasirudi shule, tujitafakari

Bint mwenyewe ndio muhangaikaji!! Sisi mbona tumesoma kulikua hamna wanaume wakutuangaisha?! Ukiamua kuanagika na wanaume ni weww mwenyewe bint binafsi yako na utashi wako hata sisi tulikua tunatongozwa haikua lazima kukubali..
ukiona mwanaume anakusumbua si useme kwa wazazi wako!?
 
Unazungumzia watoto wa like kurudi should baada ya kujifungua he wavurana mbona munawaacha nyuma?Kama ni kuathirika kielimu hata yule aliyempa mimba Kama ni mwanafunzi mwenzie ni Bora wote wawe na haki sawa tusiangalie upande mmoja.
 
Ndio maana elimu ya Tanzania inashuka Kila mwaka,sababu ni kubadili maitaala na Sheria kandamizi ili tu wapate njia ya kupata hizo fedha kutoka kwa mabeberu.
 
Kama ni swala la mkopo wa banki ya dunia kuwa usipomrudisha mtoto wa like shuleni hamtapewa huo mkopo?ili tukubaliane ni hata mtoto wa kiume anayohaki ya kumlea mama na mtoto pindi atakapokuwa fikisha mtoto miaka miwili Basi wote wazazi Hawa warudi shuleni,hii ni haki kwa wote kwani mazingira waliopitia ni magumu mpaka wakapeana mimba.
 
Kwa upande wa aliyempa mimba inakuaje?
Serikali inacheza muziki wa wafadhili wakilazimishwa kufuata tune wasizozijua, matokeo ni kuruka tula kama maharage kwenye sufuria. Msichana anapata mimba anawekewa utaratibu wa kuendelea na masomo, kwa vile ni haki yake. Mvulana mwanafunzi aliempa mimba anafungwa miaka 30. Yeye hana haki ya elimu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…