Profesa Safari: Halima na wenzie wanapaswa kukamatwa kwa kuidharau Mahakama

Profesa Safari: Halima na wenzie wanapaswa kukamatwa kwa kuidharau Mahakama

Tuwekee hapa hicho kifungu cha sheria. Otherwise piga kimya
Sasa ficha ujinga wako wewe watu watakucheka umesikia kesi imesharudishwa mahakamani inaendelea upyaaa hawatoki bungeni endeleeni na kazi zingine itafika 2025 muanze kulalamika mmeibiwa kura kumbe hamjajitbulisha kwa watu hawawajui hamjulikani
 
Sasa ficha ujinga wako fala wewe watu watakucheka umeaikia kesi imesharudishwa mahakamani inaendelea upyaaa hawatoki bungeni endeleeni na kazi zingine itafika 2025 muanze kulalamika mmeibiwa kura kumbe hamjajitbulisha kwa watu hawawajui hamjulikani
Nani kakwambia ukirudisha kesi mahakamani utaratibu mwingine hauendelei?

How stupid can someone be? Vichaa kama wewe mnatujazia server tu.
 
Hv chadema wanapata hasara kiasi gani hawa wabunge wakiwepo bungeni.?
Swala sio CDM kupata hasara wala Covid19 kuendelea kuwa bungeni bali ni umuhimu wa kuheshimu Katiba ya nchi na Utawala bora period. Wakitoka na serikali ikaendelea kuwalipa mishahara na marupurupu sawa hiyo ni kazi ya CAG kuhoji na serikali kujibu!
 
Hv chadema wanapata hasara kiasi gani hawa wabunge wakiwepo bungeni.?
Unajua lolote kuhusu katiba?
Unajua lolote kuhusu sheria?
Unajua lolote kuhusu mgawanyo wa madaraka?
Unajua lolote kuhusu kuheshimu utaratibu?
Una elimu gani, ulisoma wapi, ulimaliza mwaka gani?
 
By James Magai
More by this Author

Dar es Salaam. Siku moja baada ya maombi ya Halima Mdee na wenzake 18 kufungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema kutupwa na Mahakama Kuu, wamerejea tena mahakamani kupigania uanachama na ubunge wao.

Awali, Mdee na wenzake walifungua maombi Mahakama Kuu Masjala Kuu dhidi ya Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wakiomba ridhaa ya mahakama kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wao.

Hata hivyo maombi hayo yalitupiliwa mbali Jumatano Juni 22, 2022 na Jaji John Mgetta kutokana na kasoro za kisheria, baada ya kukubaliana na hoja mbili kati ya sita za pingamizi zilzioibuliwa na Chadema kupitia jopo la mawakili wake lililoongozwa na wakili Peter Kibatala.

Lakini, Alhamisi Juni 23, 2022 walirudi mahakamani hapo na kufungua upya maombi hayo chini ya hati ya dharura baada ya kurekebisha kasoro zilizoainishwa na mahakama.

Mawakili wao, Aliko Mwamanenge, Ipilinga Panya na Edson Kilatu wameieleza Mwananchi Digital leo Ijumaa Juni 24,2022 kuwa shauri hilo jipya la ridhaa ya kufungua shauri la maombi ya mapitio ya mahakama (kupinga uamuzi wa Chasema kuwavua uanachama, limesajiliwa kama shauri namba 27 la mwaka 2022.

Wasema kuwa sambamba na shauri hilo la msingi (maombi ya ridhaa) pia wamefungua shauri la maombi wakiomba amri ya mahakama kudumisha hali ilivyo kwa sasa (kulinda hadhi ya ubunge wa wateja wao), ambalo limepewa usajili wa namba 16 la mwaka 2022.

ADVERTISEMENT

Mawakili hao wamelieleza Mwananchi Digital kuwa wamefanikiwa kufungua tena shauri hilo mapema kiasi hicho kwa kuwa walikuwa wamejiandaa na kuwaandaaa wateja wao kwa uamuzi wowote wa mahakama.

“Tulikuwa tumejiandaa kwa uamuzi wowote na tulikuwa tumewaandaa wateja wetu kwamba lolote linaweza kutokea hivyo wanapaswa kuwa mahali pamoja ili mahakama vyovyote ambavyo mahakama ingeamuru tuweze kufanya marekebisho," amesema wakili Panya.

Amefafanua kwamba baada ya kutoka mahakamani tu kusikiliza uamuzi walirejea ofisini wakafanya marekebisho ya kasoro zilizoainishwa na mahakama na kwamba baada ya saa tatu walikuwa wamekamilisha kisha akasafiri usiku huo kuwafuata wateja wake kwa ajili ya kusaini nyaraka hizo.

“Baada ya wateja wetu kusaini, jana asubuhi tuka-file (wakawasilisha nyaraka mahakamani) na mpaka saa moja tulikuwa tumaliza ku-upload (kupakia nyaraka) maana siku hizi tuna-file online (kufungua kupitia mtandao)," amesema Panya na kuongeza,

“Mahakama baada ya kuzifanya nyaraka zetu assessment tulikwenda tukalipia kisha tukapewa namba. Kwa hiyo mpaka saa mbili tulikuwa tumeshapata na namna na tukawajulisha wateja wetu wamwandikie Spika kumjulisha kuwa tayari wameshafungua tena shauri na namba ni hiyo.”

Wakili Mwamanenge amesema licha ya kukamilisha mapema kufungua shauri hilo hawakutaka kuweka wazi wakisubiri kwanza wapate hati ya wito kwa wajibu maombi ambayo ndio itaonesha tarehe ya kutajwa na hata Jaji atakayelisikiliza.

Amesema kuwa mpaka jioni bado walikuwa hawajapata hati hiyo ya wito na kwamba wanaendelea kuisubiri kwa ajili ya kuwapelekea Chadema.

Kina Mdee wamekwama aisee!

Wakili Kilatu amesema ingawa walikuwa wanasoma taarifa nyingi na zisizo sahihi kwenye mitandao kuhusu uamuzi na hatima ya wateja wao lakini waliamua kutulia tu kwa kuwa walikuwa wanajua wanachokifanya
 
Roho mbaya tu! Kwa hiyo akina Halima wakitoka bungeni hawatapeleka wengine?

Shida mnaongea bila kufanya utafiti. Kwa Sasa CHADEMA haitaki jina lake kuhusishw na uchaguzi wa 2020. Sio ubunge Wala udiwani. Chama kina mpango wa kumuita Kenani na madiwani wote kuwaomba wajiuzulu.

Leo akina Halima wakijiita wabunge wa CCM chadema haitahangaika nao.
 
Hv chadema wanapata hasara kiasi gani hawa wabunge wakiwepo bungeni.?

Wanatumia jina lao wakati wao hawataki. Wakitumia la CCM hakuna mwenye muda nao. Mnadharau maamuzi ya chama na bado mnataka kuwa wanachama?. Unataka kuwa mwanachama kwa chama usichokiheshimu.
 

Ccm Nibebe Nibee Nibembeleze, Mikononi Mwako Niwe Salama

 
Ezekiel Mbaga, hayo yamesemwa na mtu anaitwa Prof. Safari. Sasa wewe unaihusishaje CHADEMA na maoni ya mtu?

Au unaugua ugonjwa uitwao chademaphobia na sasa umepanda hadi kwenye Bongo yako na kukuletea confusion...?
 
Hv chadema wanapata hasara kiasi gani hawa wabunge wakiwepo bungeni.?
Wapo bungeni kwa mgongo wa CHADEMA; ni ajabu kwamba wewe hilo hulijui, kwa hiyo hata ukielezwa "hasara" wanayoipata CHADEMA itakuwa ni kazi bure, kwa sababu huna uwezo wa kuelewa.
 
Jina lako linaakisi mawazo yako. Prof. Safari anazungumzia mtu ambaye analeka kesi kuwa aendelee kuwa alipo na mahakama inasema asiwepo lakini anaendelea kuwepo.

Kuna sehemu yoyote Prof. Safari kataja Chadema. Ungekuwa una hata robo ya uwezo ungejua Chadema ndio iliwafanya wawe Bungeni, labda walipelekwa na mtu mwingine - lakini Chadema ilipotaka watoke wakapeleka kesi mahakamani wakisema wako pale kwa niaba ya Chadema (wakipinga kufukuzwa uanachama!)

Pathetic!
Hivi hawa covid 19 na wa vyeti fake utofauti wao ni nn? Wote si wanakula posho za nchi bila uhalali? Mbona wa vyeti feki walivyotumbuliwa wanasiasa uchwara mliona ni udikteta ila hawa fake 19 kuachwa mnaona ni kutokuheshimu katiba. 😂😂
 
Kama siyo chadema wanapotoa hoja na wanapoingia bungeni wanawakilisha nani? Ha hawana majimbo ila majimbo yao wote ni ya Chato na Kongwa kupitia chama wanachokijua wao. Kama ni Chadema wasingekubali kuapishwa nje ya Bunge. Kuapishwa nje ya bunge ni batili. Pili kama walikana ushindi wa CCM kwenye majimbo yao? sasa wanamwakilisha nani?
Chato na kongwa hazipo tena bungeni. Sa hivi ni pemba na mbeya, si iwatimue km hawana uhalali!! Au mizimu ya chato bado inawasumbua??
 
Awamu ya tano ndio iliwatengeneza kwa wingi matakataka wa aina hiyo. Taifa lina kazi pevu kuyasafisha.
Naiombea hii nchi ipate tena rais km wa awamu ya 5. Au tutawaliwe na Putin tu maana watanzania wengi ni vichwa maji. 😎😎
 
Yaani hapo hamna wakili mnamoiga dili tu kibatala Hana chochote kumbuka kesi ya gaidi mbowe alivyokuwa hajui Sheria Kila pingamizi anakoweka anakwama hivi nyie chadema mpaka muambiweje ndiyo muamini kibatala ndiyo angemsababishi mbowe kufungwa maisha kama siyo zitto na she mkuu kumuombea kwa mama amuachie?
Kwa hiyo umehalalisha kuwa mama aliingilia mhimili wa mahakama? Ndo demokrasia hiyo mnayoisifu? Tuwe serious kesi ilikuwa ya mchongo hapo hakuna wa kushukuriwa bali ni uongo ulijitenga kutoka kwenye ukweli na msafi akawa huru.
 
Back
Top Bottom