Profesa Shivji ashangazwa na uteuzi wa wafanyabiashara kwenye uongozi wa TANESCO

Uongozi wa nchi umeshapoteza 'legitimacy' kwa umma ni wazi bin dhahiri TANESCO tayrai imeshabinafsishwa kwa mlangoi wa nyuma. Hakuna mwananchi wa kawaida atakayeweza tena kupata huduma ya umeme kwa bei nafuu na kimsingi chama tawala kimekiuka mktaba na wananchi kupitia 'Ilani' ya uchaguzi 2020-2025.

Ni bayana kwa sasa migogoro ilikuwa inajitokeza kawa kutaka kukwamisha miradi na kuhujumu ulikuwa unafadhiliwa na uongozi uliojiweka kwa sasa na wananchi wataumia sana na hakuna mwanasiasa wa upinzani atajitokeza kuwasemea wananchi maana walikuwa pamoja kuhakikisha JPM hayupo na lengo walikamilisha hivyo hawana haja ya kupigania kero na shida zinazowakabili wananchi zaidi ya kuwaneemesha wafanyabiashara.

*Njia panda changua njia pana yenye kila kitu njiani dhid ya njia nyembamba yenye uhaba wa vitu vya anasa za kupita
 
Msomi wa kiwango cha kimataifa wa Tanzania, Profesa Shivji ameshangazwa na kitendo cha wafanya biashara kuchaguliwa kuongoza taasisi za umma.
Shivji anasema sekta ya umma haiwezi kuchangamana na sekta binafsi.
Sisi wengine tumeshangazwa na uteuzi wa wafanya biashara na watu wenye maslahi binafsi kwenye bodi ya TANESCO. Yule mama Balozi ndie mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Rex Attorneys ambao wanaiwakilisha Dowans na Symbion kwenye kesi ambazo TANESCO inashitakiwa na hayo makampuni halafu anateuliwa kua board member.
Unaweza kusoma mwenyewe hapa.
C& P
JE NI HAKI MTU AMBAYE KAMPUNI YAKE INAISHITAKI TANESCO KUWA MJUMBE WA BOADI YA TANESCO,? WAANDISHI WA HABARI WASIWE VIPOFU,, WAFUKUE UKWELI
 
Sawa nimekuelewa lakini si kwa kuirejea afrika kusini. Niirejee nchi ambayo fisadi Zuma anafungwa miezi 15?!!! Utofauti uko wapi na kutofungwa?
Angalao huko anaguswa hata kwa kuhojiwa, hapa kwetu utaweza! Thubutuu!
 
We unamchagua mpiga deal kama mwezi wa kwanza kuongoza wizara unategemea nini kama sio kupigwa
 
Akili umekosa ndio nachoweza kusema
 
Siku utasikia azam hawalipi bill za umeme ndio hapo tutapojua kuwa sisi ni washamba wa waarabu
 
Na katiba mpya unayoongelea wewe ni ipi?

Ya Kikwete(Bunge la katiba) au ya Warioba(katiba pendekezwa ya Warioba)?

Embu tuanzie hapo kwanza kuboresha mada.

Maana twaweza sema tunataka katiba mpya tukaishia kulishwa matapishi.
 
Mbona ilishawahi kutokea hapohapo Tanesco? Kuna Bosi mmoja make wake ndiye aliyekuwa anapewa Tender mbalimbali hapo kwenye Shirika. Na ilifanyiwa kazi. Hii inaitwa "Conflict of interest". Ni kosa kubwa. Ni sawa na Uhujumu uchumi.
 
Mbona ilishawahi kutokea hapohapo Tanesco? Kuna Bosi mmoja make wake ndiye aliyekuwa anapewa Tender mbalimbali hapo kwenye Shirika. Na ilifanyiwa kazi. Hii inaitwa "Conflict of interest". Ni kosa kubwa. Ni sawa na Uhujumu uchumi.
I mean "Mke wake"
 
Huyu bibi huwa hata hausiki kwenye teuzi, yeye kazi yake ni kusaini tu, nadhani ingekuwa vyema angejiuzulu kabisa maana hakuna kitu cha maana anafanya
Ewe mfuasi wa jiwe hebu tulia dawa ikuingie
 
Wewe pia hapa na ujinga wako! Balozi ana law firm ambayo inatetea kampuni zinazoishitaki Tanesco, huyo mama huoni kuwa katika Bodi ya tanesco si sahihi? Je, vetting imefanyika Sawa? Au kwa vile walimwajiri Ridiwani Kikwete wakati huo
Umemjibu vyema huyo oya oya
 

Kwanza tuweke wazi huyu mzee ni professor wa History si uchumi au biashara. Bodi anaweza akawekwa mtu yeyote mpaka pale tu ambako kuna maslahi binafsi.
 
Mkuu kwani hujui Trump ana kesi ya kukwepa kulipa kodi,alitumia cheo cha uraisi kukwepa kulipa kodi kibao na aliposhtukiwa akayaka ang'ang'anie madarakani ili apate kinga ya kutopelekwa mahakamani. Unapoteua mtu kama mtoto wa Bakhresa kwenye bodi ya Tanesco maana yake makampuni yake yaanzae kupata upendeleo maalumu,pia unapomteua aliyekuwa wakili wa kampuni za kitapeli zilizoinyonya Tanesco maana yake nini huyu February ni mpigaji wa juu kwa juu, sasa tunaona team ya wapigaji wakirudi kwa nguvu,Shivji yupo sahihi.
 
... nchi inaongozwa na sera za CCM tuzingatie hilo.
Kubwa na la msingi, Ilani ya chama.
Kazi iendeleee...
Tumeipenda wenyewe! Imeisha hiyo

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…