Protokali ya Mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu ipoje?

Kazi maalum na asiyekuwa na wizara maalum ni sawa tu. Waziri una wizara au huna mengine ni mbwembwe tu. Kaka yangu mkuchika hana wizara.
Mkuu With all Due Respects!
naomba Nikueleweshe tena..
mkuchika Ni waziri wa nchi ofisi ya Rais yaani "Ministry of State President office for special work."

Ila kwa Amiri alikuwa ni "Minister without Portfolio"

Unaona hayo maandishi na hizo kazi ziko sawa?.... Minister of state in president office for special work na "Minister without portfolio"
Wanalingana?
kama ukisema wanalingana bhasi kuna kitu kwako Hakiko sawa
 
Without portfolio huenda ikasomeka mzurururaji haipendezi, special work or duty sounds better lakini bado hana portfolio. Anaejua huyu anafanya kazi gani ni raisi tu.
 
Without portfolio huenda ikasomeka mzurururaji haipendezi, special work or duty sounds better lakini bado hana portfolio. Anaejua huyu anafanya kazi gani ni raisi tu.
Hahahaha Nimeuliza una ufahamu wa hizi katiba..
  • Katiba ya Uhuru ya mwaka 1961..
  • Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika 1962
  • Katiba ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanganyika Na Zanzibar ya mwaka 1964
  • Katiba Ya Jamhuri Ya muungano wa Tanzania ya Mwaka 1965
Hizo katiba ndo zinaeleza kazi ya Waziri ambaye hana portfolio
 
Nimeziishi zote.
 
Nimeziishi zote.
Bhasi kama umeziishi Utakuwa unajua kuwa Hiyo Wizara ilikuwa ni sawa na waziri Mkuu kabla ya Kuwekwa Cheo cha Naibu waziri Mkuu..
Kipindi cha Utawala wa Mwinyi "mwanzoni"
Baada ya Katiba ya Kudumu ya mwaka 1977 kutengenezwa ilibdi kila waziri atambulike wizara yake..
Na nafikiri Historia ya Naibu waziri mkuu unaijua vizuri..
 

Anazikwa kwao Monduli...

Utaratibu utafuata protokali za serikali kupitia kamati ya mazishi ya serikali wakishirikiana na taratibu za familia...

Mwili utaagwa Karimjee na KKKT Azania Front kwa Dar es Salaam, utapelekwa na helikopta ya Jeshi Arusha, utaagwa uwanjani pale Sheikh Amri Abeid, utapelekwa Monduli na kuagwa tena na mwisho maziko...
 
Hua napambana sana huyu hakustaafu🤣 au lugha inatuzingua maana medi nazo sinasema mstaafu
Kwani nini maana Ya kustaafu..
Kama angetumbuliwa Uwaziri wake Tusingemuita Mstaafu ila Kiprotokoli aliamua kulinda heshima yake na serikali kujiuzuru ili kupata stahiki za mstaafu..

Kwa mfano..Mtumishi akiomba Kustaafu mwenyewe baada ya Miaka 55 ni sawa na kusema kujiuzuru serkalini na atapata stahiki zake na ataitwa Mstaafu ila ikitokea akafukuzwa akiwa na miaka 58 jina mstaafu hatalipata Hata kidogo..

So kiprotokali Anastahili kuitwa hivyo
 

Hatazungushwa mkuu...

Msiba utakuwa Dar, Arusha mjini na kwao Monduli...
 
Shukrani mkuu, kuna document yiyote tunaweza rejea?
 
Kiprotokali kwa kuwa bado serikali huendelea kuwahudumia viongozi wakuu wa nchi kila kitu hadi ulinzi, basi hakuna shaka yoyote kuwa serikali pia itagharamia maziko yao popote pale familia zao zitakapotaka.

Ila mara nyingi viongozi wetu wana kwao hivyo watazikwa kwao walikozaliwa.
 
Majibu:

1. Hakuna sheria ya kumzika kiongozi yeyote Dodoma iliyopitishwa na Bunge. Maamuzi ya mahali gani mtu aliyekuwa kiongozi wa umma ktk ngazi na madaraka yoyote yanabaki kuwa ni ya familia husika..

2. Protocol ya mazishi ya mtu ambaye amewahi kushika au amekufa na wadhifa/madaraka ya Waziri Mkuu hayana tofauti kubwa na mtu wa ngazi ya Vice President...

3. Kubwa na muhimu wewe kuelewa ni hili, kwamba, kuzikwa ni lazima atazikwa kwa heshima na protokali yote ya kiserikali. Mfano tayari imeshatangazwa siku 5 za maombolezo kitaifa na bendera ya taifa kupepea nusu mlingoti...
 
Kama nikutokuwa na wizara Maalumu mbona wapo wengine?Muondoe tu huyo muhindi hajawahi kuwa Waziri Mkuu

Sent from my SM-A107M using JamiiForums mobile app
 
Zanzibar mbona hauletwi mwili. Masai tupo wengi huku
 
Amir Jamal hakuwa mzungu alikuwa mhindi na alitumika kama waziri wa fedha.mzungu alikuwa Bryson waziri wa kilimo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…