Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Najiuliza sana!

Inawezekanaje Profesa Shivji awe mwanasheria na azijue sheria kumzidi mbobezi wetu wa sheria ndugu Zembwela?!

Kwamba mnataka niamini Shivji ni nguli wa sheria kumzidi Maulid Kitenge!

Eti Profesa Shivji ana mzidi kudadavua sheria za mikataba mwana sheria mbobezi wa sheria za mikataba ndugu Msigwa?!

Acheni kuniaminisha ujinga atiii!

NB: Mod, andiko langu ni swali tafadhari msiuunganishe ili niweze kupata majibu.
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

View attachment 2671928

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
Mbona huelezi mara mbili Profesa Shivja kasema anaongea laakini "hana ushahidi"?

Unafahamu maana yake nini kisheria?
 
Kweli nimeamini huwezi mwelewesha shekh utamu wa nyama choma na bia. Hii serikali haielewi kuwa sisi watanzania ni maskini na sifa ya maskini ni kufatilia mali za urithi. Sasa nyie mnataka kuuza bandari alafu pesa mgawane nyie na vizazi vyenu vyote hapa duniani hata mkifa mna hamu ya kuwa reincarneted kwenye familia zenu ili muendelee kuwa matajiri ndiyo mana akifa mtu anazaliwa mtu kwenye familia zenu?
Kwamba kuwe na amani huku taifa linaibiwa? Non sense.
 
Mbona huelezi mara mbili Profesa Shivja kasema anaongea laakini "hana ushahidi"?

Unafahamu maana yake nini kisheria?
Unawaza nini? Unataka kusema hajausoma huo mkataba.
 
Shivji haoni ndani kwa Professor Zembwela na Dr. Kitenge hawa ni wabobevu kwenye sheria za mikataba ya kimataifa.
20230620_081758.jpg
 
Najiuliza sana!

Inawezekanaje Profesa Shivji awe mwanasheria na azijue sheria kumzidi mbobezi wetu wa sheria ndugu Zembwela?!

Kwamba mnataka niamini Shivji ni nguli wa sheria kumzidi Maulid Kitenge!

Eti Profesa Shivji ana mzidi kudadavua sheria za mikataba mwana sheria mbobezi wa sheria za mikataba ndugu Msigwa?!

Acheni kuniaminisha ujinga atiii!

NB: Mod, andiko langu ni swali tafadhari msiuunganishe ili niweze kupata majibu.
Ma expert wa evaluation za mikataba zembwela na mwenzake hao ni manguli!!
 
Taifa limebarikiwa kwa kuwa na Rais mwanademokrasia haswa[emoji123][emoji2956][emoji2956]

Ingewezekanaje kwa Jaji Mugasha kuikosoa "presidential decree" iliyo chini ya Rais asiyeheshimu sauti za wakosoaji ?!!!

Majaji wanajua kuwa taifa linaendeshwa vyema kidemokrasia na uhuru wa kutoa mawazo.....

Jaji Mugasha analijua hilo fika[emoji120]

#SiempreJMT[emoji120]

#AbarikiweChifuHangayaAmen[emoji120]
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

View attachment 2671928

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
Shivji hajaona kifungu cha 5:4?

Wazi kabisa kinasema miezi 12 au ile miezi 12 mkataba uliiweka pale ya nini?

Nyinyi hata mki spin vipi, mkataba ni mwema sana kuliko mikataba yote tuliongia nchi hii.
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

View attachment 2671928

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
Watawala hawawezi kukuelewa mzee.., raia tunashukuru sana tunapata elimu mpya kila kukicha. Japo waelimishaji mnaitwa wapotoshaji mara wachochezi.
 
Najiuliza sana!

Inawezekanaje Profesa Shivji awe mwanasheria na azijue sheria kumzidi mbobezi wetu wa sheria ndugu Zembwela?!

Kwamba mnataka niamini Shivji ni nguli wa sheria kumzidi Maulid Kitenge!

Eti Profesa Shivji ana mzidi kudadavua sheria za mikataba mwana sheria mbobezi wa sheria za mikataba ndugu Msigwa?!

Acheni kuniaminisha ujinga atiii!

NB: Mod, andiko langu ni swali tafadhari msiuunganishe ili niweze kupata majibu.
Umemsahau Kitenge na Hando wanasheria wabobevu wa mambo ya mikataba.
 
Unawaza nini? Unataka kusema hajausoma huo mkataba.
Nimeuliza swali, kwanini arudie hayo mara mbili?

Na kasema wazi siuongelei mkataba wote ntaongelea vifungu kumi tu.

Maana yake ni simple, kauli yake haina mashiko ya kujadiliwa kisheria. Au haelewi mkataba wa kibishara.

Unajuwa kwenye sheria, huwezi kuandika au kusema chochote cha maana kama hujapitia vifungu vya sheria.

Hapo kaulizwa kama msomi lakini yeye karuka "kimanga" kuwa asichukuliwe "serious" hana ushahidi.
 
Back
Top Bottom