Sasa kama mtu unaweza ukapatiwa chanjo ya COVID na bado uko kwenye hatari ya kupata COVID na pengine kupoteza maisha kwa COVID sasa mantiki ya chanjo ni ipi.....??
Chanjo haikufanyi usiambukizwe bali ni kinga ya ugonjwa ukiupata usidhurike,mbona pia wapo watu ambao wana chanjo ya surua but waliugua surua? wapo wenye chanjo ya TB na waliugua TB?
 
Yaani Gwajima ndio wa kupingana na Kauli ya Amiri Jeshi Mkuu? Eti Askari wasichanjwe? Eti Madaktri wasichanjwe? Eti Rais amepokea pesa ili akubali Chanjo?
Ile chanjo ni hiari na hata Rais kasema hilo. Pia Serikali imeshadeclare kwamba unachanjwa at your own risk na litakalokukuta, usimuulize mtu.

Kamsikilize vizuri Gwajima. Hapingani kindezi tu. Ametoa sababu zake ambazo wataalamu wetu wa afya wanapaswa kutolea maelezo na sio kubwabwaja huku JF
 
Kwanini mambo makubwa na ya msingi kama chanjo yanaachwa na kuzungumziwa na watu ambao hawana taaluma ya utabibu?

Halafu kwanini mtu anatisha madaktari kuwa watakufa kama wataiunga mkono hiyo chanjo wakati huyo mtu siyo daktari?, huu si ni uganga wa kienyeji!

Sitaki kuamini kuwa eti Serikali imekuwa katili kiasi hicho kwa wananchi mpaka iruhusu chanjo yenye sumu ya kuwaua raia. Hapana serikali ya namna hiyo haipo duniani.

Naomba Serikali itoe tamko juu ya upotoshaji huu unaofanywa kwa makusudi kabisa. Watanzania wengi wataaminishwa huu uongo.
 
Samahani Mwmeshimiwa, Tukichanjwa hatupati korona??
Tukichanjwa hatuvai mask???
Hata ukipata jabs tatu, lazima uendelee kuvaa mask. Ukicheza vibaya tena, corona inakutandika tena na tena. Hakuna mwenye uhakika hizo chanjo zitaisha lini nguvu (kama zinazo) ili ukachanjwe tena

Sasa sijui kazi ya hizo vaccines ni nini?
 
Hakika mkuu tunataka muongozo na maelezo kwa wataalamu wetu wa afya kuhusu usalama wa hii chanjo miili yetu isiwe majaribio
 
Askofu wa wajinga.
 
Samahani Mwmeshimiwa, Tukichanjwa hatupati korona??
Tukichanjwa hatuvai mask???
Mkuu wangu.....

Kazi ya hiyo chanjo ni kuushtua mwili uzalishe KINGA ya kupambana na UVIKO ...kila binadamu ameumbwa tofauti na hata nguvu ya zile kinga zinazozalishwa/kushtuliwa huwa pia ziko tofauti(potency).....

Kwa hiyo unapochanjwa haina maana kuwa huwezi tena kuupata huo UGONJWA...mathalani ukipata tena UVIKO kwa mara ya pili ,tatu ,nne ,tano hapo MWILI WAKO utakuwa na "kumbukumbu" ya kupambana ile mara ya kwanza kwa hiyo hautaweza kupata MADHARA MAKALI Kama yale yaliyokupata mwanzo.......

Hoja ya kuvaa ama kutokuvaa mask unaweza kupata mifano tele.....mathalani tuwatazame waingereza katika mashindano ya "EURO"....baada ya kuitikia mwito wa KUCHANJWA waliruhusiwa kuingia VIWANJANI(WEMBLEY)bila ya BARAKAO(haikuwa shuruti).....

Kwetu sisi hapa ,tuko zaidi ya milioni 60(jumla na watoto)....Sasa chanjo iliyopokewa kwa kuanzia ni milioni 1 tu....hata wakichanjwa wote milioni 1 bado wengi watabaki bila ya chanjo sasa tunawakingaje HAWA?!!!

USHAURI WANGU: Kwa kipindi hiki TUVAE BARAKOA KWA "WALE" AMBAO HAWAJACHANJWA

#TujiandaeKuchanjwa
#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Hata ukipata jabs tatu, lazima uendelee kuvaa mask. Ukicheza vibaya tena, corona inakutandika tena na tena. Hakuna mwenye uhakika hizo chanjo zitaisha lini nguvu (kama zinazo) ili ukachanjwe tena

Sasa sijui kazi ya hizo vaccines ni nini?
Sawa mkuu.....

Mathalani chanjo dhidi ya PEPOPUNDA huwa ni moja tu?!!!
 
Sababu kila MTU anaweza kutoa sababu, hata hivyo mambo ya corona si mlisema ni waziri ndio anapaswa kuongelea? Take it or not huyo msukuma atakuja kuwagharimu
 
Sababu kila MTU anaweza kutoa sababu, hata hivyo mambo ya corona si mlisema ni waziri ndio anapaswa kuongelea? Take it or not huyo msukuma atakuja kuwagharimu
Wewe nenda kachome. Asiyetaka kuchoma maamuzi yake yaheshimiwe. But fact is, aliyechanjwa na ambaye hajachanjwa wote watapigwa na corona tu wakicheza vibaya
 
Msimamo wa Gwajima kama mtumishi wa Mungu tangu enzi za Mwendazake ulikuwa unajulikana na ndio huo huo , msijaribu kupotosha!
 
Gwajima yeye sasa atupe solution ya Tatizo..watalaam wametengeneza chanjo kwa uwezo wao kunusuru watu wasife na kuugua..Gwajima anaipinga chanjo na kutuambia tusichanjwe huku tatizo lipo linamaliza watu kila siku, atupe basi yeye solution watu wasife au kuugua...
 
Mbona yule rabi wa kiyahudi wa kiothodox kaichana chanjo waziwazi na kusema inageuza watu mashoga ni mbinu ovu hajashambuliwa na wayahudi wenzake? Halafu hukohuko wamekazana na chanjo mpaka ya vidonge wametengeneza. Gwajima ana haki ya kutoa maoni kwa chanjo inayotiliwa mashaka dunia nzima.
 
tunategemea serikal ibane viongozi wangemtoa kwenye ubunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…