Profesa Tibaijuka: Mikataba yote tunayoambiwa ni ya Siri ni mibovu. Ashangaa kwanini wananchi wapo kimya

Profesa Tibaijuka: Mikataba yote tunayoambiwa ni ya Siri ni mibovu. Ashangaa kwanini wananchi wapo kimya

Mwisho wa mchezo huo utakuwa mbaya sana.
Siku hizi hawa watawala wetu wanatuona sisi watawaliwa kuwa ni takataka tu.
Hebu chukulia mfano wa swala la DP World na Bandari lilivyo fanyika,; likapelekwa Bungeni kujadiliwa na akina Msukuma...!

Baada ya zile kelele nyingi, wananchi wakaambiwa huko baadae kelele zenu hatutaki kuzisikia. Tukaarifiwa kuwa sasa wameziba masikio, wamekuwa 'Vyura Viziwi'; wasisumbuliwe na makelele yenu, ya wananchi!
Ni kiongozi wa wapi uliyesikia akijitangazia waziwazi kuwadharau wananchi wake kiasi hicho hapa duniani na asiwajibishwe?

Nchi hii tunayo matatizo makubwa.

Ninakubaliana nawe, hatupo mbali sana na huo "mwisho mbaya".
 
Muhimu ni kile alichoongea
Lakini hiyo mikataba ya Siri haijaanza kwenye hii awamu ya Sita ya Mama bali hata mikataba ya madini na Gesi nani alishirikishwa au nani aliiona ?

Tungeshirikishwa na Mkapa na Kikwete tungekubali madini yetu ya dhahabu yachimbwe kwa Serikali kupewa asilimia 3 ????!!

Hiyo siri alikuja kuitoa JPM !
 
Tatizo la professor 👩‍🏫 ni kusema kweli akiwa nje ya meza kuu lakini akikaribishwa mezani huwa anaibadili mitazamo yake haraka sana kama vile sio yeye !!
Hebu nieleze huko huko CCM ni wangapi umesikia wakisema kama yeye, iwe wapo ndani au nje ya serikali. Kwa hiyo, kwa yeye kusema, hilo pekee lina mtofautisha na hao wengine wote; au wewe hata hiyo tofauti huioni, hata kama ni ndogo?
 
Huyu Mama naye...!, mkataba ni wa siri, wanasheria wenyewe wanaojua sheria wako kimya, unategemea nini kwa mwananchi wa kawaida?.
Hebu atuache...!.
Tuko hapa ukumbini tunamsubiri Mama tusemezane.
P
Sawa Paskali. Mnatengeneza mikataba na ndani mnaweka kipengere mnakiita "non-disclosure clause" ambacho kinazuia pande hizo mbili kwenye mikataba zisitoe au kuonesha mikataba hiyo kwa mtu wa tatu ambaye hausiki na mkataba huo. Hivyo basi mnaacha iwe ni siri yenu wawili tu. Yaani ninyi ndugu zetu wasomi mnatuangusha sana kwa hilo.
 
Tatizo la professor 👩‍🏫 ni kusema kweli akiwa nje ya meza kuu lakini akikaribishwa mezani huwa anaibadili mitazamo yake haraka sana kama vile sio yeye !!
Huyu Mama wa tuela twa mboga hapaswi kuilaumu mikataba hiyo ya siri. Hutwo tuela twa mboga alitwotupata toka kwa ndugu yake mmoja ni matunda ya siri sirini katika mikataba mibovu tuliyokwisha ingia with our eyes wide open
 
Tatizo la viongozi wetu wanapokuwa nje ya mfumo wanakuwa na hoja nzuri sana....mambo ya aina hii yanawachochea "Gen-Z
 
Mama anatumegea ili sisi kama sisi tujadili nini cha kufanya na ikiwa kwa wakati wake alishindwa kufanya chochote haimaanishi basi wote tuwe kama wao kuna cha kujadili na kuchukua hatua kwa wakati wetu kuna mambo katika ujana wako ulishindwa kuyafanya watakuja vijana watafanya mimi sioni kosa kwake na ndio maana watz hatubadiliki tumekuwa rigid.
Tiketi za ubaya ubwela zimeisha. Jezi elfu 42 Hilo tunafuatilia kweli. Lakini mambo ya msingi Kwa faida ya watoto wetu na wajukuu wetu tukiulizwa tuna majibu mepesi et tutafanyaje Sasa! Aliyeturoga kafa angekuwapo tungemlazisha atutoe kwenye chupa!
 
Exactly !
Ndio maana ukianza kuhoji maamuzi ya wakubwa unaonekana ni Adui msaliti
Huyo mkubwa kawekwa na nani awe mkubwa?. Hawajitambui na hatujitambui tunasahau kwamba tunapanga foleni kuwaajiri. Wanatakiwa watuite sisi wakubwa. Nyumba wanazoishi tumejenga sisi, ofisi wanazopigwa na viyoyozi ni nguvu zetu. Magari wanayotembelea kodi zetu. Mishahara pesa zetu. Tunachowatuma hawafanyi. Tujitambue tusiwe na WOGA kuwahoji na wamekuwa na kasumba ukiwahoji maswali ya kuwaingiza matatani wanasema OCD nenda naye huyo. Mungu TUSAIDIE tuamke tujitambue.
 
Tujibu hoja aliyoweka mezani kwanza
Si ametuamsha kwamba mikataba mingi ni mibovu? Kwa hiyo ukianza kuhoji sijui Symbion, Meremeta, Escro sijui DPW, dawa yao ni TUWAONDOE na Mikataba tuione yote kwani hii ni nchi yao? Siri zibaki ni za ulinzi wa nchi tu yaani jeshi. Tutakuja ambiwa Watanzanaia wote hamieni Congo nchi imeuzwa kama wamasai walivyoambiwa hamieni Msomera oohoooo!
 
Hebu nieleze huko huko CCM ni wangapi umesikia wakisema kama yeye, iwe wapo ndani au nje ya serikali. Kwa hiyo, kwa yeye kusema, hilo pekee lina mtofautisha na hao wengine wote; au wewe hata hiyo tofauti huioni, hata kama ni ndogo?
Hiyo ni point 🙏👍
Tatizo lake huwa anabadilika haraka sana akisogea mezani 🙌🤦🏽‍♂️
 
Si ametuamsha kwamba mikataba mingi ni mibovu? Kwa hiyo ukianza kuhoji sijui Symbion, Meremeta, Escro sijui DPW, dawa yao ni TUWAONDOE na Mikataba tuione yote kwani hii ni nchi yao? Siri zibaki ni za ulinzi wa nchi tu yaani jeshi. Tutakuja ambiwa Watanzanaia wote hamieni Congo nchi imeuzwa kama wamasai walivyoambiwa hamieni Msomera oohoooo!
Tulishaambiwa tuhamie Burundi 🇧🇮 😳
 
Huyo mkubwa kawekwa na nani awe mkubwa?. Hawajitambui na hatujitambui tunasahau kwamba tunapanga foleni kuwaajiri. Wanatakiwa watuite sisi wakubwa. Nyumba wanazoishi tumejenga sisi, ofisi wanazopigwa na viyoyozi ni nguvu zetu. Magari wanayotembelea kodi zetu. Mishahara pesa zetu. Tunachowatuma hawafanyi. Tujitambue tusiwe na WOGA kuwahoji na wamekuwa na kasumba ukiwahoji maswali ya kuwaingiza matatani wanasema OCD nenda naye huyo. Mungu TUSAIDIE tuamke tujitambue.
Ni kweli kabisa hii kasumba ya kuwaita wakubwa hata kama ni kwa kuwazodoa lakini huwa inatutia unyonge fulani hivi ya kutufanya tujione kama vile sisi tunafadhiliwa na wao !🙌👍
 
Huyu Mama wa tuela twa mboga hapaswi kuilaumu mikataba hiyo ya siri. Hutwo tuela twa mboga alitwotupata toka kwa ndugu yake mmoja ni matunda ya siri sirini katika mikataba mibovu tuliyokwisha ingia with our eyes wide open
Wamesha tuona sisi ni watu wa kudanganywa danganywa kama watoto wadogo!
Leo anasema hivi kesho atasema tofauti akidhani tutakuwa tumesahau alichokisema jana !
Call spade a spade ALWAYS !
Sio leo ni Spade lakini kesho ni kijiko kikubwa !
Mtu asiye na msimamo hafai kuongoza jamii !
 
Sawa Paskali. Mnatengeneza mikataba na ndani mnaweka kipengere mnakiita "non-disclosure clause" ambacho kinazuia pande hizo mbili kwenye mikataba zisitoe au kuonesha mikataba hiyo kwa mtu wa tatu ambaye hausiki na mkataba huo. Hivyo basi mnaacha iwe ni siri yenu wawili tu. Yaani ninyi ndugu zetu wasomi mnatuangusha sana kwa hilo.
Mkuu Kuta, KUTATABHETAKULE , kwanza ni kweli kabisa mikataba mingi ina kipengele hicho cha non disclosure kwa ajili ya kulinda siri za biashara, lakini kwa mikataba kuhusu rasilimali za taifa, haipaswi kuwa siri kwasababu inahusu public property, wenye nchi ni wananchi na sio serikali, hivyo wenye mali has the right kujua kuhusu hatma ya mali zao, ndio maana tukaamua mikataba yote ya rasilimali za taifa lazima ipitishwe bungeni bunge liridhie, na ndicho kilichofanyika kwenye ile IGA ya DPW na Bandari zetu.

Nikaomba HGA pia iwe public isiwe siri, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! nikatoa ombi hili Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA halikusikilizwa!, ile HGA ni siri, ila ile IGA ya kimaghumashi iliwekwa pembeni for illegality!.
P
 
Back
Top Bottom