Propaganda? Hao wasomi waliojaa pomoni wapo wapi? Mbona mimi siwaoni!!!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Amani iwe nanyi wakuu!

Kutokana na maoni ya watu na maneno ya mtandaoni na Bungeni kuwa wasomi wamejaa mtaani, basi Taikon niliamua kufanya kauchunguzi kadogo tangu mwaka jana mwezi wa nne kama huu. Nimeita kauchunguzi kadogo kujiepusha na masuala ya takwimu. Uchunguzi wangu na wala usiitwe utafiti ulilenga kupima ukweli wa kile kisemwacho kuhusu wingi wa wasomi mtaani, kutokana na neno ''kujaa" linalotumiwa na watu kusema wasomi wamejaa mtaani wakimaanisha ni wengi.

Bahati nzuri mimi ni mtu wa kujichanga na makundi yote ya watu, vijiweni, mitandaoni, kanisani, mikutanoni, kwenye matamasha, Night Club n.k Hivyo kwangu ni rahisi kufanya uchunguzi wangu kwa urahisi.

Baada ya kufanya uchunguzi wangu nikabaki najiuliza, hao wasomi wanaosemekana wamejaa pomoni mitaani wapo nchi ipi, au ni wasomi hewa. Au wasomi wa Kusadikika katika nchi ya kufikirika?

Nilipokuwa kwenye vijiwe kadhaa katika mikoa ya Morogoro, Dar es salaam, Iringa(Mafinga), Mbeya(uyole), Kilimanjaro(moshi mjini) Dodoma(nane nane) nilichochea mada za kujadili wasomi. Nikashangaa kuona vijana wa karibu vijiwe vyote wakisema kwa matambo yenye uhakika kuwa wasomi siku hizi ni wengi mpaka wanakosa ajira. Vijana wengi na hapa ni zaidi ya 80% walikiri kuwa wasomi kwa sasa wamejaa mabarabarani wakizurura kama machinga.
Hapo nikabidi nifanye kautafiti kadogo katika vijiwe hivyo, nikauliza swali, kwani hapa wangapi wana shahada moja, nikashangaa wote wakiwa kimya. Nikauliza wangapi wana walau stashahada, pia kukawa kimya kwa vijiwe vingi ingawaje vipo vijiwe kwenye baadhi ya mikoa walijitokeza wenye shahada na diploma japo walikuwa wachache. Yaani kwenye kundi la watu kumi basi mmoja angekuwa na diploma au degree.
Hapo nikawauliza ikiwa mnasema wasomi wamejaa na ninyi mpo zaidi ya kumi lakini wenye diploma na degree hakuna au wakiwepo hazidi mmoja. Huko kujaa mnakosemea ni kupi?

Haya nikauliza, kwenye familia yenu mliozaliwa, yaani wewe na ndugu zako. Wangapi wanaelimu ya shahada? wengi wa walijibu hakuna kwao mwenye shahada moja. Hata hao wenye diploma bado walikuwa wachache sana.

Hata hapa JF unaweza ukajiuliza, kwenu wasomi ni wangapi? Au rafiki zako kwao wasomi ni wangapi wenye elimu kuanzia ngazi ya diploma mpaka shahada?
Hapo utapata picha kuwa hao wasomi waliojaa pomoni ni propaganda tuu.

Wasomi wamejaa pomoni wakati shule hazina waalimu?
Wasomi wamejaa pomoni wakati Mahospitali hayana matabibu, wauguzi na wafanyakazi wa kutosha?
Wasomi wamejaa pomoni wakati huko mahakamani kuna mlundikano wa kesi kutokana na uhaba wa majaji, na mahakimu na mahakama?
Wasomi wamejaa pomoni wakati Huko mashambani maafisa kilimo wapo wachache?
Wasomi wamejaa pomoni wakati Maafisa maendeleo wapo wachache?
Wasomi wamejaa pomoni wakati huduma za kibenki bado ni haba hapa nchini? na wanaozitumia ni wachache kutokana na kipato na elimu duni?
Wasomi wamejaa pomoni wakati huko Bungeni tuu kuna wabunge wanachangia vitu vya hovyo?

Ni wasomi gani hao?

Wasomi wamejaa pomoni wakati watu hata kusoma na kuandika hawajui, hata hapa Jf kuna watu wanachanganya L na R?
Wasomi wamejaa pomoni wakati watu wana mazao lakini kuna uhaba wa maafisa masoko?
Wasomi wamejaa pomoni wakati miji ipo shaghala baghala kwa ukosefu wa mipango miji?
Wasomi wamejaa pomoni wakati raia hata hawajui haki zao za msingi? Hao ni wasomi maandazi

Wasomi wamejaa pomoni wakati vyombo vya habari wamejaa makanjanja ambao habari zao niza kitoto, na habari za watu wenye akili ndogo
Wasomi wamejaa pomoni wakati watunga sheria baadhi yao wanatunga visheria vya kipuuzi kubana haki za raia na watu hawahoji kitu.

Wasomi wamejaa pomoni ipi katika mita ya wapi ndugu zangu?
Wasomi wamejaa pomoni ilhali watu wengi ndani ya jamii hupenda udaku na udakuzi kuliko masuala ya maana

Labda wasomi wa kuunga unga, lakini kama ni wasomi OG mtaani kwa kweli ni wachache sana.

Nafahamu hii ni propaganda iliyotungwa kwa mpango maalumu wa kukimbia wajibu na majukumu ndani ya jamii

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
 
Uchunguzi wako unawezekana uko sahihi sana,hao wasomi huenda hawapendi kukaa kwenye vijiwe wakihofia kuchekwa na wasio soma kwamba mbona mpo vijiweni wakati mna kisomo;?Hebu jaribu kuangalia kwenye matangazo ya kazi ofisi mbalimbali nafasi imetangazwa moja.Waombaji elfu kumi!.Ndo utajua wasomi wapo ila wanajichimbia home au kwenye cafe za internet.
 
Nitarudi
 
Kwahyo uchunguz wako ulikwambia wenye shahada tangu 2015 wameajiriwa wote au sijaelewa?
 
watu wakijaa pomoni si unajua maana yake mkuu?
Yaani wamezagaa kila mahali

Kuhusu kutuma maombi wingi wa wasomi ni kutokana na nafasi zinazotangazwa kuwa chache, ukitaka kujua wingi wa wasomi unachoangalia ni uwiano wa wasomi na wasiosoma ndani ya familia, kwenye jamii, kwenye huduma za kijamii kama kanisani, misikitini, hospitalini, mahakamani, Benk nk
 
Sijazungumzia suala la ajira hapa,
Ila nazungumzia ishu ya wingi wa wasomi kwenye jamii ni tofauti na jinsi usemwavyo.

Wanasiasa wanatumia Propaganda hiyo ili kuzembee katika suala la kuajiri vijana.
 
watu wakijaa pomoni si unajua maana yake mkuu?
Yaani wamezagaa kila mahali

Kuhusu kutuma maombi wingi wa wasomi ni kutokana na nafasi zinazotangazwa kuwa chache, ukitaka kujua wingi wa wasomi unachoangalia ni uwiano wa wasomi na wasiosoma ndani ya familia, kwenye jamii, kwenye huduma za kijamii kama kanisani, misikitini, hospitalini, mahakamani, Benk nk
Wasomi wapo mkuu inategemea ni vijiwe vya aina gani huwa unafanya huo uchunguzi,msomi ashinde vijiwe vya stand kufanyeje?Pitia kwenye mofisi au Njoo Mtumba Dodoma kwenye ofisi za wizara au sasa hivi njoo bungeni kwa sasa uone wasomi wanavyohaha kuwatafuta waheshimiwa wawafanyie mipango ndo utajua wapo wasomi wanahangaikia ajira.
 
Ulicholenga haswa ni kipi ndugu!?

Kuna watu wanakimbia wajibu wao mkuu
Wasomi wapo mkuu inategemea ni vijiwe vya aina gani huwa unafanya huo uchunguzi,msomi ashinde vijiwe vya stand kufanyeje?Pitia kwenye mofisi au Njoo Mtumba Dodoma kwenye ofisi za wizara au sasa hivi njoo bungeni kwa sasa uone wasomi wanavyohaha kuwatafuta waheshimiwa wawafanyie mipango ndo utajua wapo wasomi wanahangaikia ajira.

Unafahamu wenye dhahada moja hapa Tanzania na Diploma hawafiki milion 2?
 
Mkuu mwaka jana walipotangaza NEC nafasi za kusimamia Uchaguzi mkuu ungejaribu kupita pale uwanja wa Taifa ungeona raia waliyokuwa wamejaa kugombea kuingia ndani kwa ajili ya usahili mpaka nguvu ya ziada kutoka JKT na polisi ikatumika.
 
kweli mkuu huo ni ubunge tuu,je udiwani?
 
Back
Top Bottom