Mkuu labda unisaidie, hivi bodi inaweza amua mambo tu kiholela bila hata waziri au Rais/vyombo vya usalama kushauri otherwise prior to maamuzi? Mbona wakiboronga huwa wanatimuliwa? Maadam wanafanya kazi ndani ya sheria na kanuni basi wakizivunja watatimuliwa tu.
2. Ni kheri uchukue wafanya biashara wanaojua soko linahitaji nini na market patterns ni zipi kuliko profesa wa UDSM ambaye anajua theories tu lakini hana practical experience ya kuendesha taasisi pana kama TANESCO!!
3. Kingine Tanzania na dunia nzima inaendeshwa kwa ubepari ama market economy lakini ni ngumu sana kuchora mstari kati ya private sector na public sector.
Mfano tunajua kuna mawaziri ambao wana biashara na hisa kwenye sekta binafsi je Mwigulu au Jenista wawe disqualified kuwa viongozi serikalini kisa wana biashara binafsi? Au double standards ni pale mfanya biashara mkubwa tu anapokua kwenye bodi ya TANESCO ila akiwa mwanasiasa ni halali ???
VERDICT: Mimi siungi mkono mafisadi kuwepo kwenye bodi ila naunga mkono 100% kujaza watu wa private sector kwenye taasisi za umma ili waweze kuongeza ufanisi. Imagine TTCL inavyoendeshwa!! leo hii wakihamisha management nzima ya Vodacom/Tigo kwenda TTCL unadhani ufanisi hautongezeka?
kikubwa ni sheria za kudhibiti bodi, manunuzi, tenda, matumizi n.k ziangaliwe na zisimamiwe 100% trust me kutakua hakuna madhara hata Seth akipewa TANESCO!!